Habari wakuu, Naomba mwenye uzoefu na hili jambo anipe mwongozo.
Nataka kuweka umeme kwenye kakibanda changu lakini kutoka iliko nguvu hadi kibanda kuna uwezekano wa kuwa na nguzo 3 tatu.
Gharama halisi ya kuingiza umeme inaweza kufika shilingi ngapi? Nimeuliza hivyo kwa sababu napata maelezo tofauti. Asante kwa muda wako
Salama ndugu mteja,
Fahamu kuwa,
•Gharama za kuunganisha umeme ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 320,960/=,
•Mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618/=,
•Umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670/=
•Aidha, gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014/=,
•Mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385/=,
•Umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156/=.
Zingatia
Gharama ya kuunganisha umeme vijijini kwa wateja wa njia moja ni shilingi 27,000/=
Gharama hizi ni kama ilivyoelekezwa na EWURA.
NB: Gharama zote zimejumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) 18%
Zingatia gharama halisi utazipata baada ya wataalamu wetu wa vipimo kufika kwenye eneo lako na kufanya tathmini..^NI