kuna watu huwa wanafikiri gari ni toyota tu, hata mimi zamani nilikuwa nafikiri simu lazima iwe nokia. anyway toyota wana spare mpaka za buku jero kwa sababu ni rahisi kuzifeki na vile vile used zipo kibao na pia za wizi zipo. lakini mazda pia spare zipo, ukikosa mkoani agiza dar arafu ni genuine, the fact ni kwamba gari zote za japan spares zipo sema tu labda bei.
back to the topic mimi nimeingiza demio ya 2003 ina kama mwezi now inafanya poa tu mafuta inanusa,ndani mufindi kama kawa, CIF ilikuwa $ 2400. kwa sababu ya uchakavu wa mwaka 1, nimelipa kodi jumla 3,300,000 so mpaka nimeikalia imechukua jumla 8,250,000/= kitu mang'anyu kipya km 31,000 tu. so usiogope, yani kuna window 8 arafu kusiwe na sight mirror ya mazda wabongo bana,kwanza mi sijawahi kuona juu ya mawe zaidi ya gx 100 na corola tehe tehe,