Gerson Msigwa aipongeza MSD kwa kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba

Jan 12, 2019
89
150
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, ameipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa jitahada zake za kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba kwani vitaipunguzia serikali gharama ya kuagiza dawa nje ya nchi.

Msigwa ametoa pongezi hizo hii leo, wakati akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Meja Jenerali Gabriel Saul Mhidze (Dkt) alipotembelea Makao Makuu ya MSD yaliyoko Keko jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Meja Jenerali Gabriel Mhidze amesema kwa sasa MSD inazalisha aina 10 za dawa, pamoja na barakoa ambapo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa fedha, viwanda 7 vya MSD vitakamilika na vitazalisha dawa za ngozi, mipira ya mikono, dawa za maji za watoto na mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

IMG-20210907-WA0004.jpg

IMG-20210907-WA0005.jpg

IMG-20210907-WA0006.jpg

IMG-20210907-WA0001.jpg

IMG-20210907-WA0002.jpg

IMG-20210907-WA0003.jpg
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
9,533
2,000
Hakuna meeting room hapo Msd...hiko mbona kama kikao tu cha masela wanajadili issue za Simba na Yanga au Hamisa na Sepenga...
 
We Know Next

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
752
500
Major General Mhidze, ni mmoja wa Watanzania wachache na waadilifu waliofika rank hiyo ktk Jeshi la Tanzania. Kusema ule ukweli, amewadhibiti wale wapiga deals pale MSD na network zake. Huu ulikuwa moja ya uteuzi bora kabisa uliofanywa na Hayati Magufuli.

Hongera Major General Mhidze, wajanja wakikuletea ujinga wao, warushe kichurachura!
 
Kugosola

Senior Member
Aug 7, 2021
125
250
Nafikiri Msigwa hajachukua muda wa kuisoma hiyo taasisi kwamba ina uoza mkubwa sana chini ya huyo afande, kuna madudu mengi sana hapo mahali.

Ndugu Msigwa msitake kutumia ukanda ili kumsafisha huyo afande aliejaa madudu ya kila aina, Corporate Management kwa huyo afande ni zeero kabisa.

Ndugu Msigwa hebu zipitie threads ziliweza kuchambua madudu ya hapo mahali na members wa JF otherwise ungeweza kuzipitia hizo thread zilizopita ungejifikilia mara mbili mbili kutembelea hapo mahali, huyo afande hana lolote analolijua kuhusu supply chain achana na mambo ya uongozi.

Kama vipi, nitawaomba wana JF warushe tena threads zihusuzo uozo wa hapo MSD ikiwa ni pamoja na udhaifu wa huyo afande katika kuiendesha hiyo taasisi

Narudia tena, Ndugu Msigwa acha mambo ya kuanza kusafishana ki-ndugu na ki-kanda maana nasikia mdogo wako kapewa hapa juzi tu ukurugenzi wa Manunuzi wakati hana sifa kisa ni mtu wa kwao afande na mdogo wa Garson Msigwa, Msigwa acha hizo hiyo taasisi huifahamu!!
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,497
2,000
Maendeleo kwa VITENDO...

Kazi Inaendelea KIVITENDO....

#TanzaniaTuitakayo
#SiempreJMT
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
10,497
2,000
Major General Mhidze, ni mmoja wa Watanzania wachache na waadilifu waliofika rank hiyo ktk Jeshi la Tanzania. Kusema ule ukweli, amewadhibiti wale wapiga deals pale MSD na network zake. Huu ulikuwa moja ya uteuzi bora kabisa uliofanywa na Hayati Magufuli.

Hongera Major General Mhidze, wajanja wakikuletea ujinga wao, warushe kichurachura!
Ajabu ni kuwa wako members WANAMPINGA humu JF 😲😲

Sijui baadhi yetu watanzania tunataka MALAIKA akaiongoze MSD?!!!

Inashangaza kwa kweli.....
Inashangaza mno......

#SiempreJMT
#KaziIendelee
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,059
2,000
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, ameipongeza Bohari ya Dawa (MSD) kwa jitahada zake za kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba kwani vitaipunguzia serikali gharama ya kuagiza dawa nje ya nchi.

Msigwa ametoa pongezi hizo hii leo, wakati akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Meja Jenerali Gabriel Saul Mhidze (Dkt) alipotembelea Makao Makuu ya MSD yaliyoko Keko jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Meja Jenerali Gabriel Mhidze amesema kwa sasa MSD inazalisha aina 10 za dawa, pamoja na barakoa ambapo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa fedha, viwanda 7 vya MSD vitakamilika na vitazalisha dawa za ngozi, mipira ya mikono, dawa za maji za watoto na mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

View attachment 1927191

View attachment 1927192

View attachment 1927193

View attachment 1927194

View attachment 1927195

View attachment 1927196
Huwa sina imani na Serikali kufanya biashara soon kodi zitaanza kuendesha hasara ,hivyo viwanda wawe wanashirikiana na sekta binafsi vinginevyo ni hatarishi.
 
Kugosola

Senior Member
Aug 7, 2021
125
250
Ajabu ni kuwa wako members WANAMPINGA humu JF 😲😲

Sijui baadhi yetu watanzania tunataka MALAIKA akaiongoze MSD?!!!

Inashangaza kwa kweli.....
Inashangaza mno......

#SiempreJMT
#KaziIendelee
Gerson Msigwa angemuuliza afande maswali yafuatayo;

1. Ni Bodi ipi ilipitisha huo mradi!

2. Report ya cost benefit analysis ya huo mradi iko wapi!

3. Huo mradi umeanzishwa kwa sheria ipi ya Bunge?, kwasababu MSD ilianzishwa kwa sheria namba 13 ya Bunge ya mwaka 1993 kwa kufanya; manunuzi, kuhifadhi na kusambaza dawa za binadamu, kazi ya uzalishaji haipo. Hatutaki kuwa na kiongozi ambae anajifanyia tu mambo kwa utashi wake utafikili yuko nyumbani kwake

4. Nani alipitisha kujenga kiwanda kwao Iringa, je kuna kuna report yoyote ya upembuzi yakinifu?

5. Je nani alipitisha kuanza uzalishaji wa hizo gloves badala ya dawa, maana MSD ina catalogue items ya dawa 385 ambazo zinahitajika hospitalini at any time T

6. Mkandarasi wa ujenzi alipatikanaje? Kulikuwa na ushindani? Maana inasemekana ilikuwa through single source ikiwa ni pamoja na materials za dawa

7.

8.

Hayo ndo maswali aliyotakiwa kuuliza Msigwa!
 
Kugosola

Senior Member
Aug 7, 2021
125
250
Huwa sina imani na Serikali kufanya biashara soon kodi zitaanza kuendesha hasara ,hivyo viwanda wawe wanashirikiana na sekta binafsi vinginevyo ni hatarishi.
ooh yes, kabla ya kuja huyu afande wa Gerson Msigwa hapa MSD Serikali ilikuwa na mpango mzuri sana wa kuanzisha viwanda under PPP - Public Private Partneship na ulifikia hatua nzuri sana, na ulikuwa ni mpango jumuishi ukihusisha all stakeholders. Na hili jambo liliangaliwa in a broad perspective na Serikali kuwa mradi endelevu and not in a piecemeal!

Lakini alipokuja huyu afande akaamua kuupiga chini mradi wa PPP na kuanza na initiative za kwake ambazo haziwezi kuliletea tija Taifa.
 
Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,976
2,000
Hivi Msigwa ana cheo gani vile?
Kama umeniwahi maana huyu jamaa sio waziri yeye msemaji wa serikali ila msemaji anapewa tu maamuzi ya serikali na kuyafikisha ila anafanya kazi kama waziri fulani asiyekuwa na wizara maalumu. Kazi yake ni nini na kama nani anafanya ziara hizi? au ana majukumu mengine hatuyajui mimi nadhani Mama anapoteza mwelekeo kila leo anatafuna kuliko uwezo wake ni wakati wa kuvunja serikali yote na kuunda upya from zero ila kwa sasa wengi wamepwaya vibaya sana kuanzia yeye mwenyewe.
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,059
2,000
ooh yes, kabla ya kuja huyu afande wa Gerson Msigwa hapa MSD Serikali ilikuwa na mpango mzuri sana wa kuanzisha viwanda under PPP - Public Private Partneship na ulifikia hatua nzuri sana, na ulikuwa ni mpango jumuishi ukihusisha all stakeholders. Na hili jambo liliangaliwa in a broad perspective na Serikali kuwa mradi endelevu and not in a piecemeal!

Lakini alipokuja huyu afande akaamua kuupiga chini mradi wa PPP na kuanza na initiative za kwake ambazo haziwezi kuliletea tija Taifa.
Huwa mnatoka wapi haya majitu yasiyojifunza hata kwenye historia? Tanga lini serikali ikafanya biashara?

Ili biashara ifanikiwe inakuwa driven na personal motives sasa Serikalini kuna personal motives?

Huu upumbavu wa majitu yenye mentality za kijaa unanikera Sana ,sio mda tutaanza kuchukua kodi za kufidia hasara. Viwanda sio majengo ni biashara zenye risks kubwa zinahitaji sekta binafsi zaidi.
 
Kertel

JF-Expert Member
May 11, 2012
4,712
2,000
nilidhani wataanza uzalishaji wa tracer medicine kadri ya essential drug list ya nchi,hakuna kitu hapo.
 
Chupayamaji

JF-Expert Member
Sep 19, 2017
3,797
2,000
Kuna dawa huwa zinaletwa na MSD nchini ila hospital na hata kwenye ghala za Msd huzipati.Ila ukienda kariakoo kwenye maduka unazikuta na zina nembo kabisa ya msd.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom