Gen Z Uprising 2026: Global Updates Mega thread - Yanayojiri

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,041
Reaction score
8,425
Maandamano ya wanafunzi nchini France (yaliyoanza Septemba 2026) ni sehemu tu ya hadithi. Europe kumechangamka, wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vikuu wanaingia mitaani wakikosoa kuzorota kwa mazingira ya elimu na mapungufu ya mfumo kiujumla.

The student protests in France are only part of the story. Across Europe, high school and uni...webp

Kuanzia Belgium hadi Albania, Greece hadi Ireland (kuanzia Septemba na Oktoba 2026), wanafunzi wanahamasishana kudai elimu bora, ufadhili zaidi, na kuondoa/kumaliza ukosefu wa usawa katika jamii. Baadhi ya waandamanaji wamezikosoa serikali zao kwa kuweka zaidi nguvu zao kwenye vita badala ya elimu. Katika viwanja vya Albania, ujumbe ni mkali zaidi: "Kile ambacho Albania inahitaji ni mapinduzi, mabadiliko. Haiwezi kuendelea hivi."

Nchini Germany, (mnamo Septemba 25, 2026) zaidi ya wanafunzi 45,000 waliandamana katika miji takriban 100 kupinga mpango wa serikali kurejesha sheria ya lazima ya vijana kujiunga na jeshi. Walipinga shule kutumika kama sehemu ya kuandaa wanajeshi, wakisisitiza uhitaji wa uwekezaji kwenye elimu badala ya vitani. Shule zimevamiwa na kukaliwa, au majaribio ya kufanya hivyo yamefanyika katika miji ya Hamburg na Berlin.

Nchini Italy, maandamano yalifikia kilele mnamo Oktoba 16 - 17, 2026 (katika kile kilichoitwa "No Meloni Day), ambapo zaidi ya vijana 400,000 waliingia mitaani katika miji mikubwa kama Turin, Naples, Rome, na Bologna, wanafunzi walipinga sera za elimu za Waziri Mkuu Giorgia Meloni, ongezeko la matumizi ya kijeshi, na sheria mpya ya kupunguza idadi ya wanafunzi wahamiaji mashuleni, huku vurugu zikiibuka na kusababisha baadhi ya watu kujeruhiwa. Wanafunzi nchini Greece nao wakihusisha maandamano yao (Oktoba 2026) na yale ya Ufaransa.

Nchini Spain (Oktoba 14, 2026), mgomo wa walimu usio na kikomo ulitangazwa, wakidai mishahara mizuri na mazingira bora ya kujifunzia kwa wanafunzi. Maandamano ya kutetea elimu ya umma pia yalifanyika katika Chuo Kikuu cha Complutense cha Madrid, ambapo polisi wa kutuliza ghasia waliwatawanya waandamanaji.

Baadhi ya uhamasishaji umechukua muda mrefu zaidi ya siku au wiki chache. Nchini Serbia, kufikia Oktoba 2026, wanafunzi wamekuwa wakiandamana kwa miaka miwili dhidi ya ufisadi, uzembe, na ukosefu wa uwazi. Yote yalianza baada ya kuporomoka kwa kituo cha treni na kuua watu 16, tukio ambalo lilikuja kuashiria hasira ya umma juu ya kudorora kwa taifa.

Wakati huo huo, nchini Austria, maelfu wameingia mitaani tangu kuanza kwa mwaka wa masomo (Septemba 2026) kupinga sheria inayowapiga marufuku wasichana walio chini ya umri wa miaka 14 kuvaa hijabu. Wanafunzi na wafuasi wanashutumu ubaguzi wa rangi na unyanyasaji, wakiwa na ujumbe wazi: "Kichwa changu! Hijabu yangu! Uamuzi wangu!"

The student protests in France are only part of the story. Across Europe, high school and unive.webp

1792332311075.png

Kwa upande mwingine, mnamo Oktoba 15 - 16, 2026, maandamano huko Buenos Aires (Argentina) yaliyokuwa yakidai kuongezwa kwa ufadhili wa vyuo vikuu vya umma yaliishia katika mapigano kati ya waandamanaji na polisi wa kutuliza ghasia. Maafisa walifyatua risasi za mpira, kutumia mizinga ya maji na kupiga mabomu ya machozi, huku waandamanaji wakirusha mawe na fataki. Maandamano hayo yanalenga serikali ya Rais Javier Milei na utekelezaji wake wa sheria inayorekebisha ufadhili kwa vyuo vikuu vya umma, kufuatia miezi kadhaa ya migomo, maandamano vyuoni na maamuzi ya mahakama.

