GDP ya Tanzania na matajiri wake

GDP ya Tanzania na matajiri wake

Comment ya juu imejibu comment yako hii, comprehension bado ni janga la Taifa, Soma uelewe. Na si kila mtu ni lumumba na Chadema, hutaniona kokote kwenye hivyo vyama vyenu.
We taka taka akili za lumumba kwani hatuzijui,si zimejaa kinyesi tu
 
Takwimu zinaweza kutofautiana kutokana na chanzo cha taarifa na sababu zinginezo.

Kwa mujibu wa IMF, GDP ya Tanzania ni dola [za Kimarekani] bilioni 85.

Kuna watu huwa wanadai Tanzania kuna hela na Watanzania wana hela.

Okay, sawa. Labda sisi wengine tuonavyo tofauti huwa hatuelewi, hatujui, au yawezekana tuna matatizo mengine tu.

Ukiwasikiliza wanaodai kuwa Watanzania wana hela, unaweza kudhani Tanzania ndo nchi yenye uchumi mkubwa zaidi duniani.

Watanzania wananunua na kujenga majumba ya mabilioni ya dola [au ni shilingi?]. Hivyo, Watanzania wana hela.

Sasa, pengine kwa ujinga wangu mimi, nauliza hivi:

Hivi nchi kama Tanzania yenye GDP ya dola bilioni 85 [kwa muktadha tu, Marekani ina GDP ya dola trilioni 30], inaweza kuzalisha matajiri wenye utajiri zaidi ya dola bilioni 85?

Yaani Tanzania yenye GDP ya dola bilioni 85, iwe na matajiri wenye utajiri wa zaidi ya dola bilioni 85, tuseme labda bilioni 90, bilioni 100, na kadhalika?

Hilo linawezekana kweli?

The math ain’t mathing, please make it make sense.
Yaani mmiliki wa amazoni tu anamiliki bilioni zaid ya 100 . Kwa maana hiyo tajiri mmoja wa marekani anamiliki zaidi ya uchu wa tanzania .
 
Back
Top Bottom