Gesi ailimia 84 kubaki Mtwara

Gesi ailimia 84 kubaki Mtwara

Makupa

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
7,237
Reaction score
4,347
Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania limewatoa wasiwasi wananchi wa Mtwara kuhusu gesi itakayosafirishwa kwenda Dar-es-Salaam kwa kuwa gesi zaidi ya asilimia 84 itabaki mkoani humo. Mkurugenzi mtendaji wa TPDC Yona Killagane alisema haya jana wakati akijibu hoja ya Mbunge wa wa Kilwa Kaskazini ,Murtaza Makungu aliyetaka kujua shirika hili linachukuliaje hoja za wananchi wa Mtwara kuhuhu kutandazwa kwa bomba hilo la gesi kwenda Dar-es-Salaam.Kutokana na ufaafnuzi huo wa TPDC,hoja za gesi ya Mtwara zilizokuwa zikiendeshwa kisiasa zilipotea na Kamati ikajielekeza kwenye mamboa mengine ya msingi kuhusu shirika. Ni wakati muafaka sasa wananchi waliokuwa wanachochewa na wanasiasa wa ovyo kuelewa ukweli huu kuliko kutegemea upotoshaji unaofanywa na hawa wanasiasa wahuni
 
Hiyo gesi itabaki vipi huko wakati walishasema Mtwara ina gesi kidogo!
mitambo yote ya kuzalisha gesi inayopatikana kwenye kina kirefu cha maji ambapo ni umbaali wa kilomita 80 kutoka nchi kavu itajengwa maeneo ya mtwara na lindi mkuu
 
Hiyo gesi itabaki vipi huko wakati walishasema Mtwara ina gesi kidogo!
kwani kitu kikiwa kidogo hakifai kugawanya kwa %. maana yake gesi nyengine itatumika mtwara na kuzalisha umeme mtwara na asilimia kidogo itaenda nje ya mtwara.au na hii unataka upinge?
 
mitambo yote ya kuzalisha gesi inayopatikana kwenye kina kirefu cha maji ambapo ni umbaali wa kilomita 80 kutoka nchi kavu itajengwa maeneo ya mtwara na lindi mkuu
Yetu macho! Tumesha ahidiwa mengi zikiwemo meli kwenye maziwa yetu makuu (tanganyika, nyasa na victoria), lakini hadi sasa hamna dalili!
 
Naibu waziri alisema atawaagiza wawekezaji wakang'oe mitambo iliyoishafungwa huko mtwara na kuwaacha wana mtwara kama walivyokua zamani.mbona hawa viongozi wana kinzana?kunanini hapo kwenye ges?kwani kunauharaka gani kwani ikibaki alidhini itaoza? Watatuuli mtwara hatoki mtu na gesi mjemtufanye kama nyamongo na mwadui hatutaki bana
 
dah, kumbe mtwara kuna watumiaji wakubwa gesi kuliko marekani
 
Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania limewatoa wasiwasi wananchi wa Mtwara kuhusu gesi itakayosafirishwa kwenda Dar-es-Salaam kwa kuwa gesi zaidi ya asilimia 84 itabaki mkoani humo. Mkurugenzi mtendaji wa TPDC Yona Killagane alisema haya jana wakati akijibu hoja ya Mbunge wa wa Kilwa Kaskazini ,Murtaza Makungu aliyetaka kujua shirika hili linachukuliaje hoja za wananchi wa Mtwara kuhuhu kutandazwa kwa bomba hilo la gesi kwenda Dar-es-Salaam.Kutokana na ufaafnuzi huo wa TPDC,hoja za gesi ya Mtwara zilizokuwa zikiendeshwa kisiasa zilipotea na Kamati ikajielekeza kwenye mamboa mengine ya msingi kuhusu shirika. Ni wakati muafaka sasa wananchi waliokuwa wanachochewa na wanasiasa wa ovyo kuelewa ukweli huu kuliko kutegemea upotoshaji unaofanywa na hawa wanasiasa wahuni
Mmmh........ Hili ni changa la macho orijino!! Itakuwa wanataka tu kuwapoza machungu watu wa kusini, anyway huu ni upepo tu, mbona utapita kama "mapepo" mengine yaliyotangulia kwenye nchi hii!!!
 
Huyu naye ni kubwa J.I.N.G.A Ameyajuaje haya kuwa 80% ya gesi itabaki Mtwara?, Kwanza hiyo sera ya gesi asilia bado hajaandikwa? Pili jana mwenyewe alikiri kwamba ofisi yake haina mikataba ya gesi including ujenzi wa bomba la kwenda Dar.

Sasa hii ya 80% kubaki Mtwara ameipataje? au na yeye ameoteshwa kama yule mzee wa ndoto! Hili ni changa la macho! Yeye hawezi kuwa informed kuliko Prof Muhongo Waziri wa Nishati.
 
WANAJIDANGANYA TU,kama ilo walijua mbona hawakusema tokea mara ya kwanza wameanza kuleta maneno ya shombo,akiwamo waziri na rais wake,wao si wamesema gesi hipo msimbati sio mtwara,watakula jeuri yao
 
Asilimia 84% ni kiasi gani cha gesi (ujazo gani utakaotumika mtwara?? Asilimia 84% zinabaki mtwara zikitumika majumbani au zikitumika viwandani au????
Acheni ujinga wa kucheza na statistics. Actually huyuKilaghane hajasema chochote hapo zaidi ya kuwapiga watu na sindano ya ganzi!
 
Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania limewatoa wasiwasi wananchi wa Mtwara kuhusu gesi itakayosafirishwa kwenda Dar-es-Salaam kwa kuwa gesi zaidi ya asilimia 84 itabaki mkoani humo. Mkurugenzi mtendaji wa TPDC Yona Killagane alisema haya jana wakati akijibu hoja ya Mbunge wa wa Kilwa Kaskazini ,Murtaza Makungu aliyetaka kujua shirika hili linachukuliaje hoja za wananchi wa Mtwara kuhuhu kutandazwa kwa bomba hilo la gesi kwenda Dar-es-Salaam.Kutokana na ufaafnuzi huo wa TPDC,hoja za gesi ya Mtwara zilizokuwa zikiendeshwa kisiasa zilipotea na Kamati ikajielekeza kwenye mamboa mengine ya msingi kuhusu shirika. Ni wakati muafaka sasa wananchi waliokuwa wanachochewa na wanasiasa wa ovyo kuelewa ukweli huu kuliko kutegemea upotoshaji unaofanywa na hawa wanasiasa wahuni

Upuuzi mwingine huu wanaolalamika ni wananchi wa mtwara kwa ujumla wao wakiwa mtwara, yeye anatoa majibu kama hayo kwa mtu mmoja akiwa Dar. wanaogopa nini kwa ujumla wao kama ni wakweli kuacha ofisi na kwenda mtwara kuwaambia na kuwaahidi wanamtwara kuwa 84% ya gas itabaki kwao? Hapo ndipo wanapozidi kuwasha moto kwa kutowashirikisha waanzisha maada!
 
Mbona haya hayakusemwa mapema na waziri. Kinyume chake ilikuwa ni kebehi, kemea na kashifu. Tatizo ni kuwaamanisha watu kwamba hiyo asilimia 84 itawafaidisha watu wa Mtwara.
 
ha tu da nga nyi kiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!
 
Yani bila chenga, hii mijitu mijinga sana inatufanya sisi watoto sana
Ndugu yangu watanzania niwaelewa sana na si watu wa vurugu lakini ukilianzisha ,kulizima shughuli.Viongozi wetu inaonekana hawana umoja au command post yao inapwaya.Hii ina maana hawana mwongozo wa kuonyesha nani aongee nini na wapi ndo maana watu wa Mtwara na Tz kwa ujumla wanashindwa kupambanua lipi na lipi na kuwapa matatizo viongozi wetu wa ngazi za juu Rais na WM.Mradi wa gesi sio wa mwaka jana au juzi.Vikao mbalimbali kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa vimeisha fanyika na kulidhiana kwa manufaa ya mradi huu.Makundi ya viongozi hata wabunge,madiwani,hata Zito na kamati yake walitembelea nchi mbali mbali Ulaya kuona ni jinsi gani na muundo mzima wa utawala wa gesi ili waje wawaelimishe wananchi.Wamekula posho nyingi za dola na sasa wanageuka serikali.Hawa viongozi ni ndumila kuwili ,wasitufanye ndondocha.Kama uko kambi ya upinzani na ulikubali kula posho kili hadharani ili upanguse midomo yako.Tatizo kuna wafitini wengi na kumbe jua linawaka linawaumbua.Watanzania hawataki marumbano yasiyo na tija .Mbunge unasimama unapinga mradi wa gesi kumbe kamati zote teule ulikuwepo na Norway/Sweden /ukrane/China ulienda na kupata takrima ACHA HIZO.Huu mtandao wa jamii sio pinzani wa serikali ila unataka kutoa fursa ili wananchi wapate elimu kwa kutoa facts.Hapa sio mahali pa kujipatia umaarufu.Sisi hata chama chetu kikifanya sio sawa tutasema maana kuna watu wanapandikizwa.We Kalaghe usizubutu kusema mkataba huu hujui basi ondoka ofisini au unataka mshauri ?Hivi nyi viongozi wa kusini hamjui kuwa mradi huu ni Trilion za dola za kimarekani 1.86 kutoka Uchina Exim bank.Mbona mlifanyiwa tafrija mnatutia dongo jikoni.Nyie viongozi wa kusini si mlienda Norway mkakutana na Kampuni inaitwa Statoil na Exxon wanaochimba gesi Kitalu namba mbili-Mkoa wa lindi(Lavan na Zafarani-Pwani ya Kilwa mkapewa takrima bisha. Je nyie viongozi wa kusini si mridhia kutoa eneo kwa Aghakhan Foundation kujenga hospitali kubwa kama Apollo ya India iwe sambamba na ujenzi wa bomba?.Mwisho hayo ni madokezo yanayoashiria kuwa viongozi ni wanafiki waanzisha vurugu ili kumkomoa mtoto wa kabwela BYE
 
Back
Top Bottom