Februari – Machi 2026, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop, Senegal walifanya migomo mikubwa kupinga ugumu wa maisha, kufungwa kwa chuo, na kudai haki zao za msingi.

Agosti – Septemba 2026, wimbi la maandamano lililipuka katika jimbo la Jharkhand, India ambapo wanafunzi waliingia mitaani kupinga vikali ufisadi, udanganyifu, na kuvuja kwa mitihani ya ushindani ya serikali.

Kote ulimwenguni, wito wa mabadiliko makubwa unazidi kupaza sauti. Utawala na njia zilizokuwa zikitumika nyuma haziomeshi kufanya kazi tena. Tawala zetu za Africa zinaona na kujifunza kutoka kwenye haya? Kama mpaka Watanzania walitoka kuandamana, je wanafikiri wanaweza kuendelea kufanya yale yale na kupata matokeo mapya?

Tutarajie kupata mifumo mipya ya Utawala yenye kujali, kuzingatia na kuonyesha kwa vitendo misingi ya Haki na Uwajibikaji?
 
Wapunguze au wakate misaada kabisa, pesa zote iwe za misaada ya kijeshi, kibinadamu waikate waboreshe upungufu huo, mambo ya kusaidia nchi au watu wa mataifa mengine Kwa Makosa au uzembe walioufanya wenyewe sio ishu kabisa....

hebu fikiria nchi kama za Kiafrika Hadi Leo zinalamba misaada Kila kukicha, misaada ya kijeshi kibao inatolewa bureee kabisa, sawa kuna return unayotegemea kurudi but hiyo return inarudi Kwa matajiri wachache ambao wao na familia zao wanasomesha watoto wa kwenye elite schools....
 
Yatafika tu mpaka huku, kwa sababu Vijana maisha wanayopitia wanaona hawana cha kupoteza. Kama hapa nchini kwetu maigizo na ujinga mwingi sana.

Hivi yule Waziri wa Vijana mbona naona kama kapotea hivi ?
Ipo siku ...... Waziri baada ya kupiga shoo ya kuwapa matumaini vijana, anaendelea na mishe zake!
 
Huo ni ujinga kabisa hivi Mkuu unakumbuka pale Tunisia yule Mmchinga na migambo wa jiji ?

Siku zote huwa nasema yule Mmachinga wa Tunisia atabaki shujaa wa vijana wengi wanaonyimwa haki zao japo alijilipua na mafuta ya taa. Lakini balaa lilitokea lilisababisha mabadiliko nchi nyingi za kiarqbu
 
Maandamano ya wanafunzi nchini France (yaliyoanza Septemba 2026) ni sehemu tu ya hadithi. Europe kumechangamka, wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vikuu wanaingia mitaani wakikosoa kuzorota kwa mazingira ya elimu na mapungufu ya mfumo kiujumla.

Kuanzia Belgium hadi Albania, Greece hadi Ireland (kuanzia Septemba na Oktoba 2026), wanafunzi wanahamasishana kudai elimu bora, ufadhili zaidi, na kuondoa/kumaliza ukosefu wa usawa katika jamii. Baadhi ya waandamanaji wamezikosoa serikali zao kwa kuweka zaidi nguvu zao kwenye vita badala ya elimu. Katika viwanja vya Albania, ujumbe ni mkali zaidi: "Kile ambacho Albania inahitaji ni mapinduzi, mabadiliko. Haiwezi kuendelea hivi."

Nchini Germany, (mnamo Septemba 25, 2026) zaidi ya wanafunzi 45,000 waliandamana katika miji takriban 100 kupinga mpango wa serikali kurejesha sheria ya lazima ya vijana kujiunga na jeshi. Walipinga shule kutumika kama sehemu ya kuandaa wanajeshi, wakisisitiza uhitaji wa uwekezaji kwenye elimu badala ya vitani. Shule zimevamiwa na kukaliwa, au majaribio ya kufanya hivyo yamefanyika katika miji ya Hamburg na Berlin.

