German President Arrives in Tanzania For Five-day State Visit

German President Arrives in Tanzania For Five-day State Visit

Huyo ndo mkuu wa nchi wa Ujerumanı(head of state).Ni maarufu sema tu wewe ndo hauna uelewa kutosha kuhusu mifumo ya utawala wa mataifa duniani.

Chancellor was Ujermani huchaguliwa na wanna chi .Rais huchaguliwa name bunge.
 
Inaonekana mleta mada hata media hafuatlii, ikulu toka jana waltoa tarfa ktk media pia leo magazet yameandka ratba ya mgen huyo atakapokuwa tz,ww unasema wamefcha taarfa na kujfanya wa kwanza kuujuza umma.

=======

RAIS WA UJERUMANI, MHE. JOACHIM GAUCK KUWASILI NCHINI KESHO

Rais wa Ujerumani, Mhe. Joachim Gauck anatarajiwa kuwasili nchini usiku wa tarehe 02 Februari, 2015 kwa ziara ya kitaifa ya siku tano kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mhe. Rais Gauck atapokelewa rasmi na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Februari, 2015 na atakagua Gwaride la Heshima na kupigiwa mizinga 21. Wananchi wanaombwa kuwa watulivu wakati mizinga hii ikipigwa kwani ni salama.

Baada ya mapokezi hayo, Mhe. Gauck atafanya mazungumzo ya faragha na Rais Kikwete yakifuatiwa na mazungumzo rasmi. Aidha Marais hao watakutana na Waandishi wa Habari.

Baadaye siku hiyo ya Februari 03, Mhe. Rais Gauck atakutana na Wafanyabiashara, atatembelea Kanisa la Kilutheri la Azania Front, atakutana na Wawakilishi wa Taasisi za Kiraia na kushiriki Dhifa ya Kitaifa itakayoandaliwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete, Ikulu.

Mhe. Rais Gauck ambaye ameongozana na Mke wake Bibi Schadt, Viongozi Waandamizi kutoka Serikali ya Ujerumani na Ujumbe wa Wafanyabiashara tisa, ataondoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar tarehe 04 Februari, 2015 ambapo atafanya mazungumzo rasmi na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kabla ya kushiriki kwenye Mkutano wa Kamati ya Pamoja ya Viongozi wa Dini kuhusu Amani. Rais Gauck pia atakutana na Vijana kutoka Ujerumani wanaojitolea katika Programu ya Weltwarts Visiwani humo.

Jioni ya Februari 04, Mhe. Gauck ataondoka Zanzibar kuelekea Mkoani Arusha. Akiwa Mkoani humo siku ya tarehe 05 Februari, 2015 atatembelea Taasisi mbalimbali za kimataifa ikiwemo Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na kuhutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA). Mhe. Gauck na ujumbe wake watatembelea pia Hifadhi ya Wanyama ya Serengeti ambapo atazindua Kituo kipya cha kudhibiti Ujangili.

Mhe. Rais Gauck anatarajiwa kumaliza ziara yake hapa nchini tarehe 06 Februari, 2015 na kuondokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kurejea Ujerumani.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
01 Februari, 2015

Msamehe bure, asubuhi ni viroba badala ya chai.
 
Kwa mujibu wa Radio deutsche welle ya Ujerumani, Rais huyu ataenda Zanzibar kwa Boat
 
vipi barabara zilidekiwa? wamachinga na ombaomba hawajafichwa?
 
IKULU wamegoma kutoa taarifa za ugeni huuu on hourly basis mpaka sisi wana JF tumeaumbua

QUOTE]

Hata mimi nisie mtu wa media nimesoma taarifa za ujio wa Rais wa Ujerumani. Wewe umelala doro au unataka kupotosha kwa makusudi tu.
 
Ni wazi wale waliokuwa wanafuatilia mapokezi ya ujio wa Rais wa Ujerumani nchini kupitia TBC1 mtangazaji amerudia kauli hiyo mara kadhaa, namna Waziri Muhongo alivyochangia ujio wa Rais huyu hususan katika uwekezaji wa sekta ya mafuta na gesi. Kubali Kataaa Prof Muhongo hana mpinzani katika utendaji!

Hii inakwenda sambamba na Makala kutoka TAZAMA TANZANIA . Angalia namna mwandishi alivyomwelezea.
Kwaheri Profesa Muhongo, lakini umetuachia misingi ya uzalendo kiutendaji (Source Tazama Tanzania).

Profesa Muhongo amejiuzulu, mwangwi wa weledi hautaisha (Source Tazama Tanzania).
 
Ni wazi wale waliokuwa wanafuatilia mapokezi ya ujio wa Rais wa Ujerumani nchini kupitia TBC1 mtangazaji amerudia kauli hiyo mara kadhaa, namna Waziri Muhongo alivyochangia ujio wa Rais huyu hususan katika uwekezaji wa sekta ya mafuta na gesi. Kubali Kataaa Prof Muhongo hana mpinzani katika utendaji!

Hii inakwenda sambamba na Makala kutoka TAZAMA TANZANIA . Angalia namna mwandishi alivyomwelezea.
Kwaheri Profesa Muhongo, lakini umetuachia misingi ya uzalendo kiutendaji (Source Tazama Tanzania).

Profesa Muhongo amejiuzulu, mwangwi wa weledi hautaisha (Source Tazama Tanzania).

Kikwete atafanya la maana sana kama atamteua prof.Muhongo kuwa mkurugenzi wa shirika la reli TRL, naamini ataweza kulifumua na kulisuka upya liweze kujiendesha kwa tija.
 
Kweli amewakamata pabaya Muhongo...yaani mnajigongagonga kwake ili asiwatibulie, siyo?
 
Rais akienda nje tunalalamika wageni wakija tunalalamika pia Jena lipi sasa?

Jema ni kuandamana tu na kuwalalamikia polisi, hilo ndilo wanaloliona kwao ndio jema.
 
Kwa nini JK akienda Germany hapokelewi hivyo?

Mengine usipende kuuliza maana yanatia fedheha na masononeko ya moyo.
ImageUploadedByJamiiForums1422951748.345393.jpg
 
Kwa nini fursa isifunguliwe sambamba na makubaliano
Kwa vijana wa Tanzania kuoa/olewa na Wajerumani?
Kama ilivyokuwa mwanzo.
Taifa litakuwa na mtazamo mpya kifikra.
 
I wish tungeendelea kutawaliwa na Wajerumani! UK hawakufanya lolote la maana katika ardhi yetu...
 
Back
Top Bottom