Magnificient
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 1,177
- 733
Kwanza nawasalimu wadau wote wa jf! Juzi juzi hapa kuna mshkaji wangu wa muda mrefu kaniambia dhamira yake ya kuoa, nikafurahi na kuahidi kumpa sapoti kadiri nitakavyoweza. Jamaa kaenda kuchumbia ukweni ndipo kizaazaa kikaanzia hapo. Barua haikuwa na shida, elfu ishirini tu ilitosha. Kilichoendelea ni kwamba jamaa akaambiwa mpenzi wake kataka mahari ya laki nne tu, ila wanaukoo nao wanataka jasho la malezi ya yule binti! Watu na mahitaji yao kwenye mabano ndo kama ifuatavyo:
Baba (boda boda 1 tu) mama (jiko la gesi) mjomba (kiroba cha mbolea) babu (simu yenye redio) bibi (kanga, vitenge na ndoo ya mafuta ya alizeti) na kaka ndo kataka afunguliwe biashara ya tigo pesa! So akaambiwa ajiandae andae tarehe 14.2.2014 aende kupeleka hivyo vitu na wao wamfanyie mipango ili tar 26.2.2014 ndoa ifungwe. Kwa ufupi rafiki yangu hana uwezo kiviile, ila kama laki 3 angemudu na wadau tungeongeza hata 3 nyingine; ila hayo makorokoro ndo pasua kichwa. Sasa hapa rafiki afanyaje? Nakabidhi kwenu wadau.