Gharama za safari na mapumziko Zanzibar

Gharama za safari na mapumziko Zanzibar

WanaJF!!

Ninategemea kuanza likizo ya siku 28 hivi karibuni. Katika plan yangu ninatarajia kwenda Unguja kwa mapumziko ambapo nitakaa kwa juma zima.

Msaada ninaohitaji kutoka kwenu ni huu:-
(i) Minimum na maximum ya bei ya nauli za boti
(ii) Gharama za hoteli hu-range kuanzia bei gani? Mfano, kwa mji kama Mwanza, Arusha na Dodoma, Tsh 25,000 to 30,000 unapata chumba Standard kabisa.
(iii) Gharama ya taxi (town trip) ni bei gani?
(iv) Gharama ya chakula ikoje?

Nisaidieni ili nijue kama nitamudu au lah!!!
(1)gharma ya boti minimu tsh 23,000/= maximum(VIP) tsh 35,000/=
(2)room za hotel jipange kuanzia tsh 40,000-usd900
(3)tax 5000
(4) depend on ur on initative ila ni kawaida kama hotel za dar au mwanza but kuna some slight diference
ur most welcome to spice island(zanzibar yetu ni nzuri sana atakae kuja na aje):frusty:
 
MKUU kama unaenda kwa mapumziko kweli nakushauri usiishie stone town ! Nenda Nungwi! Kutoka stone town hadi Nungwi watakushika Dola hamsini kwa tax, kama ukipanda chai Maharage ni kwenye elfu 2500 hadi 4000!
Ukifika Nungwi kuna beach hotels nyingi, kama Amaan Bungalows, hapa kidogo ni ghali, chumba ni kuanzia dola 70 hadi 150 kwa siku, lkn kuna Nungwi in! Hapo mm ndio nafikiaga mara kwa mara. Bei zao ni mpaka dola 35 kwa night! Kama ukitaka kwenda naweza kukupatia contacts zao!
Chakula ni kuanzia elfu 9 nakuendelea inategemea na aina ya chakula!
Ukiwa huko utasahau mihangaiko yako yote wewe ni kula bata tu!

Hali ya uchumi kama itaruhusu, nitakwenda pia Nungwi. Tupe contact mzee
 
Nakushauri ulale BARASTE Lodge,bei ya single ni 35,000/=,gharama za taxi ni kubwa ungekuwa mzoefu ningekushaur self drive z cheaper!
 
Hivi hapo Zenji wale dada poa kama wa Corner Bar na mnyama wa taifa a.k.a mdudu wanapatikana wapi?
 
Poa unaweza kufukia uroa,ni east coast.kuna samaki lodge na palumbo reef.unaweza pata chumba kwa elfu arobaini,vyakula kwa kuanzia elfu kumi.
Ni pazuri kwa kufikia kama una mapumziko.

Sent from my BlackBerry 9380 using JamiiForums
 
shukrani sana wana jf maana mmetusaidia wengi humu ila mwenye kupafahamu vizur huko atuelezee kimapana bei mbalimbali za logde na hotel za huko.
 
kama unaenda na shemeji akikisha avai vimini asije mkuta ya wale wazungu bure

#kunjani kuti
 
Hivi hapo Zenji wale dada poa kama wa Corner Bar na mnyama wa taifa a.k.a mdudu wanapatikana wapi?

forodhani pale utawakuta mpaka wakaka poa ukiwa macho juu juu unaweza opoa dume mwenzako ukidhani binti mbichi
 
Mkuu, mimi nimetoka znz juzi kula bata kama wewe. Niliingia jumamosi asubuh na shemej yako na kurudi juma tatu jioni.
Nilikaa Shangani hotel. kati kati ya mji mkongwe. Chumba nilichukua cha 55,000 kwa siku. Yaani kuenda forodhani unatembea tu kwa mguu ni dakika mbili kwa mwendo wa maringo. Forodhani ni kama garden jioni kuna mavyakula kibao mpaka urojo

