Airtel imepandisha gharama za internet, 400mb kwa sasa sh. 5000. Piga *154*44#
Nadhani makampuni ya simu ya Tanzania ni ya wakubw. Maana yanavyowaibia na kuwadhalilisha watanzania nashindwa hata kuelewa nini mantiki ya kuwa na serikali. Katika Afrika ni Tanzania pekee yenye huduma aghali na za hovyo za simu na umeme. Lini tutakuwa huru jamani. Tumeacha wezi wachache watuchuuze na kutula tujikiona siyo?
Usidanganyike kaka tz tuna bei rahisi sana ya internet kama huamini nakupa details na source tuanzie kenya
kenya
Safaricom 50 mb wanauza ksh 100 sawa na 2000 ya bongo
500mb ni ksh 499 sawa na elf 10 huku, wakati voda unapata 750 mb na ukimaliza bundle unapata net free sema speed ndogo
Angalia hapa kwa maelezo ya bundle za safaricom
Safaricom -PrePay Data Bundles
Ukija airtel ndo usiseme ghali sana kwa siku ksh 150 per day unlimited sawa na elf 3 kwa mwezi ksh 2999 karibia elf 60 wakati tigo standar elf 35 tu na speed nzuri
Jivunie kua mtanzania
yeah man! Umesema vema mkuu! But kwanini wanapandisha gharama bila taarifa? Wakati wangeweza kuchapisha tangazo lao hapo juu kwenye red &white? Huku ni kutokujali wateja wao!
Sio kweli, mi juzi nimenunua mb 400 kwa sh 2500. Andika internet kwenda 15444.
Nyie mnaenda *154*44# kutafuta nini? Andika internet kwenda 15444 na utapata 400mb! Mi naitumia na leo ni siku ya pili tangu nijiunge. Acheni uzushi!