Mabaki ya Mjusi mkubwa kuliko wote au dinasauria yako huko Mjini Berlin, Ujerumani yaligunduliwa wakati wa Ukoloni wa Wajerumani huko Kusini mwa nchi yetu,
kwenye nchi iliyokuwa inaitwa Ujerumani ya Afrika Mashariki Wajerumani wakayakusanya, kuyatunza na kuyasafirisha mpaka kwao kwenye kuyaweka kwenye hifadhi!
Leo hii Watanzania tunasema kwamba
Mzungu kaiba mjusi wetu na hatunufaishi kiuchumi, hivi hii ni
fair kweli kusema Mzungu kaiba mabaki ya Dinasauria?? Ni kwa nini tunasema huyu mjusi ni mali yetu? Ni kwa sababu tu amegunduliwa kwenye ardhi ambayo leo hii tunaiita TZ?
Na je kama wataalamu wa mambo ya kale (
Archeologist) wa Ujerumani wasingefanya utafiti na kugundua mabaki ya huyo Mjusi kwa maana nyingine kama
wasingekuja TZ leo hii tungekuwa tunaongelea habari za huyo Mjusi?
Sasa ni
kwa nini tunataka kudai kitu ambacho hatujakitolea jasho? Ni kama vile tu mabaki ya mtu wa kale huko Olduvai Gorge ambayo yako kwenye jumba la Makumbusho London Uingereza, yaligunduliwa na Mzungu, Je sisi tuna haki ya kuyadai leo hii na kusema kwamba ni yetu?
Tunatumia kigezo gani? Kwanza wakati yanagunduliwa
kulikuwa hakuna nchi iitwayo Tanzania, hivyo kwa upande wa Mjusi ina maana aligunduliwa nchi iliyoitwa Ujerumani ya Afrika Mashariki na siyo Tanzania vile vile kwenye Olduvai Gorge!
Kwa nini na sisi kwenye Tanzania yetu leo hii tusifanye tafiti zetu na kugundua wenyewe mabaki ya kale na ya kuyatunza
badala ya kudai kazi ambayo Mzungu alifanya tena kwa gharama yake mwenyewe? Au tunataka kusema mambo ya kale yanayaostahili kugunduliwa yamekwisha yote hapa nchini?
Mabaki ya Mjusi mkubwa kwenye Jumba la makumbusho, Berlini!
Mabaki ya binadamu wa kale ktk Olduvai, jijini London Uingereza!
Maba