Cha muhimu zanzibar, kabla hujanunua chochote uliza kwanza bei. Ukila au kupata huduma bila kuuliza unapigwa za juu mpaka ukome

Nilitafuta guide wa kishkaji akanizunguusha mji mkongwe wooote aka stone town. Beit el ajaib aka house of wonders, slave market, palace musium, kaburi la tip tip, jumba la watoto yatima, ngome kongwe

Mwisho akanipeleka mpaka kule wanaita darajani akaniacha huko nikawa nazurura tu.
Hii mizunguko yote niliianza saa tano asbhi kufikia saa kumi jioni nimeua
Mshikaji nikampa buku 15 tu.

Siku ya pili yake nikachukua dau sijui ngalawa nikaenda kwenye kisiwa kinaitwa Prison island. Kule kuna kobe aka tortoise wenye umri mpaka miaka 200 na niwakubwa balaa. Then nikamalizia hapohapo kuogelea na shemejio ndio huyu mwenye kidau sijui kingalawa akaturudisha stone town. Ni kasafar ka 25minutes. Very fun. Na tulikaa huko prison islnd masaa matatu. Tumemlipa shs 30,000.

Sikuya mwisho tukamalizia palace musium, hapo hapo kuna ma guide unampa buku 5 kishkaji coz serekal inamlipa. Kote huku ni walking distanca

Mnamo saa 1000 tukajimuvzisha kwa mguu hadi bandarini tukakata ticket boat za azam vip saaafi kabisa shs 35,000 kwa kichwa. Tukarud hotelini kwa mguu tukachukua mabegi tukaenda bandarini kwa mguu kwa kua tickt ni vip tukakaa waiting roooom ya vip huko tukala na kunywa vilivyopo for free but with limt kimoja kimoja. raha sana.
Kwenda kula tulikua tunaenda Malindi kutoka hapo hotelini kwa shs elfu nne bei ya tax. huko malindi kuna hotel maarufu kwa biriani inaitwa Passing show.

Uzuri wa Shangani hotel ni walking distance mambo mengi.

Nb: Chuku boti za asubuhi au jioni sana coz mchanna nilichemka shemeji yako hakuhimili rough sea na mawimbi but for me it was fine n fun. Mida nlokushauri bahar si chafu. Asanteeeeee
 
MKUU kama unaenda kwa mapumziko kweli nakushauri usiishie stone town ! Nenda Nungwi! Kutoka stone town hadi Nungwi watakushika Dola hamsini kwa tax, kama ukipanda chai Maharage ni kwenye elfu 2500 hadi 4000!
Ukifika Nungwi kuna beach hotels nyingi, kama Amaan Bungalows, hapa kidogo ni ghali, chumba ni kuanzia dola 70 hadi 150 kwa siku, lkn kuna Nungwi in! Hapo mm ndio nafikiaga mara kwa mara. Bei zao ni mpaka dola 35 kwa night! Kama ukitaka kwenda naweza kukupatia contacts zao!
Chakula ni kuanzia elfu 9 nakuendelea inategemea na aina ya chakula!
Ukiwa huko utasahau mihangaiko yako yote wewe ni kula bata tu!
Mkuu usiende Nungwi kama hutaki kukaa katikati ya Darajani,huko wamejaa wauza sembe na ma kaka poa,nenda Breeze Beach Club & SPA kule Bwejuu ukale Likizotime. Ukiwa njiani utapita kwenye hifadhi ya Jonzani {sio ule mtaa wa wajanja pale mjini} hapo utaona kima wajanja aka kima punju,wao kukukatikia taarabu mbona simple! Yaani kama unaenda na shem mwambie ajiandae kuhudhuria klinik kwani najua matokeo yatakuwa mazuri tu. Kitu kingine unapoamua kusipendi mambo ya pesa au gharama tupa kuleee kuna hotel ukiuliza bei wanakwambia upishe/uanze mdogomdogo.
 
