Geor Davie ni nani?

ASKOFU na Nabii George David ?€˜Geordavie?€™ wa Kanisa la Geordavie Ministry ?€˜Ngurumo ya Upako?€™ lililoko jijini Arusha na Kawe, Dar. Kwa sasa ndie anaaminika kuwa ndiye Askofu mwenye utajiri mkubwa na Ulinzi wa hali ya juu, Kuna watu wengine wamefananisha ulinzi wake kama wa Viongozi wa juu serikalini.

Mbali na kulindwa na walinzi wake binafsi pia hulindwa na Polisi (FFU) ili kumhakikishia amani na ulinzi wa kutosha kila
mahali anapokuwa. Waumini wake wengi wanapata wakati mgumu kumuona na kuongea nae kwasababu ya ulinzi huu
mkali alio nao huyu askofu.

GEORDAVIE1.jpg


Mbali ya kuwa na chopa iliyokuwa ikiimarisha ulinzi ambayo ameinunua hivi karibuni, askofu huyo alikuwa na msururu wa magari yenye thamani kubwa yanayomfanya kutajwa kuwa tajiri kuliko maaskofu wengine wanatoa huduma katika makanisa ya kiroho Tanzania.

Akiwa Karatu, mbali na ulinzi binafsi, Geordavie alikuwa akilindwa na askari wa jeshi la polisi, askari kanzu, Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa usalama barabarani.

GEORDAVIE10.jpg
 
Niliwahi kusikia kuwa pia ndiye baba mzazi wa producer Nisher! Kuna kaukweli kidogo hapo?
 
kitu alichoharibu alikua anatembea na mke wa mtu mpaka akasababisha mwenye mke akachanganyikiwa
 
Duu ila sawa tu, vibaka wasiibe sadaka na vipi kuhusu sadaka, nikuanzia sh. gapi?
 
Kwa kawaida shetan huwa ana nguvu sana unatakiwa ufanye kaz ya ziada kuepuka vishawishi vyake!
 
Wewe ni mfuasi wake halafu unauliza!!!!!
Sio mfuasi huyo ndio mwanae anatengeneza mangoma na kina jomakini. ''utawatambua kwa matunda yao''

ukimsikiliza hauwezi kuamini ndio kijana wa mchungaji, na baba yake naye wameendana kama wasela tu.

wateule muwe macho hizi ni nyakati za mwisho na manabii wa uongo ndio kama hawa.
 
Nabii GeorDavie ni mtumishi wa Mungu na huduma yake ipo Arusha Kisongo na ni Kilomita 13 kutoka mjini Arusha njia ya kwenda Dodoma na ni baada ya uwanja wa ndege tu. Huduma yake inaitwa "Ngurumo Ya Upako" na ni kati ya watumishi wa Mungu ambao wana Upako wa kipekee amabo umekuwa gumzo kwa watu wengi. Mungu ana njia nyingi sana ya kujidhihirisha kwa wanadamu na kama wakati wa zamani za kale aliwatumia watu mbali mbali kwa namna tofauti na hivyo hivyo kwa Nabii GeorDavie.

Watumishi wa Mungu ktk biblia walilingwa kwa kumuhubiri Kristo Yesu( injili) na walitambulika kwa miujiza waliyokuwa wakifanya hadi ikafikia hatua ya watu kutaka kuwasujudia kama miungu ila walikataa na kujinyenyeza zaidi. Ila sio huyu baba yako anayelaumiwa kwa wizi, kufarakanisha ndoa, miujiza fake na ya kubahatisha, uzinzi na usanii mwingi. Kama ni Mtumishi wa Mungu aliye hai walinzi wa nini?. Je lipi kubwa alilofanya huyo nabii anayewatabiria wanawake wachumba ati Dada umelia sana mungu anakwenda kukupa mume wakati akijua kuwa nowadays we have relationship crisis lipi alilobalo la kumzidi mtu wa Mungu Moses Kulola ambaye hakuwahi kuwa hata na yelo kwake wa kumlinda( apumzike kwa amani). Ninaimani hatakanyaga tena Mwanza kwa Jina la Yesu mfufuka namfungia hapo Arusha na hata toka hapo mpaka kazi yake itakapofikia mwisho . Nasema haya kwa mafuta halisi ya kinabii . Amen.
 
Back
Top Bottom