Masulupwete
JF-Expert Member
- Feb 15, 2012
- 2,366
- 2,397
Wamarudishe Dayanasori wetu.
Ni sahihi mkuu. ila kuna maeneo mawili tofauti. huyo wa ujerumani ni yule alipatikana lindi na tayari alishahojiwa bungeni lakn kuna hao wengi zaidi waliopatikana ziwa nyasa haieleweki walipelekwa wapi
Lini Ujerumani Watarejesha Mabaki ya Mjusi Mkubwa (Dinosaur) Wetu.
1.Wadau suala hili lilizungumzwa sana miaka michache iliyopita na kulikuwa na dalili nzuri. Lakini ni muda mrefu sasa sijaskia lolote huku hawa jamaa wakiendelea kupiga hela kwa mjusi wetu huyu.
2.Nimefatilia historia ya mijusi hawa na kuona kumbe kuna mabaki mengine mengi zaidi ya wadudu hawa walioishi zaidi ya miaka milioni 240 iliyopita yalipatikana maeneo ya ziwa nyasa (nyasasaurus) lakini haijaelezwa mabaki yao yalipelekwa wapi na km nchi tunafaidika vipi.
Naona km taifa tunapoteza pesa na historia ya nchi kirahisi hivi.Mwenye ufahamu wa haya mambo msaada pls.
Kinachofanya mtake mjusi arudishwe ni kukosa kwenu taarifa sahihi tu.
Ili kumtunza mjusi kuna taaluma na gharama zinazohusiana.
Mnayo bajeti ya kumtunza mjusi?
Mnayo technical know how ya kumtunza mjusi.
Mjusi yuko Berlin pale. Wajerumani wameandika kuwa mjusi katoka Tanganyika. Hakuna wizi hapo.
Kinachotakiwa ni ushirikiano na wajerumani katika kumtumia mjusi kuitangaza Tanzania sio mpaka mjusi awe physically nchini.
By the way, pale Berlin mjusi anaonwa na watu wengi kuliko iwapo angekuwa Bongo. Kwahiyo mjusi anaitangaza vizuri zaidi Tanzania akiwa Berlin.
Vilevile tafiti zinaonyesha mijusi wengine wapo Lindi chini ya ardhi. Ebu tufikirie kuwachimba hao walio ardhini kabla hatujamlilia aliyetafutwa na wajerumani na kuchimbwa na vibarua watanganyika (hawa vibarua picha zao zipo pale Berlin).
weka picha ya Mjusi wetu wasituletee ujinga bana!
....ujangili umezidi Tanzania si ajabu akiletwa majangili yatampora !!!!