gharama za Kukomboa kontena Dar es salaam PORT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

gharama za Kukomboa kontena Dar es salaam PORT

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by mimimpole, Jan 4, 2010.

 1. m

  mimimpole Member

  #1
  Jan 4, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 5
  Naomba gharama za kukomboa Gharama Kontena la futi 20, lenye vifaa vya ujenzi wa nyumba binafsi bandari ya DSM.

  1.thamani ya vitu vyote humo ndani ni kama $8,000
  2.Kulisafirisha hadi Dar itanigharimu $2000

  USHURU ninaotakiwa kutozwa ni kiasi gani?nimesoma taarifa za TRA wanadai kodi ni 15% kwa vifaa vya ujenzi.(stand to be corrected)

  je kuna gharama nyinginezo?kuclear kontena hilo kutagharimu kiasi gani?nataka kutumia njia za halali bila kutoa Rushwa(natumai sitaombwa).nitalipa kodi zote na ushuru husika.

  kwa wajuzi naomba makadirio hayo.
   
 2. m

  mzanganyika JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 257
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama umeambiwa duty ni 15% usisahau kuna na VAT ya 18%.

  Gharama za usafiri kutoka bandarini hadi utakapoytaka mzigo ufike na kuna gharama za clearing agent.

  Kama unataka freight agent akupe estimate za uhakika na fee yake ili uamue nijulishe.Mjomba wangu ni freight agent mwenye experience zaidi ya miaka 10.
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Jamani hakuna usumbufu kama wa container....kuna fees kibao angalia status ya container....port to port au to home...kila moja ina gharama yake!kukagua TRA wata uplift lazima....then dola 75 za SDV sijui hata za nini....wanasumbua sanaaaaa
   
 4. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,169
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145

  Mmmh! Itabidi uandae kidogo baba mambo yaharakishwe kwa nijuavyo mie.
  Haiitwi RUSHWA, inaitwa TAKRIMA mkuu.
  Ol th best.
   
 5. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Siyo rushwa au Takrima; hii huiwa inaitwa 'GREASING OF PROCEDURES'
   
 6. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2010
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Je ni aina ipi ya vifaa vya ujenzi unayotaka kusafirisha kwenda Dar kwa container?

  Kutokana na usumbufu mkubwa ambao ni more likely utajitokeza esp banadarini na TRA unaweza jikuta ni bora ununue hivyo vifaa Dar, ila uwe makini tu upata vitu vyenye ubora.

  Vinginevyo labda hivyo vifaa unavyosafirisha kwa container havipatikaniki Dar
   
 7. Madikizela

  Madikizela JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 4, 2009
  Messages: 320
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  ChomaChoma hapo umenena!!
   
 8. m

  mimimpole Member

  #8
  Jan 12, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 5
  Nashukuru wadau kwa majibu yenu na ushauri.

  kwa wale wanaoshauri kununua vifaa hivyo Dar,hili halipo kwenye meza kwa sasa.mimi ni mmoja kati ya watanzania wengi tuliochoka na vifaa feki hasa kwenye sekta ya Ujenzi.zile kauli za imetoka spain wakati ukweli unafahaamika hazimvutii kila mtu.

  Vifaa vingi Bongo havipo,kama vipo vipo katika Premium price wakati Ughaibuni ni bei chee..,

  mnalionaje hili la kununua LCD TV 42" kwa 2M wakati bei yake ni $500?!sasa kama usafiri unacost $100 kodi ni 40%.mbona bei bado haifiki huko?!

  plus hiyo 2M LCD TV haichelewi kuwa feki vilevile na ni models za miaka mi-3 nyuma!

  ushauri kwa wafanyabiashara wetu.MBADILIKE.WATANZANIA wanastuka kuhusu mbinu zenu
   
 9. Hebrew

  Hebrew JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2010
  Joined: Jul 3, 2008
  Messages: 509
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Mimi nakushauri ulitolee Tanga ..maana Dar utasumbuliwa sana. Mimi walinitesa sana 2008..yaani container lilichukua wiki sita kutoka...ila jamaa yangu alipeleka la kwake Tanga na likatoka mapema sana!!
  Na hawasemi rushwa tena ila utaombwa zawadi
   
 10. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2010
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mimimpole, kuhusu kuwepo kwa vifaa feki bongo hili halina ubishi, unatakiwa uwe makini sana na vilevile uwe na uelewa mzuri kuhusu vifaa vya ujenzi.

  Mimi swali langu kubwa labda ungeeleza ni aina gani ya vifaa vya ujenzi unataka kupeleka bongo?? Sitegemei kama unataka kupeleka bongo mfano cement, mchanga au mbao. Kwa hiyo elezea ni vitu gani hasa unadhamiria kupeleka kwa container?

  Mfano ulitoa wa LCD TV sina ubishi na vifaa vya electronics/electricals. Isipokuwa TVs siyo vifaa vya ujenzi.

  Ndugu yangu nina uzoefu mkubwa sana na shughuli za ujenzi.

  Kama labda ni nyaya za umeme hapo sawa ndo maana nakuomba uelezee vifaa unavyotaka kusafirisha.

  Kumbuka vifaa vingi vya ujenzi inafaa viwe locally resoursed na vichache sana utahitaji ku-import.
   
 11. m

  mimimpole Member

  #11
  Jan 13, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 5
  umepatia mkuu,

  vifaa ni kwa ajili ya Finishing,sidhani kama mchanga/kokoto za Bongo zina tatizo lolote.naongelea electric installations/plumbing accesories/floor tiles/sanitary equipments/window panels etc.

  last time i quoted mafundi wa bongo cost ya hivyo vyote ilikuwa inachezea $25,000.

  Bahati nzuri kuna internet siku hizi hata sie kina yakhe tunaweza kutazama kulikoni.kwa sasa am looking at spending $16,000-$18,000.not much of savings but everyone knows how difficult any hard earned money is to part with.

  thanks for your concerns and advices,tutafika tu!
   
Loading...