Gen Z, Kitu gani mnawashangaa Millennials?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,417
Reaction score
5,020
Kumekuwa na hali ya kila kizazi kukishangaa kizazi kingine, mfano Millennials wengi wanawashangaa namna Gen Z wanavyochukulia mambo, wanaona kama wanayachukulia kwa wepesi hata kama yanaonekana mazito na namna hawakubali kupelekeshwa ili akusikilize inabidi umpe sababu yenye mashiko haijilishi umri wako, tofauti na wao ilikuwa ilmradi aliyesema ni mkubwa basi analazimika kusikiliza.

Je, Gen Z kipi kinawashangaza au kinawafanya muwaone Millennials walikuwa wanazingua wakati wao?
 
Achana na sisi milli. Sisi ndio tumewafundisha maujanja na kawaida mwanafunzi huwa kiwembe kuzidi teacher. Na ndio furaha ya kila mwalimu sio kutengeneza vilaza. Gen_Z oyeeee
 

Gen Zero kwa kujiamlia mambo! Mpaka tuwatie laana nyie🙌🏾
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…