KERO "Gharama za Kumuona Daktari" NI MSEMO ULIOFICHIKA

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ni ukweli kwamba gharama zinazotajwa ili uweze kuonana na daktari hazijawahi kuwa za daktari na waala daktari hajawahi kuzipokea ila ni gharama ambazo zimewekwa ili kusaidia uendeshaji wa huduma za afya na vitu vingine kwenye kituo husika.

Na kama serikali inamaanisha kuwa ni gharama za kumuona daktari basi ziende moja kwa moja kwa mhusika aweze kunufaika nazo maana kwanza analipa pesa ya leseni kila mwaka halafu pesa inayoitwa ya daktari ni anaikusanya tu lakini hanufaiki nayo.

Kuliko kuleta taharuki kwenye jamii kuwa kumuona daktari ni mpaka pesa ilihali pesa yenyewe hajawahi ipata nashauri yawekwe maneno mengine mfano: MEDICAL FEE (ADA YA TIBA) ili kumtoa daktari kwenye hiyo taharuki ya kuwa anapaswa kulipwa hela ndo uweze kuonana naye.
 
Nikashangaa mpaka mbunge mzima anashindwa kuelewa kuwa Consultation fee/Gharama ya kumuona Daktari hapewi Daktari.

Yani Mbunge mzima research ya dakika 5 imemshinda. Ingekuwa consultation fee anapewa Daktari basi Madaktari wasinge ganga njaa mjini
 
Ni ukweli kwamba gharama zinazotajwa ili uweze kuonana na daktari hazijawahi kuwa za daktari na waala daktari hajawahi kuzipokea ila ni gharama ambazo zimewekwa ili kusaidia uendeshaji wa huduma za afya na vitu vingine kwenye kituo husika.

Na kama serikali inamaanisha kuwa ni gharama za kumuona daktari basi ziende moja kwa moja kwa mhusika aweze kunufaika nazo maana kwanza analipa pesa ya leseni kila mwaka halafu pesa inayoitwa ya daktari ni anaikusanya tu lakini hanufaiki nayo.

Kuliko kuleta taharuki kwenye jamii kuwa kumuona daktari ni mpaka pesa ilihali pesa yenyewe hajawahi ipata nashauri yawekwe maneno mengine mfano: MEDICAL FEE (ADA YA TIBA) ili kumtoa daktari kwenye hiyo taharuki ya kuwa anapaswa kulipwa hela ndo uweze kuonana naye.
Kweli kabisa, daktari halipwi hela yoyote na mgonjwa. Ni mshahara tu basi.

Hili la kusema hela ya kumuona daktari limekaa kimtego, linaleta picha kwamba daktari ndiye anayepatiwa hizo hela wakati siyo.
 
Consultation fee. Na ikumbukwe pia kuwa inawezekana mgonjwa akaishia kuonana na dr na shida yake ikapata ufumbuzi.
 
Back
Top Bottom