Gerson Msigwa: Poleni mliopata sintofahamu kutokana na baadhi ya mitandao kuandika nimefiwa na Mama Mzazi

Gerson Msigwa: Poleni mliopata sintofahamu kutokana na baadhi ya mitandao kuandika nimefiwa na Mama Mzazi

Inside10

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
33,614
Reaction score
40,160
Habari iliyonifikia hivi punde, Kupitia ukurasa wa Gerson Msigwa, Instagram

Marehemu Hannah Mayige (waliokaa, wa kwanza kulia), Mimi na watumishi wenzangu wa TBC Kituo cha Songea tulimuita Mama kutokana na jinsi alivyotuongoza akiwa Mkuu wa Kanda ya Nyasa wa TBC.

Tulimwita Mama kwa sababu pamoja na kutusimamia kazini, alishughulikia kwa karibu masuala ya kifamilia ya sisi watumishi. Waliougua aliwapelekea chakula na alilala hospitali akiuguza, waliofiwa alihusika mwanzo hadi mwisho, waliovurugana kwenye ndoa alisimama kidete na ndoa zote zilikuwa salama zikiwemo alizozikuta zikipumulia mashine, alisisitiza watumishi kupeleka watoto shule na kuwasimamia, mtumishi alipostaafu au kuhama aliandaa hafla ya kumuaga, alijenga upendo na umoja wa kiwango cha juu, aliwatia moyo watumishi wapya nikiwemo mimi, na alipenda kila mtumishi amche Mungu.

Hakika alikuwa Mama, Mama hasa. Sitasahau siku tano alizokaa kijiji kwetu wakati wa msiba wa Dada yangu, akilala chini, akipika, akifagia uwanja, akifua nguo na alikuwa mfariji mkubwa wa Mama yangu Mzazi.

Naomba radhi kwa wale walioona post yangu ya kwanza nilipomuita “Mama Yangu” na wakadhani ni Mama yangu Mzazi. Mama yangu mzazi yupo hai, japo Hannah nae ni Mama yangu.

Poleni mliopata sintofahamu kutokana na baadhi ya mitandao kuandika nimefiwa na Mama Mzazi.

LALA SALAMA MAMA HANNAH MAYIGE.
1764504499585.png
 
Back
Top Bottom