nataka kutumia njia za halali bila kutoa Rushwa(natumai sitaombwa).
nataka kutumia njia za halali bila kutoa Rushwa(natumai sitaombwa). nitalipa kodi zote na ushuru husika.
Mmmh! Itabidi uandae kidogo baba mambo yaharakishwe kwa nijuavyo mie.
Haiitwi RUSHWA, inaitwa TAKRIMA mkuu.
Ol th best.
Naomba gharama za kukomboa Gharama Kontena la futi 20, lenye vifaa vya ujenzi wa nyumba binafsi bandari ya DSM.
1.thamani ya vitu vyote humo ndani ni kama $8,000
2.Kulisafirisha hadi Dar itanigharimu $2000
USHURU ninaotakiwa kutozwa ni kiasi gani?nimesoma taarifa za TRA wanadai kodi ni 15% kwa vifaa vya ujenzi.(stand to be corrected)
je kuna gharama nyinginezo?kuclear kontena hilo kutagharimu kiasi gani?nataka kutumia njia za halali bila kutoa Rushwa(natumai sitaombwa).nitalipa kodi zote na ushuru husika.
kwa wajuzi naomba makadirio hayo.
Mimimpole, kuhusu kuwepo kwa vifaa feki bongo hili halina ubishi, unatakiwa uwe makini sana na vilevile uwe na uelewa mzuri kuhusu vifaa vya ujenzi.Nashukuru wadau kwa majibu yenu na ushauri.
kwa wale wanaoshauri kununua vifaa hivyo Dar,hili halipo kwenye meza kwa sasa.mimi ni mmoja kati ya watanzania wengi tuliochoka na vifaa feki hasa kwenye sekta ya Ujenzi.zile kauli za imetoka spain wakati ukweli unafahaamika hazimvutii kila mtu.
Vifaa vingi Bongo havipo,kama vipo vipo katika Premium price wakati Ughaibuni ni bei chee..,
mnalionaje hili la kununua LCD TV 42" kwa 2M wakati bei yake ni $500?!sasa kama usafiri unacost $100 kodi ni 40%.mbona bei bado haifiki huko?!
plus hiyo 2M LCD TV haichelewi kuwa feki vilevile na ni models za miaka mi-3 nyuma!
ushauri kwa wafanyabiashara wetu.MBADILIKE.WATANZANIA wanastuka kuhusu mbinu zenu
Mimimpole, kuhusu kuwepo kwa vifaa feki bongo hili halina ubishi, unatakiwa uwe makini sana na vilevile uwe na uelewa mzuri kuhusu vifaa vya ujenzi.
Mimi swali langu kubwa labda ungeeleza ni aina gani ya vifaa vya ujenzi unataka kupeleka bongo?? Sitegemei kama unataka kupeleka bongo mfano cement, mchanga au mbao. Kwa hiyo elezea ni vitu gani hasa unadhamiria kupeleka kwa container?
Mfano ulitoa wa LCD TV sina ubishi na vifaa vya electronics/electricals. Isipokuwa TVs siyo vifaa vya ujenzi.
Ndugu yangu nina uzoefu mkubwa sana na shughuli za ujenzi.
Kama labda ni nyaya za umeme hapo sawa ndo maana nakuomba uelezee vifaa unavyotaka kusafirisha.
Kumbuka vifaa vingi vya ujenzi inafaa viwe locally resoursed na vichache sana utahitaji ku-import.