Gharama za sherehe ya harusi

Gharama za sherehe ya harusi

Nimeshuhudia sherehe moja rafiki yangu aliifanya kwa milion 10. Ilifana sana na vitu vyote basic vilikuwepo. Ilikuwa na guests 200
 
Ukileta swali kama hili humu jf huwezi pata majibu wala kwa jamii yetu hupati majibu.

Hii siyo kama bei ya godoro No.

Kwanza watz wengi ktk sherehe hizi tunafanya kwa kujikweza ili tuonekane asiye na uwezo snalazmisha uwezo.

Harusi inaweza hata kugharimu 20,000 tu yaani hela ya taksi to-from hom.ikishabarikiwa na shekh au pastor imekwisha mengine showoff.
Wewe ndugu yangu ushaoa?au kuolewa?ghalama ilikuwa 20,000/=?
 
Nafahamu hilo lakini najua hata ingekuwa wewe usingekubali
mimi nimeshaamua hivyo na ndilo nitakalofanya .. sipotezi muda kushurutisha watu wanaishangie ili nifanye harusi ... wakati tendo muhimu pale ni kufunga ndoa .. mimi harusi hapana
 
Rafiki kwanza nipe idadi ya watu unaopenda wawepo kwenye sherehe then nikupe mchanganuo
 
kama unayo M 3 unaweza ukafanya na ikafana kabisa, unahitaji upate watu waaminifu ili wasimamie hyo shughuli yako,
 
wengi tunaandaa mambo ya nje nivae shela harusi kubwa ... tunaandaa kufurahisha jamii huku tukisahahu kujifanyia evaluation in detail je kweli moyo wangu upo tayari kuishi na huyu binti na je nitamvumilia mangapi kwa mda gani? na je yeye kajiandaa kiasi gani kukubaliana na mapungufu yangu? na je ni kweli kuna chemistry between you too au mnaoneana huruma au mnafanya tu bila kujua kwa nini mnafanya? lingine mmemtanguliza Mungu kiasi gani katika kusimamia ndoa yenu au Mungu anapewa nafasi ndogo ndiyo maana hata kwenye kadi mnawaambia watu mkutane ukumbini huku tendo muhimu la ibada hamataki jamii ishiriki ,, na pia ninyi mpo pale kama misanamu tu huku mkiwa na mawazo sijui ukumbini kumepelea nini? sijui mtu wa keki kafika ? sijui kamati imekaaje?

muhimu ni kuandaa mioyo zaidi kuliko sherehe za masaa mawili wakati ndoa ni maisha ..........

hakika umenena tena busara tupu tulio wengi huwa tunakurupuka tu psychologicaly hatujajiandaa kuishi kwa uvumilivu kwenye ndoa siku mbili tatu ndoa haipo.
 
Wewe ndugu yangu ushaoa?au kuolewa?ghalama ilikuwa 20,000/=?

Nishaoa mkuu ila ukitaka kufanya kama watu wanavyotaka utaishia kumaliza sherehe na kuanza kudeal na madeni.fanya kadiri ya uwezo wako mkuu.
 
Nimeshuhudia sherehe moja rafiki yangu aliifanya kwa milion 10. Ilifana sana na vitu vyote basic vilikuwepo. Ilikuwa na guests 200

Duuu 10 millions si mtaji kbs huo wa biashara? How come u spend 10 millions kwa kitu cha masaa kumi tuu?
Unamaliza harusi for ten million then bank account inasoma 20000 Tshs ya kutunzia account.
 
harus ya kazi gani.

Ikumbukwe harusi ni sherehe baada ya ndoa so harusi si lazima cha muhimu padre,pastor au sheikh abariki ndoa then nenda hom epuka madeni yasiyo ya msingi.

nakubaliana na wewe lakini mwenzangu hawezi kukubali hilo,ni wachache sana wanaokubali ndoa bila sherehe hasa wanawake
wakiona wenzao wameolewa kwa sherehe tena kubwa tu.
 
Nimeshuhudia sherehe moja rafiki yangu aliifanya kwa milion 10. Ilifana sana na vitu vyote basic vilikuwepo. Ilikuwa na guests 200
Ningepata bajeti kama ya hiyo,ingenisaidia pakuanzia.
 
Duuu 10 millions si mtaji kbs huo wa biashara? How come u spend 10 millions kwa kitu cha masaa kumi tuu?
Unamaliza harusi for ten million then bank account inasoma 20000 Tshs ya kutunzia account.

Unachosema ni kweli lakini kama ungekuwa wewe ungefanyaje?
 
Nishaoa mkuu ila ukitaka kufanya kama watu wanavyotaka utaishia kumaliza sherehe na kuanza kudeal na madeni.fanya kadiri ya uwezo wako mkuu.

Ndo najitahidi nifanye kwa uwezo wangu japo ingekuwa ni uamuzi wangu tu nisingetaka sherehe au sherehe ingesubiri mpaka niwe na uwezo wakuigharamia kama sio yote basi kwa kiasi kikubwa.
 
mimi nimeshaamua hivyo na ndilo nitakalofanya .. sipotezi muda kushurutisha watu wanaishangie ili nifanye harusi ... wakati tendo muhimu pale ni kufunga ndoa .. mimi harusi hapana
Natamani wote tungekuwa na akili kama yako.
 
Sherehe ya watu 250, inaweza kukucost 10-12M, na inakuwa sherehe ya kawaida tu..
 
Back
Top Bottom