Ushauri wa Gerald Hando kuhusu tiktok ni mwiba kwa uhuru

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Asubuhi nilikuwa nasikiliza redio ambapo hawa ndugu zetu walikuwa wanajadili suala la dawa za kulevya ambapo waathirika na wanaotuhumiwa watapimwa. Katika kuelezea hilo mmoja wa watangazaji, Gerald Hando akasema jambo liende kwa wizara na TCRA.

Jambo lake ni kuwa Tiktok inaharibu vijana na watoto. Kwa hoja yake ni kuwa marekani inajaribu kuzuia tiktok sio tu kwa masuala ya taarifa binafsi lakini pia kulinda watoto.

Mimi napata shida na namna yoyote inayojiweka mbele kupinga teknolojia badala ya kutafuta namna bora za kutumia digital kukuza demokrasia.

Kama ambavyo baadhi ya mitandao imezuiwa nchini, naona kabisa tunaenda kuzuia mitandao mingi zaidi kwa sababu hizi zinazotolewa na wadau ambazo hazina mashiko.

Nawasilisha.
 
Marekani hawajaribu kuzuia tiktok kwa sababu za maadili, ni uongo mkubwa na upotoshaji unaofanywa na huyo hando.
Tiktok inaandamwa Marekani kwa sababu za kisiasa tu.
 
Asubuhi nilikuwa nasikiliza redio ambapo hawa ndugu zetu walikuwa wanajadili suala la dawa za kulevya ambapo waathirika na wanaotuhumiwa watapimwa. Katika kuelezea hilo mmoja wa watangazaji, Gerald Hando akasema jambo liende kwa wizara na TCRA.

Jambo lake ni kuwa Tiktok inaharibu vijana na watoto. Kwa hoja yake ni kuwa marekani inajaribu kuzuia tiktok sio tu kwa masuala ya taarifa binafsi lakini pia kulinda watoto.

Mimi napata shida na namna yoyote inayojiweka mbele kupinga teknolojia badala ya kutafuta namna bora za kutumia digital kukuza demokrasia.

Kama ambavyo baadhi ya mitandao imezuiwa nchini, naona kabisa tunaenda kuzuia mitandao mingi zaidi kwa sababu hizi zinazotolewa na wadau ambazo hazina mashiko.

Nawasilisha.
Si TikTok pekee hata upuuzi uitwao Instagram, Telegram, Facebook ni uozo mtupu.

JF, LinkedIn, Sky sports, Goal.com ndiyo Apps sahihi kidogo na Twitter.
 
Tusipokuwa makini na mambo ya uhuru, tunatengeneza kizazi bomu kweli. Instagram ishamal;izana na mabinti maana asilimia kubwa sasa ni wadangaji wanatafuta maisha wanayoona wenzao wanayapost Instagram.
Nyie ambao hampendi uhuru hamieni Korea Kaskazini, Afghanistan, Iran, China na nchi za mfano huo. Msitake kuwaweka watu wote kwenye chungu cha ujima, udikteta na ufashisti.
 
Back
Top Bottom