Nchini Italy, maandamano yalifikia kilele mnamo Oktoba 16 - 17, 2026 (katika kile kilichoitwa "No Meloni Day), ambapo zaidi ya vijana 400,000 waliingia mitaani katika miji mikubwa kama Turin, Naples, Rome, na Bologna, wanafunzi walipinga sera za elimu za Waziri Mkuu Giorgia Meloni, ongezeko la matumizi ya kijeshi, na sheria mpya ya kupunguza idadi ya wanafunzi wahamiaji mashuleni, huku vurugu zikiibuka na kusababisha baadhi ya watu kujeruhiwa. Wanafunzi nchini Greece nao wakihusisha maandamano yao (Oktoba 2026) na yale ya Ufaransa.

Nchini Spain (Oktoba 14, 2026), mgomo wa walimu usio na kikomo ulitangazwa, wakidai mishahara mizuri na mazingira bora ya kujifunzia kwa wanafunzi. Maandamano ya kutetea elimu ya umma pia yalifanyika katika Chuo Kikuu cha Complutense cha Madrid, ambapo polisi wa kutuliza ghasia waliwatawanya waandamanaji.

Baadhi ya uhamasishaji umechukua muda mrefu zaidi ya siku au wiki chache. Nchini Serbia, kufikia Oktoba 2026, wanafunzi wamekuwa wakiandamana kwa miaka miwili dhidi ya ufisadi, uzembe, na ukosefu wa uwazi. Yote yalianza baada ya kuporomoka kwa kituo cha treni na kuua watu 16, tukio ambalo lilikuja kuashiria hasira ya umma juu ya kudorora kwa taifa.

Wakati huo huo, nchini Austria, maelfu wameingia mitaani tangu kuanza kwa mwaka wa masomo (Septemba 2026) kupinga sheria inayowapiga marufuku wasichana walio chini ya umri wa miaka 14 kuvaa hijabu. Wanafunzi na wafuasi wanashutumu ubaguzi wa rangi na unyanyasaji, wakiwa na ujumbe wazi: "Kichwa changu! Hijabu yangu! Uamuzi wangu!"

Kwa upande mwingine, mnamo Oktoba 15 - 16, 2026, maandamano huko Buenos Aires (Argentina) yaliyokuwa yakidai kuongezwa kwa ufadhili wa vyuo vikuu vya umma yaliishia katika mapigano kati ya waandamanaji na polisi wa kutuliza ghasia. Maafisa walifyatua risasi za mpira, kutumia mizinga ya maji na kupiga mabomu ya machozi, huku waandamanaji wakirusha mawe na fataki. Maandamano hayo yanalenga serikali ya Rais Javier Milei na utekelezaji wake wa sheria inayorekebisha ufadhili kwa vyuo vikuu vya umma, kufuatia miezi kadhaa ya migomo, maandamano vyuoni na maamuzi ya mahakama.

Februari – Machi 2026, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop, Senegal walifanya migomo mikubwa kupinga ugumu wa maisha, kufungwa kwa chuo, na kudai haki zao za msingi.

Agosti – Septemba 2026, wimbi la maandamano lililipuka katika jimbo la Jharkhand, India ambapo wanafunzi waliingia mitaani kupinga vikali ufisadi, udanganyifu, na kuvuja kwa mitihani ya ushindani ya serikali.

Kote ulimwenguni, wito wa mabadiliko makubwa unazidi kupaza sauti. Utawala na njia zilizokuwa zikitumika nyuma haziomeshi kufanya kazi tena. Tawala zetu za Africa zinaona na kujifunza kutoka kwenye haya? Kama mpaka Watanzania walitoka kuandamana, je wanafikiri wanaweza kuendelea kufanya yale yale na kupata matokeo mapya?

Tutarajie kupata mifumo mipya ya Utawala yenye kujali, kuzingatia na kuonyesha kwa vitendo misingi ya Haki na Uwajibikaji?
Uprising....
Worldwide
 
Back
Top Bottom