ukitaka kupumzika basi usilale hotel ya elf 30 au 40, kwani sio nzuri sana, hasa kwa zanzibar hotel ni ghali kidogo..chumba cha elf 30 sio kizuri saaaaana kwa mapumziko, kinafaa km umeenda kikazi..
unapoenda kupumzika unatakiwa upumzike kweli, na uinjoi likizo yako..sio unaenda hotel, maji hamna, au shuka mbofu mbofu, kachumba kodgoo, haina maana ni bora ukae home kwako ambako ni pazuri...

alafu wiki ni kubwa siku 3 zinatosha kabisa, zanzibar sio kubwa sana na wala hakuna masehemu meeengi ya kutembea(kwa mtizamo wangu) kwa ivo unaweza kujikuta umeboreka kama umelipia hotel kwa wiki, bora ulipie siku 3 kwanza... usiku usiache kwenda forodhani, ni pazuri kwa vyakula na kupunga upepo

nakutakia mapumziko mema, hope utakuwa na mwenzi wako..enjoy your holiday

we ni kamusi kweli..hadi na mm
nimeshawishika kwenda
 
Mkuu ukienda zbar usiache kufika NUNGWI kule ndio wa starehe za dunia ni pazuri ajabu.unaweza kwenda kwa kukodi gari self driving au kwa hiace.
vyakula bei nzuri na hata pa kulala kutokana na hela yako.
Jamani kwani kasema anaenda kuuza sembe? Au sijamwelewa? Kasema anaenda likizo sasa Nungwi akafanye nini? Au MV SPICE ISLANDER ilishatolewa majini? Ndugu usirubunike na hawa jamaa,sepa zako kusini hasa maeneo ya Paje,Bwejuu na Makunduchi {sio tusi mh},Michamvi lakini ujue basi japo Kitaliano kidogo mfn; fulakulo nk.
 
Hata wewe "kishuka"?! Makubwa!

mbona unatolea lugha ya kuudhi? kishuka ni wale wazungu choka mbaya wanaokuja kutalii afrika unakuta wanashidia ndizi mbivu mkate na maji pale forodhani baada ya kutembea umbali mrefu
 
Jamani kwani kasema anaenda kuuza sembe? Au sijamwelewa? Kasema anaenda likizo sasa Nungwi akafanye nini? Au MV SPICE ISLANDER ilishatolewa majini? Ndugu usirubunike na hawa jamaa,sepa zako kusini hasa maeneo ya Paje,Bwejuu na Makunduchi {sio tusi mh},Michamvi lakini ujue basi japo Kitaliano kidogo mfn; fulakulo nk.
Mkuu likizo moja nilienda Paje! Nakumbuka nilikaa hotel wanaiita Paje by night kama sijakosea, tatizo ni lile eneo la beach lenyewe, sio pana sanai! Lkn beach ya Nungwi nimeipendea mchanga wake na upana wa beach yenyewe! Sijafika Bwejuu na Makunduchi, labda likizo ijayo nikajaribu huko hasa kwenye hao kima punga!
 
Nashukuru wa jf tumefaidika wengi,Me ninataka kuoa,natarajia nitakuwa huko kwa mapumziko,naomba kujua bei ya Ndege,kutoka Kilimanjaro to Zenji ni pesa ngapi?
 
WanaJF!!

Ninategemea kuanza likizo ya siku 28 hivi karibuni. Katika plan yangu ninatarajia kwenda Unguja kwa mapumziko ambapo nitakaa kwa juma zima.

Msaada ninaohitaji kutoka kwenu ni huu:-
(i) Minimum na maximum ya bei ya nauli za boti
(ii) Gharama za hoteli hu-range kuanzia bei gani? Mfano, kwa mji kama Mwanza, Arusha na Dodoma, Tsh 25,000 to 30,000 unapata chumba Standard kabisa.
(iii) Gharama ya taxi (town trip) ni bei gani?
(iv) Gharama ya chakula ikoje?

