Genius ni mojawapo wa aliens wa kificho?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,114
22,566
Salaam, Shalom!

Kwanini watu waliotokea kuwa na akili nyingi sana tangu utotoni huitwa geniouses?

Je watu hao, Wana mahusiano yoyote na aliens Kutoka Ulimwengu mwingine?

Na kwanini watambulike kama geniuses wakati Kwa kawaida genius ni Neno linalotokana na genie au jini/ majini?

Kwanini waitwe genius Badala ya intelligent, au Kuna tofauti kati ya watu hao wawili?

Karibuni🙏
 
Jiniazi ni mdadisi tu 'curious' tu hamnaga kipya.

Mi nimewasoma sana hao majiniazi (nimejisoma) hadi kugundua kuwa. Maana mi mwenyewe ni jiniazi (potelea mbali atakayemaindi)

Udadisi ndo akili, ndo ujiniazi.

Muda si mrefu nikaja kumsikia jiniazi mwenyewe aliyethibitishwa, kwamba huo ndio ukweli. Ni UDADISI TU hakuna kubwa la ziada sana ya hapo
Screenshot_20240229-161916_Chrome.jpg

Kama ambavyo matajiri wakubwa ni ile kuiishi tu sifa yao ya 'utafutaji mali endelevu'
Basi vivyo hivyo majiniazi wakubwa, ni vile tu kuiishi sifa yao ya 'utafutaji maarifa endelevu'

Mshauri binafsi wa vijana - Taifa
 
Kwanini watu waliotokea kuwa na akili nyingi sana tangu utotoni huitwa geniouses?
Duniani kuna maarifa mengi, yanamsubiri atakayeyatafuta ayatumie naye ataitwa jiniazi. Mdadisi

Kama ambavyo duniani kuna mali nyingi, zinamsubiri atakayezitafuta na azitumie ataitwa tajiri. Mtafutaji.

Wote ni watu kama watu wengine. Tabia zao tu. To be is to do, to do is to be.
 
Genius maana yake yeye hajioni ukiona wewe unajiona ni Genius fahamu tu wewe sio genius

Maana Mimi nikikutazama nikaona unafanya vitu ambavyo Mimi siwezi kufanya ntakuita Genius.
 
Duniani kuna maarifa mengi, yanamsubiri atakayeyatafuta ayatumie naye ataitwa jiniazi. Mdadisi

Kama ambavyo duniani kuna mali nyingi, zinamsubiri atakayezitafuta na azitumie ataitwa tajiri. Mtafutaji.

Wote ni watu kama watu wengine. Tabia zao tu. To be is to do, to do is to be.
Exactly hilo ndio lilikuwa jibu la ‘Richard Feynman’ alipoulizwa are you special. Jibu lake likikuwa hapana yeye ni mtu wa kawaida tu sema alipenda physics toka akiwa mdogo na kusoma sana kwa bidii.

Akaongezea uelewa alioupata huko ndio umemjengea msingi kuja na ideas mpya za physics. Lakini hana tofauti na mtu mwingine yeyote zaidi ya bidii na muda mwingi aliotenga kusoma physics.
 
Wengi wao ni mareptile yaani watu mijusi au transformers watu wanachukua idea kupitia ulimwengu wa maono na kuzigeuza in real world
 
Halafu magenius siku hizi hawapo tena?? Zaidi ya hawa hawa tunaowasomaga kwenye vitabu mbona hamna wapya???.....hadi kuna muda nahisi hii dunia mengi ni maigizo hamna ukweli
Ingia kwenye documentary za ubunifu na uvumbuzi utawaona
 
Exactly hilo ndio lilikuwa jibu la ‘Richard Feynman’ alipoulizwa are you special. Jibu lake likikuwa hapana yeye ni mtu wa kawaida tu sema alipenda physics toka akiwa mdogo na kusoma sana kwa bidii.

Akaongezea uelewa alioupata huko ndio umemjengea msingi kuja na ideas mpya za physics. Lakini hana tofauti na mtu mwingine yeyote zaidi ya bidii na muda mwingi aliotenga kusoma physics.
Hakika 👊
 
Back
Top Bottom