luhala
JF-Expert Member
- Feb 25, 2012
- 412
- 142
Hapana, mimi siamini hivyo hata kidogo kwani wapo wengi tu wanaochukia ufisadi lakini wamebanwa na system. Gen. Sarakikya si mmoja wa hao unaowasema kwani ameonekana wazi kutojihusisha na siasa tangu atajwe tajwe kuhusika na jaribio la mapinduzi la kwanza 1971.Wakubwa wote wa JWTZ ni Mafisadi wa CCM, au umesahau Shimbo na mkwala wake kwenye uchaguzi wa 2010?
Wapo wengi tu wanaochukia ufisadi ndani ya CCM na wapo walio risk kuweka wazi misimamo yao hiyo baada ya kustaafu lakini CCM waliwatisha kuwanyanyasa na kuwabana warudi "kundini" angalau kimwili. Wapo waliobaki adamant (Shupavu) hadi mwisho wa maisha yao kama Hayati Col. Mwasomola na wapo walioamua kurejea nyuma kama Hayati Gen. Marwa ambaye mwaka 1995 alivunja ukimya na kuamua kuitumia haki yake ya msingi ya kujiunga na kikundi au chama chochote ili mradi havunji sheria pale alipoamua kujiunga na CHADEMA na kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA jimbo la Tarime. Nakumbuka jinsi Mzee yule alivyobanwa na vyombo vya dola ili arudi CCM. Walianza na kutumia vyombo vya dola "kuvuruga kampeni zake na kuhakikisha anaaibishwa kwa "kushindwa" kwa kishindo na baada ya hapo kutishia kusimamisha pensheni na ruzuku alizokuwa akipokea toka serikalini kwa ajili amekuwa "mwanasiasa". walifika mbali zaidi kumpiga marufuku kuingia katika kambi yoyote ya JWTZ kwa sababu ni mwanasiasa wakati ule ule kina Kikwete, Komba na wengine kibao walikuwa wakiingia na kutoka kwenye kambi za JWTZ watakavyo licha ya kujiuzulu JWTZ kwa minajili ya kujiunga na siasa! Alifanya Tactical withdrawal na kurejea CCM ambapo mara moja vikwazo vyote na mizenggwe aliyowekewa iliondolewa. Alipata kuniambia binafsi kwamba katiba tuliyokuwa nayo ilikuwa dhaifu kiasi cha kutoweza kusimamia kilichotamkwa nayo na aliamini (Ingawa nilikuwa namwona kama anayeota) kwamba siku moja nchi itakuwa na katiba mpya na imara. Alikufa wengi wakiamini ni mwanaCCM safi lakini moyoni Mzee yule alivutiwa sana na siasa za CHADEMA. CHADEMA wana haki ya kujivunia shujaa huyu na angalau kumtaja kama mmoja wa waasisi wa siasa za upinzani nchini aliyehatarisha maisha yake na familia kuonyesha hisia zake dhidi ya ufisadi wa CCM.