Gerald Hando anatumia vibaya nafasi yake ya utangazaji wa kipindi cha Power Breakfast | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gerald Hando anatumia vibaya nafasi yake ya utangazaji wa kipindi cha Power Breakfast

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by moto ya mbongo, Jul 4, 2012.

 1. moto ya mbongo

  moto ya mbongo JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 336
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 45
  [FONT=&amp]GERALD HANDO ANATUMIA VIBAYA NAFASI YAKE YA UTANGAZAJI WA KIPINDI CHA POWER BREAKFAST CHA CLOUDS FM:[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Katika kumsikiliza Gerald Hando jana 03/JULAI/2012 na leo 04/JULAI/2012 katika segment yao ya JICHO LA NG'OMBE saa 12:55 asubuhi mtangazaji huyu anaonesha kabisa anaeneza propaganda na anatumika kusafisha njia kwa manufaa ya wachache badala ya kutumia nafasi ya chombo cha habari kwa manufaa ya umma.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Jana akizungumzia ishu ya jaribio la kumuua Dr. Stephen Ulimboka alijaribu kuhamisha muelekeo wa jinsi jambo lilivyo kwa kusema kuwa kuchukuliwa kwake (Dr) na kwenda kupigwa kule alikopelekwa msitu wa Pande kuna watu wengine au madaktari wengine walikuwepo kwa hiyo lawama isielekezwe kwa serikali.Jambo hili linahiataji uchunguzi huru ili kuupata ukweli halisi wa jambo hili.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Leo pia katika jicho la ng'ombe ameongea kwa vijembe kuwa katika bunge la bajeti wabunge hawazungumzii masuala ya bajeti na badala yake wanaingiza hoja za kibinafsi(personal) akitolea mfano kuwa mamabo ya mitaani kama kufumaniwa mwishoe yataongelewa bungeni.Jambo hili limeniacha na mshangao mkubwa kwani siku ya jana Bungeni Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA Mheshimiwa John Mnyika alimtaja Mbunge wa Iramba Magharibi kupitia CCM Mheshimiwa Mwigulu Nchemba kuwa alihusika katika wizi wa EPA wa bilioni 133.Nchemba alikanusha na Mnyika amepewa siku 7 za kuthibitisha kauli yake hiyo.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Kitu kinachostaajabisha kwa hawa jamaa akina Gerald Hando na wanaowatumia ni kupinga kitu kama hicho kwa sababu dhaifu eti si muda muafaka kuzungumzia mambo kama hayo napenda kuwauliza wao na wadau wote mnaoisoma thread hii je wananchi wa Tanzania waliobiwa na mafisadi kwa miaka mingi na kudanganywa kuwa masuala hayo ni ishu za usalama wa taifa watatetewa na nani?????Je kuna muda gani muafaka wa kuzungumzia iwapo mambo hayo yameshughulikiwa kwa udhaifu mkubwa na miaka inazidi kuyoyoma jamaa wakiendelea kuzalisha faida na kuficha mapesa katika akaunti za siri ng'ambo?
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Baada ya kampuni ya ukaguzi wa mahesabu ya Delloite & Touche kugundua mwaka ule wanasiasa kwa kushirikiana wafanyabiashara na mabenki ya hapa nchini kupitia benki kuu waliiba mabilioni ya pesa katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

  Kampuni ile ilizuiwa kuendelea na kazi na mambo yalipokuwa moto serikali iliunda tume ya watu watatu Ludovick Utouh Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu wa Serikali ,Saidi Mwema Mkuu wa Jeshi la Polisi na mwendesha mashtaka wa serikali Johnson Mwanyika aliyestaafu kwa sasa.

  Jambo lilelifanywa katika kununua muda(buying time)ili wananchi wasahau na watulie ili mambo yao yaende vizuri.

  Matokeo yake wachache walitolewa mhanga kama akina Rajabu Maranda na Farijala Hussein wakati wale wengine waliambiwa warudishe wengine waasia,mtanzania mwenye asili ya Irani na jamaa zake,wanasheria na wazawa wengine waliachiwa wale keki ya taifa dhidi ya wanyonge wengi wa Tanzania.

  Kukafuatia kauli za mara mafisadi hawakamatiki ni wajanja sana.Nyaraka za usajili wa makampuni yale bandia zilipotea kule BRELA na mabenki kama CRDB,Akiba Commercial Bank yaliyotoa pesa zile hayajatoa majina na ni akina nani walichukua pesa zile usanii uliendeshwa hapo hakuna cha maana kilichopatikana ili kusaidia wananchi na nchi yetu.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Kitu hiki wananchi wengi wanaosikiliza radio hii ya Clouds FM na wenye upeo mdogo wanaona Hando kusema kitu kama hiki ni sawa tu bila kujua kuwa kuna wachache wanaofaidi nchi tena kwa njia haramu na kwa kukandamiza wananchi walio wengi.

