MOI: Huduma za upasuaji zinaendelea kama kawaida, mwenye changamoto afike ofisini tumsaidie

MOI: Huduma za upasuaji zinaendelea kama kawaida, mwenye changamoto afike ofisini tumsaidie

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,110
Reaction score
15,376
Baada ya mdau mmoja wa JamiiForums.com kudai kuwa mgonjwa wao amekaa zaidi ya wiki mbili katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) akisubiri kufanyiwa upasuaji, huku wakielezwa kuwa kuna vifaa vinasubiriwa, jambo linaloongeza gharama kwa familia, taasisi hiyo imetoa ufafanuzi.

Hoja ya Mdau ~ Mgonjwa wetu anateseka akisubiri upasuaji wiki ya pili sasa MOI, wanasema “Kuna changamoto ya vifaa”

Meneja Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi amesema ndugu wa mgonjwa huyo wafike ofisini ili kusaidiwa kufuatilia taratibu, akieleza kuwa mgonjwa aliyelazwa wodini tayari yupo kwenye ratiba ya matibabu na ni muhimu kwa taasisi.

Ameongeza kuwa sababu za kuchelewa kufanyika kwa upasuaji hutofautiana; baadhi hushirikishwa kwa ndugu na nyingine ni za kitaalam zaidi, ambapo madaktari huendelea kumuandaa mgonjwa ili awe tayari kufanyiwa upasuaji.

Amesema "Kwa sasa, huduma za upasuaji zinaendelea kama kawaida, ikiwa ni pamoja na orodha ya wagonjwa wanaopangiwa kufanyiwa upasuaji kila siku. Pia, Idara ya Dharura (Emergency) inaendelea kutoa huduma, ingawa kuna baadhi ya wagonjwa wenye mahitaji maalum ya vifaa, hali inayoweza kusababisha ucheleweshaji katika baadhi ya kesi."
 
Tangu lini taasisi ya serikali ikawa na huduma bora ? Hapo ni bora liende tu., mtumishi yeye mwisho wa mwezi akaunti inasoma !!!!
 
Back
Top Bottom