BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 328
- 414
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, ameipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa jitahada zake za kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba kwani vitaipunguzia serikali gharama ya kuagiza dawa nje ya nchi.
Msigwa ametoa pongezi hizo hii leo, wakati akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Meja Jenerali Gabriel Saul Mhidze (Dkt) alipotembelea Makao Makuu ya MSD yaliyoko Keko jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Meja Jenerali Gabriel Mhidze amesema kwa sasa MSD inazalisha aina 10 za dawa, pamoja na barakoa ambapo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa fedha, viwanda 7 vya MSD vitakamilika na vitazalisha dawa za ngozi, mipira ya mikono, dawa za maji za watoto na mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi.