George w bush anatafuta nini Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

George w bush anatafuta nini Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WILSON MWIJAGE, Dec 16, 2011.

 1. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mpaka sasa Nchi ya Marekani iliyopata uhuru mwaka 1776 imeishaongozwa na marais 44 wakati Tanzania iliyopata uhuru mwaka 1961 imeongozwa na marais 4 tu. Marais wote wa Tanzania wamekwenda Marekani mara nyingi sana tofauti na wenzao wa Tanzania. Nitaongelea marais 10 tu wa Marekani ambao wanaendana na uhuru wa Tanzania. Tukianza na rais wa 35 John F. Kennedy aliyetawala Marekani tangu 1961 - 1963 mpaka rais wa sasa Barrack Obama aliyeanza kutawala tangu 2009 mpaka sasa. Ni rais mmoja tu 'George W. Bush' ambaye ameitembelea Tanzania mara nyingi.

  KWANINI Bush? " Vyandarua, kuzindua hospitali ya Ocean road, kuangalia saloon iliyopo Kinondoni au kuna kingine nyuma ya pazia ukizingatia kwamba Tanzania inajiandaa kufanya biashara ya gesi/mafuta?, anatauta nini?? Tafadhali nijuze!
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Nadhani urekebishe hapo ili nami nipate mwelekeo wa kuchangia!
   
 3. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2011
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sentensi hii ilipaswa kusomeka hivi;
  "Marais wote wa Tanzania wamekwenda Marekani mara nyingi sana tofauti na wenzao wa Marekani" na sio
  Marais wote wa Tanzania wamekwenda Marekani mara nyingi sana tofauti na wenzao wa Tanzania.

  Nashukuru kwa kuliona
   
 4. m

  matawi JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Uraniam huo unamtoa udenda mzee wa watu
   
 5. String Theorist

  String Theorist JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 203
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  anafuatilia ule mpango wa kujenga military base pale kigamboni ambapo kwa juu utajengwa mji wa kigamboni. Also kuna mikataba ya kuchimba uranium hakumalizia kusign.
   
 6. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kikwete analojibu.
   
 7. status quo

  status quo Member

  #7
  Dec 16, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  nimeshtushwa sana na kitendo cha baadhiya watanzania kumtuhumu ndugu george bush baada ya kufanya ziara yake hapa nchini wiki kadhaa zilizopita. kwa wale msiomjua bush naomba niwape historia fupi ya huyu mtu, bush alizaliwa new haven, Connecticut mwaka 1946, akiwa mtoto wa kwanza wa george h w bush.

  alipata elimu ya msingi na sekondari huko houston, texas na baada ya kumaliza masomo alijiunga na chuo kikuu cha yale, na lifanikiwa kutunukiwa digrii ya historia. na baadaye mwaka 1973 alijunga na chuo kikuu cha havard ambako alitunukiwa MBA. katika kipindi hiki chote bush aliishi maisha ya utukutusana akijingiza katika makundi mabaya na kupelekea kuwa mlevi wa kupindukia na jambo hili likamfanya kukosana na baba yake mzazi ambaye kipindi hcho alikuwa afisa mkubwa wa serikali.

  maisha ya george bush yalibadilika mwaka 1986 ambapo alikuwa akigombea nafasi ya ujumbe katika bunge la marekani yaani 'congress', katika uchaguzi huo mpinzani wake alimtuhumu juu ya kitendo cha kuwanunulia pombe wanafunzi wa chuo fulani katika jimbo hilo ili wampigie kura, kwa sababu jimbo hilo lilikuwa na watu wengi ambao walichukia ulevi kwasababu ya imani yao ya kikristo, bush alianguswa vibaya na akajutia sana jambo hilo ndipo akaamua kuokoka mwaka huo (1986), baada ya kuokoka bush alibadilika sana kiasi cha kumshanga sana baba yake ambaye awali walikuwa hawaelewani kabisa.

  bush alichaguliwa kuwa governor wa jimbo la texas mwaka 1994 na alishika wadhifa huo hadi pale alipochaguliwa kuwa raisi mwaka 2000. akiwa madarakani bush alibadili sera za chama chake cha republican ambazo zilizuia msaada kwa nchi nyingi ikiwamo tanzania na hii ni kutoka na na vita baridi, mmoja wa watangulizi wake ronald reagan aliwahi kusitisha msaada kwa tanzania mwaka1981 kwa sababu ya nchi kuwa karibu sana na nchi za kikomunisti,

  lakini george bush aliamua kubadili sera hiyo na ndio maana marekani ilitoa msaada mkubwa kwa tanzania enzi za utawala wake. na watanzania lazima mjue kuwa wenzetu hawa ni watoaji sana na hii ni kwa sababu ya kanuni ya kibiblia aliyo iweka MUNGU, " ni heri kutoa kuliko kupokea".

  hivyo ujio wa bush ni muendelezo wa utoaji ambao bush anaufanya ili ampendeze Mungu na si vinginevyo, hivyo nawaomba watanzania mbadili mtazamo juu ya ziara za bwana bush nchini, bush ni mtu mwema si kama mnavyo fikiri,

  nawasilisha.
   
 8. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,654
  Likes Received: 3,301
  Trophy Points: 280
  Na cameron yupo mbioni kuja kuangalia tumefikia wapi kuhusu ile issue
   
 9. libent

  libent JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  naona wewe humjui vizuri mwanachama huyu wa freemason angalia usipumbazwe na hiyo misaada. Nashut down
   
 10. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa. Heri kutoa kuliko kupokea. Tuambie Bill Gates naye alikuja kimyakimya kufanya nini?
   
 11. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  yuko kibiashara zaidi...na ni kweli yeye ni mfanya biashara mzuri sana katika sekta ya energy na mafuta...na vyote si ni hot cake Tz?
   
 12. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,261
  Trophy Points: 280
  Siku nyingine tumia button ya kuedit tu inatosha, kuliko kupost bandiko lingine halafu kule juu kunabaki na maandishi yale yale! au hauoni hapo chini ya thread yako kuna option ya kuedit?
   
Loading...