  WATANZANIA TUAMKE ILI TUKOMBOKE TUKIRUHUSU WANYONYAJI WEUSI WENZETU KUTUIBIA UTAJIRI WA NCHI NA MEDIA ZINAZOSET AGENDA PIA KUTUMIKA KUTUDANGANYA TUTAISHIA PABAYA.

  TAFAKARI. [/FONT]
   
 2. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Huyo jamaa mbona ni bwabwa, ulikuwa hujui...

  Pia uelewe kuwa anayemlipa mpiga zumari ndiye anayechagua wimbo kwa hiyo hapo anatimiza matakwa ya mabwana zake. Pia hao jamaa wa Clouds wanatekeleza ule usemi maarufu pale CCM wa JIKOMBE UKOMBOLEWE. Radio yenyewe hata Kodi hailipi na TRA wala hawaendi, matangazo ya serikali yanapitia huko mostly na Radio Uhuru na TBC kwa hiyo propaganda ndio malipo yake
   
 3. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ndo anaongea sasa hivi.
   
 4. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Japo summary basi mie niko kwene guta ntaskilizia wapi hio redio Mpwa? mbona wantamanisha bureee weye jamani.
   
 5. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona simsikii.?
   
 6. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #6
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280

  Clouds ndio maharisho ya nani??
   
 7. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mangarinkonekiruuupaa
   
 8. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
   
 9. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nimependa sehemu moja, kuwa baada ya kutekwa Defender ,zilikua zinapita hilo eneo.Ila Jambo moja lililonisikitisha ni namna Gerald toka jana alivyowaandaa watu kisaikolojia kuhusu DR.Deo.Yaani asilimia kubwa ya wasikilizaji wa Clouds wanaanza kumsuspect Dr.Deo, while kumbuke Ulimoka alimchagua yeye kati ya wale Madr.wengine.
  Lakini pia nimependa location,Kova alituambia ni Leaders Club, while Jamaa anatuambia karibia na Ultmate Security pale Tunisia.
   
 10. K

  KISWAHILI Member

  #10
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanamtumia.....
   
 11. L

  Lugeye JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 1,080
  Likes Received: 1,378
  Trophy Points: 280
  kazi yao ni kuandaa barthday party kwa baba mwanaisha unategemea nn hapo washenz wakubwa hao
   
 12. S

  Shambano Member

  #12
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  katumwa na mabwana zake huyo
   
 13. A

  AZIMIO Senior Member

  #13
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Redio siku hizi ni moja tu,MAGIC FM kwa asubuhi kila kitu unakipata ukianzia na magazeti,kuchangia mada kwa uwazi kwa kupiga simu,akiingia Google aka Kibwana Dachi RAHA KABISA, Michezo,yaani wana kila kitu,HAMENI HUKO MIMI NIMESHAHAMA SIKU NYINGI.
   
 14. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kweli me niliposkia huyu Hando akiongea utumbo wake nilibadiri station, sikuwa na haja ya kusikiliza ujinga wake. anafikiri Watanzania wote ni mbumbu km yeye. eti kuzungumzia EPA ni kuwatoa kwenye mada ya budget. nina wasi wasi km radio hii haukupata finance kwenye hihela ya EPA. kipindi fulani nilimsikia akimtukana Samwel Sita wakati ametemwa kwenye u-speaker. bila shaka dogo hoyu analamba soli za watu ili apate kula na familia yake.
   
 15. D

  DCM Senior Member

  #15
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 165
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Anataka ukuu wa wilaya huyo,lazima ajikombe si unajua na jamaa akisikia huwa ajali merits ili mradi kajipendekeza utasikia keshateuliwa mkuu wa wilaya.
   
 16. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Mambo yote MORNING MAGIC.. Kibwana Dachi namkubali sana..
   
 17. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Thanks kutujuza kuanzania sasa nahamia Margic FM.
   
 18. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  choko huyo alafu nae nasikia wadudu wmeanza kumla kama kibonde
   
 19. Utotole

  Utotole JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 6,344
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Hivi ni kweli hawalipi kodi hawa jamaa, na TRA wapo tu? Halafu tunasema hatuna pesa za kutosha kuiendesha nchi wakati tunazifuja wenyewe?
   
 20. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  Klauds niliipenda enzi izo siku hizi hapana nasikiliza baadhi ya vipindi tu,
  inanichefua zaidi pale akianza tu kuongea gerald hando real huwa ninachange stesheni,
  huyu anatumiwa vibaya, nahisi uko mbeleni tutaanza kuwaadhibu wabaya wetu kama vibaka tukikutana nao mitaani, maana uyu dogo anatukejeli kila siku watanzania,
  na ninaamini ni maskini kama sisi tu kwani kazi iyo ya kutangaza naamini ni kazi ya kawaidi tu
   
Loading...