Gharama za kuwekewa umeme

Gharama za kuwekewa umeme

Ndugu mteja,

Tunakushukuru kwa kuelewa maelekezo yetu. Tunaomba utupatie namba ya ombi/namba ya simu iliyotumika kuwasilisha ombi hilo au namba ya malipo ili tuweze kufuatilia taarifa za ombi hilo na kukupatia msaada zaidi.

Asante kwa kuwasiliana na TANESCO Huduma kwa Wateja. ^RS
Kama hauko smart kwenye mitandao utatekwa usitoe huo utambulisho.
 
Mambo sio salama kutoa taarifa zako kiboya boya hata kama unashida ya umeme. Tunaongozwa na Mafia families Mexican cartels na mafioso.
 
Kuna mdau aliniambia Maximum ni nguzo mbili kwa mteja kulipia nguzo ambayo ni 690k kitu kama hicho, ikitokea zinakuwa zaidi ya nguzo 2 ilo eneo inahitajika kufanyiwe mradi kama wanavyosema na issue ya mradi ina involve mambo mengi kama kuongezeka kwa manpower, vifaa, aina ya usafiri na mambo ya VAT
Hivyo inabidi mteja asubiri Wao walete mradi eneo husika ambapo kama budget ya mwaka huo ipo, akireport ofisin kwao watatenga budget then atajengewa mradi kazi yake itakuwa kulipia tu 320k na kuwasha umeme.

Lakini kama mteja anaharaka zake ndio anapewa gharaman zote na hizo gharama nahisi haziko constant zina vary kulingana na umbali wa eneo na mambo mengine wenyewe wanajua
 
Mtanzania bwana akijenga nyumba huiita kibanda eti nna kakibanda KANGU. Umekuwa kuku? Jiamini sema nna nyumba yangu sio nna kibanda changu.
Wewe ukisema una Nyumba ,je Chivayo ,Rick Ross ,50 cent ,Lugumi ,GSM ,Samuya nao waseme wana nini?

Umepanga tofali zako elfu 3500 na ina sqm 144 kwenye kiwanja cha 20 kwa 20?
 
Habari ndugu mteja,

asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja, tafadhali fanya maombi ili hatua zingine zifuate na uweze kupata huduma.^HN
Mkuu, mie nilishafanya Application imepita miezi miwili sasa, halafu kama wiki 2 zilizopita nilipigiwa simu na TANESCO hapa nilipo wakaniambia watanitumia Control number nilipie waje kufunga umeme ila mpaka muda huu hawajatuma

Hapo inakuaje Sheikh?
 
akikujibu hili la control number nistue..wiki ya 3 sasa inaenda hawajatuma
Mkuu, mie nilishafanya Application imepita miezi miwili sasa, halafu kama wiki 2 zilizopita nilipigiwa simu na TANESCO hapa nilipo wakaniambia watanitumia Control number nilipie waje kufunga umeme ila mpaka muda huu hawajatuma

Hapo inakuaje Sheikh?
 
Kama hauko smart kwenye mitandao utatekwa usitoe huo utambulisho.
Habari ndugu mteja,

Asante kwa kuwasiliana nasi na kwa kutoa maoni yako.

Tunaelewa umuhimu wa kulinda taarifa binafsi. Hata hivyo, taarifa za NIKONECTI hutuwezesha kufuatilia hatua iliyofikiwa katika ombi la mteja, pamoja na matokeo ya vipimo vilivyofanywa na wataalamu wetu.

Taarifa hizi hutupatia ufahamu wa kina kuhusu ombi la mteja na kutuwezesha kutoa msaada stahiki. Bila taarifa hizo, ufanisi wa kufuatilia na kutatua changamoto zinazohusiana na maombi ya kuunganishiwa umeme unaweza kupungua.

Aidha unaweza kutoa taarifa kupitia ujumbe wa binafsi (inbox), ukiachana na ukurasa huu unaweza kutoa taarifa juu ya changamoto yeyote moja kwa moja ukiwasiliana na mtoa huduma wetu kwa kupitia namba 180 (huduma ni bure). asante.^MY
 
Mkuu, mie nilishafanya Application imepita miezi miwili sasa, halafu kama wiki 2 zilizopita nilipigiwa simu na TANESCO hapa nilipo wakaniambia watanitumia Control number nilipie waje kufunga umeme ila mpaka muda huu hawajatuma

Hapo inakuaje Sheikh?
Ila pamoja na mambo yao TANESCO kwenye kuunganisha umeme lately wamenifurahisha. Kuna location mbili baada ya kulipa walinipigia simu baada ya siku 2 wakaja kufunga umeme. Location ingine ambayo ilihitqji nguzo moja nilipia 696k I think hii walichukua wiki mbili tu.
 
Duuh, sasa hili eneo nalozungumzia ni mjini kabisa
 
Mkuu inakuwaje Umbali wa njia tatu zaidi ya mita 120?
Habari ndugu mteja,

Asante kwa kuwasiliana nasi.

Tungependa kukufahamisha kuwa utaratibu haujabadilika, mtaalamu wetu atakufikia kwanza kwa ajili ya kufanya upimaji na ukaguzi eneo linalohitaji huduma ya kuunganishiwa umeme, endapo umbali kutoka kwenye miundombinu ya umeme hadi eneo lako itakuwa zaidi ya mita 120, utashauriwa kusubiri hadi mradi utakapofika katika eneo lako.

Hata hivyo, endapo utakuwa tayari kulipia gharama zinazohusika kabla mradi haujafika karibu na eneo ulipo, wataalamu wetu watakufanyia makadirio ya gharama kulingana na mahitaji yaliyobainika na kukupatia namba ya malipo (control number).

Asante.^MY
 
Mkuu, mie nilishafanya Application imepita miezi miwili sasa, halafu kama wiki 2 zilizopita nilipigiwa simu na TANESCO hapa nilipo wakaniambia watanitumia Control number nilipie waje kufunga umeme ila mpaka muda huu hawajatuma

Hapo inakuaje Sheikh?
Habari ndugu mteja,

Asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto hiyo,

Tunaomba utupatie namba yako ya ombi au namba yako ya simu uliotumia kufanya maombi hayo, ili tuweze kufanya ufuatiliaji juu ya changamoto hii na kukupatia utatuzi na msaada zaidi.

Asante.^MY
 
Ila pamoja na mambo yao TANESCO kwenye kuunganisha umeme lately wamenifurahisha. Kuna location mbili baada ya kulipa walinipigia simu baada ya siku 2 wakaja kufunga umeme. Location ingine ambayo ilihitqji nguzo moja nilipia 696k I think hii walichukua wiki mbili tu.
Habari ndugu mteja,

Asante kwa kuwasiliana nasi,

Tunashukuru kwa kutambua juhudi zetu katika kukupatia huduma bora, tafadhali endelea kufurahia huduma zetu. TANESCO tunayaangaza maisha yako.

Asante.^MY
 
Back
Top Bottom