Gharama ya kuahirisha kuchukua hatua(Procrastination)

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,480
5,506
Je umewahi kuahirsha jambo lolote lile katika maisha au biashara? Umewahi kuahirisha jambo dogo au kubwa kwa umuhimu?

Kuahirisha ni tabia ya kuacha kufanya jambo fulani na badala yake unafanya jambo jingine.Ni tofauti na uvivu amapo mtu hafanyi jambo lolote.Katika ulimwengu wa biashara na ujasiriamali hali hii hujitokeza sana na ni moja kati ya sababu kubwa ya kushindwa ama kuazisha biashara au kuanguka kwa biashara za aina nyingi.Uhairishaji husababishwa na masuala mengi lakini kubwa huwa ni ama kukosa kipaumble au kushindwa kutokana na ugumu.Kwa kawaida ubongo wa mwanadamu hupenda kufanya yale mambo ambayo yanampa mtu furaha ya upesi na ambayo hayana ugumu katika kuyatekeleza(Low risk and quick rewards).Haya hupewa kipaumbele kwa kutegemea mtu anapenda na kufurahia nini.Ni muhimu kufahamu mambo haya ili uweze kujua namna ya kuyakabili.

Uhairishaji unapotokea huonekana ni jambo la kawaida lakini unapoanza kuleta madhara na kujikuta ama una mambo mengi kuliko uwezo wako au umepoteza fursa fulani kwa sababu ya kuahirisha jambo fulani asi hiyo inakuwa na Uhairishaji mbaya na wenye madhara.Utajuaje kuwa wewe nu muahirisha mbaya?Kuna namna nyingi za kupima kiwango chako cha uhairishaji.Baadhi ya mbinu hizo ni pamoja na:
  1. Kutoa ahadi nyingi ambazo huwezi kuzitekeleza.
  2. Kufanya mambo mengi katika dakika za mwisho.
  3. Kukosa hamasa pale jambo linapokuwa sio la haraka
  4. Kuwa na hamasa zaidi jambo linapokuwa la uharaka.
Zipo pia namna nyingine za kufahamu kama una tatizo hili mfano kutokuwa na ratiba ya utekelezaji wa shughuli zako au kutokufuata ratiba uliyojiwekea.Kufanya mambo na kuyaacha nusu na kurukia mengine bila kukamilisha hata moja.Kuacha jambo kwa sababu ya ugumu na mengine kama hayo.

Uhairishaji ni mbaya sana. Ukiahirisha kutuma barua ya maombi ya kazi unaweza kukosa nafasi ya kazi kwa sababu ya kusahau taarifa muhimu.Unaweza kukosa fursa za kibiashara na mafanikio.Unaweza kupoteza wateja na marafiki wa muhimu katika maisha yako.Unaweza kujikuta unapata magonjwa ya moyo na wasiwasi.Unaweza pia kupata hasara na gharama za ziada kwa sababu ya kukosa ubora.

Je unawezaji kupunguza kiwango cha uhairishaji?
Kwanza lazima tukubali kwamba kwa sababu ya maumbile huwezi kuwa mkamilifu kwa 100% katika eneo uhairishaji lakini unaweza kupunguza uhairishaji pamoja na madhara yake kwa kujietengenezea desturi nzuri na kujenga haiba yako katika njia sahihi.Yafuatayo ni baadhi ya mambo unayoweza kufanya ili kujisaidia.
  1. Kwanza Jifahamu na ufahamu yale mamba ambayo unayafurahia.Ukiyafahamu mambo haya unaweza kutumia kigezo hicho katika kujenga ratiba na utaratibu wako wa kazi ambao hautaathiri hii raha yako.
  2. Pili tengeneza ratiba yako ya siku,wiki,mwezi na mwaka na daima jifunze kuweka vipaumbele katika kila jambo kwa kuzingatia uwezo wako
  3. Tatu Jifunze kwani moja ktika ya changizo kubwa la uhairishaji na uwezo hafifu au ugumu wa jambo au kukosa uelewa.Kadiri unavokuwa na uelewa wa jamba fulini ndivyo unavyofurahi kulifanya na kuridhika nalo.
  4. Nne jitahidi uwe na Dayari(Diary au Notebook) hii iwe ni kwa ajili ya kutunza zile kumbukumbu ambazo ni za muhimu na kipaumbele.Usiandike kila kitu ali vile vya muhimu na kinapokamilika hakikisha unaandika (DONE au unatiki)
  5. Tano ni kujenga desturi ya kujipongeza kila unapokamilisha jambo,Kwa mfano kama ukimaliza jambo unaweza jipa 15min za kufanya unachofurahia au siku moja ya mapunziko au kalikizo fulani kwa ajili ya kujipongeza.Hii desturi inakuwezesha kufanya ubongo wako upate ridhiko na furaha.
Je unachukua hatua gani katika kuhakikisha kuwa unashinda tabia ya KUAHIRISHA mambo?Je ni mambo mangapi ambayo umeahirisha ambayo yamekuathiri au kuwaathiri wengine kwa namna ambayo unaijutia? Tujadili.
 
Mwaka jana nlkuwa siumwi meno wala nn ila nkasema itabid niende kwa dentist ajili ya usalama tu ili niimarishe meno, si nkaghairi mwaka mpya umeingia nmeanza kuumwa meno tabu tupu
 
Back
Top Bottom