Nisaidieni ili nijue kama nitamudu au lah!!!

Kama utakuwa umeenda na shemeji yetu basi usisahau Cheti cha Ndoa, vinginevyo mtazunguka sana kupata mahali pa kulala ambapo mtalazimika kwenda kwenye hoteli za kitalii ambapo0 nyingi ni gharama sana
 
Mkuu, mimi nimetoka znz juzi kula bata kama wewe. Niliingia jumamosi asubuh na shemej yako na kurudi juma tatu jioni.
Nilikaa Shangani hotel. kati kati ya mji mkongwe. Chumba nilichukua cha 55,000 kwa siku. Yaani kuenda forodhani unatembea tu kwa mguu ni dakika mbili kwa mwendo wa maringo. Forodhani ni kama garden jioni kuna mavyakula kibao mpaka urojo

Cha muhimu zanzibar, kabla hujanunua chochote uliza kwanza bei. Ukila au kupata huduma bila kuuliza unapigwa za juu mpaka ukome

Nilitafuta guide wa kishkaji akanizunguusha mji mkongwe wooote aka stone town. Beit el ajaib aka house of wonders, slave market, palace musium, kaburi la tip tip, jumba la watoto yatima, ngome kongwe

Mwisho akanipeleka mpaka kule wanaita darajani akaniacha huko nikawa nazurura tu.
Hii mizunguko yote niliianza saa tano asbhi kufikia saa kumi jioni nimeua
Mshikaji nikampa buku 15 tu.

Siku ya pili yake nikachukua dau sijui ngalawa nikaenda kwenye kisiwa kinaitwa Prison island. Kule kuna kobe aka tortoise wenye umri mpaka miaka 200 na niwakubwa balaa. Then nikamalizia hapohapo kuogelea na shemejio ndio huyu mwenye kidau sijui kingalawa akaturudisha stone town. Ni kasafar ka 25minutes. Very fun. Na tulikaa huko prison islnd masaa matatu. Tumemlipa shs 30,000.

Sikuya mwisho tukamalizia palace musium, hapo hapo kuna ma guide unampa buku 5 kishkaji coz serekal inamlipa. Kote huku ni walking distanca

Mnamo saa 1000 tukajimuvzisha kwa mguu hadi bandarini tukakata ticket boat za azam vip saaafi kabisa shs 35,000 kwa kichwa. Tukarud hotelini kwa mguu tukachukua mabegi tukaenda bandarini kwa mguu kwa kua tickt ni vip tukakaa waiting roooom ya vip huko tukala na kunywa vilivyopo for free but with limt kimoja kimoja. raha sana.
Kwenda kula tulikua tunaenda Malindi kutoka hapo hotelini kwa shs elfu nne bei ya tax. huko malindi kuna hotel maarufu kwa biriani inaitwa Passing show.

Uzuri wa Shangani hotel ni walking distance mambo mengi.

Nb: Chuku boti za asubuhi au jioni sana coz mchanna nilichemka shemeji yako hakuhimili rough sea na mawimbi but for me it was fine n fun. Mida nlokushauri bahar si chafu. Asanteeeeee

Umemaliza kila kitu, ila next time ukija jaribu kutembelea shamba pia (Nungwi na maeneo mengine ya beach). Staili yako inafaa sana kwa budget zetu na bado unafurahia vitu vingi. Huko usiende kulala, unaenda na kurudi stone town.
 
Kama utakuwa umeenda na shemeji yetu basi usisahau Cheti cha Ndoa, vinginevyo mtazunguka sana kupata mahali pa kulala ambapo mtalazimika kwenda kwenye hoteli za kitalii ambapo0 nyingi ni gharama sana
Usimtishe bana mbona watu wanapuyika tu huku bila taabu,akija atuone wakuu ,tutamtoa tongotongo za macho atainjoi tu!
 
Back
Top Bottom