Ndugu zangu wana JF,
Mimi kijana mwenzenu naomba kuchukua nafasi hii kuomba kujuzwa gharama halisi za kuandaa sherehe ya harusi,
Nimeona nitumie jukwaa hili kwa kuamini ya​ kwamba nitapata maoni na taarifa kutoka kwa watu ambao wameshapita kwenye hatua hii na pia itakuwa msaada kwa ambao wanajiandaa kuingia kwenye hatua hii kama mimi,nimekuwa kwenye mahusiano na mwenzangu kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu sasa na sio kwamba muda wote huo nilikuwa sitaki kuoa ila kila nikifikiria gharama za sherehe zinanikwamisha hasa nikiangalia kipato changu,nimekuwa nikisema ngoja nisevu pesa kwaajili ya jambo hili lakini mwisho wa siku yanatokea mambo yanaharibu mipangilio yangu.
Kwa sasa nimeona liwalo na liwe, nimepanga kuoa mwakani mwezi wa tisa Mungu akipenda, kwahiyo kwa kutumia jukwaa hili naomba kujuzwa bajeti ambayo inatosha kuandaa sherehe ya kawaida ambayo tunaweza tukajumuika na kufurahi ambayo haitakuwa na mbwembwe nyingi kwa maana ya kwamba mimi kama bwana harusi nahitaji kuwa na kiasi gani?
Maana nikiangalia uwezo wa familia na watu wa wangu wa karibu ni mdogo,maana nataka niangalie kama naweza ningependa nusu ya gharama ya bajeti nijigharamie mwenyewe,natumini nitapata maelekezo chanya kwa maana ya wapi nitapata ukumbi,mc,vinywaji,nakadhalika ambavyo vitakuwa standard lakini kwa bei ya kawaida.
Kwa ufupi ni hayo,kama kuna makosa ya uwasilishaji na uandishi mtanisahihisha.
Naomba kuwasilisha kwenu
NB,gharama ziwe za sherehe ya ukumbini