Gharama za hospital ni kubwa. Jitahidini muwe na bima

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
8,109
14,063
Mpaka sasa nimetumia 133,000/= kwa ajili ya vipimo. Na kuna kipimo ki1 nimeacha sababu ya kukosa pesa. Nina maumivu mgongoni. Kuanzia usawa wa mbavu kuja juu.

Nimekuja kumwona dr baada ya kumpa maelezo kaniandikia kufanya vipimo vya ultrasound, xray, na vipimo v3 vingine kutoka kwenye damu. Ambavyo ni kwa ajili ya kuangalia mafuta. Yaani chollestral. Nimeacha kufanya xray ambayo nitaifanya j3.

Dah gharama za matibabu ni kubwa. Ambao hamjaajiriwa kama mimi, bima ya afya ni muhimu. Tujitahidi kuwa nayo itakusaidia kwa kweli.
 
Unanikumbusha Kuna mwaka nimeumia mpirani nimepata maumivu makali kifuani. Nimefika zahati binafsi Daktari ananiambia nina UTI. Nikamwambie nipe NHIF yangu niondoke.

Ninachotaka kusema kama huna uelewa wa matibabu hospitali binafsi zinatumia njia chafu ili utoe hela nyingi pasipo na uhitaji wa msingi.
 
Dr kilaza au kajiskia uchangie pato la hospital... x ray na ultrasound at once kwaajili ya tatizo moja?

Then ataku refer kwa physiotherapist
Nilimwelewa maelezo yake. Alisema xray ni kwa ajili ya kuangali mapafu na ultrasound alitumia kwa ajili ya kucheck figo, ini, bandama,na kipofu cha mkojo.
Nipo hapa nasubiria kwenda kumwona tena aniambie vipimo vimesoma kitu gani.
 
Una umri gani mkuu samahani kwa kuuliza
 
Tunapoelekea ni kwamba utalazimishwa lakini ndio hivyo hicho kikaratasi chako huenda mengi utakayohitaji yatakuwa hayamo hivyo itabidi ujiongeze tu....

Hii nchi inapoelekea panatisha..., hakuna safety net na huduma zote zimegeuka kuwa biashara / miradi

Duuuh huko mahospitalini siku hizi kuna vilaza sana, miezi iliyopita dada angu alikuwa anatokwa na damu puani, eti akaambiwa shida ni typhoid aisee halafu no extra info kuhusu tatizo hilo zaidi ya kupewa Ctx.
 
Unanikumbusha Kuna mwaka nimeumia mpirani nimepata maumivu makali kifuani. Nimefika zahati binafsi Daktari ananiambia nina UTI. Nikamwambie nipe NHIF yangu niondoke.

Ninachotaka kusema kama huna uelewa wa matibabu hospitali binafsi zinatumia njia chafu ili utoe hela nyingi pasipo na uhitaji wa msingi.
Hata huko serikalini hali ni hiyohiyo tu mkuu, kutokwa damu puani ===Typhoid
 
Back
Top Bottom