German President Arrives in Tanzania For Five-day State Visit

LEMONT BISHOP

Member
Joined
Oct 29, 2014
Posts
85
Reaction score
89
IKULU wamegoma kutoa taarifa za ugeni huuu on hourly basis mpaka sisi wana JF tumeaumbua

994489_944609195558126_2726240642989893341_n.jpg

10959879_944609218891457_1887313153725720444_n.jpg

10945737_944609248891454_6892090133386456183_n.jpg

RAIS WA UJERUMANI, MHE. JOACHIM GAUCK KUWASILI NCHINI KESHO

Rais wa Ujerumani, Mhe. Joachim Gauck anatarajiwa kuwasili nchini usiku wa tarehe 02 Februari, 2015 kwa ziara ya kitaifa ya siku tano kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mhe. Rais Gauck atapokelewa rasmi na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Februari, 2015 na atakagua Gwaride la Heshima na kupigiwa mizinga 21. Wananchi wanaombwa kuwa watulivu wakati mizinga hii ikipigwa kwani ni salama.

Baada ya mapokezi hayo, Mhe. Gauck atafanya mazungumzo ya faragha na Rais Kikwete yakifuatiwa na mazungumzo rasmi. Aidha Marais hao watakutana na Waandishi wa Habari.

Baadaye siku hiyo ya Februari 03, Mhe. Rais Gauck atakutana na Wafanyabiashara, atatembelea Kanisa la Kilutheri la Azania Front, atakutana na Wawakilishi wa Taasisi za Kiraia na kushiriki Dhifa ya Kitaifa itakayoandaliwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Kikwete, Ikulu.

Mhe. Rais Gauck ambaye ameongozana na Mke wake Bibi Schadt, Viongozi Waandamizi kutoka Serikali ya Ujerumani na Ujumbe wa Wafanyabiashara tisa, ataondoka Dar es Salaam kuelekea Zanzibar tarehe 04 Februari, 2015 ambapo atafanya mazungumzo rasmi na Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kabla ya kushiriki kwenye Mkutano wa Kamati ya Pamoja ya Viongozi wa Dini kuhusu Amani. Rais Gauck pia atakutana na Vijana kutoka Ujerumani wanaojitolea katika Programu ya Weltwarts Visiwani humo.

Jioni ya Februari 04, Mhe. Gauck ataondoka Zanzibar kuelekea Mkoani Arusha. Akiwa Mkoani humo siku ya tarehe 05 Februari, 2015 atatembelea Taasisi mbalimbali za kimataifa ikiwemo Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na kuhutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA). Mhe. Gauck na ujumbe wake watatembelea pia Hifadhi ya Wanyama ya Serengeti ambapo atazindua Kituo kipya cha kudhibiti Ujangili.

Mhe. Rais Gauck anatarajiwa kumaliza ziara yake hapa nchini tarehe 06 Februari, 2015 na kuondokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kurejea Ujerumani.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
01 Februari, 2015
 
Inaonekana mleta mada hata media hafuatlii, ikulu toka jana waltoa tarfa ktk media pia leo magazet yameandka ratba ya mgen huyo atakapokuwa tz,ww unasema wamefcha taarfa na kujfanya wa kwanza kuujuza umma.

=======

Duh......mikataba maliasili zetu yaaaaani
 
Mbona magazeti yote ya leo yaliandika kuhusu ugeni huu? Hakuna lililofichwa labda wewe hukusoma magazeti ya maana ya leo.
 
amealikwa na askofu malasusa kuchangia chuo kikuu pale mwenge,ikulu anapita tu kama kariakoo.yuko kidini zaidi.
 
Huku ugeni ni wa chadema kwani hamjui kuwa ujerumani ndio inaifadhili chadema hivyo amekuja kuangalia maendeleo ya cdm tanzania lazima babu slaa utamsikia tu
 
hawa si ndo rafiki zake dr,wAnajipendekeza tena kwa jk?
 
Scramble n partition of Tanganyika part III, asipofika mtwara sijui?
 
  • Thanks
Reactions: 999
Yule wa Urusi vipi ntena? au JK kaogopa mkwara wa Obama?
 
acheni kelele mgeni akija kwako mtendee mema!!! mkaribishe!!!
 
Duh......mikataba maliasili zetu yaaaaani

Si tulionyeshwa picha kuwa, mara baada ya kufika kule aonana na bilgate pamona na angela. Nikahoji kwa nini tusipewe kilichoongelewa na matokeo yake tunapewa mipicha pekee, nikaendelea kusema ina maana uwezi wa waandishi wetu wa tanzania huwa ni kupiga picha pekee katika safari za bosi?
Majuto mjukuu ngoja tusubiri azaliwe.
 
Kwa nini JK akienda Germany hapokelewi hivyo?

Jk ni mbahili hua hatumagi pesa za maandalizi ya mapokezi yake ila wageni kama hawa hua wanatumaga kafungu kakuimarisha ulinzi na shangwe za kupokelewa kwao coz wanajua wasipofanya ivyo unaweza ukalazwa maji matitu guest house
 
Back
Top Bottom