ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 19,565
- 44,756
Nimeona katika data za bank ya dunia kwenye Google kwamba GDP ya Tanzania kwa 2020 Ni dollar 62.41 billion..sikuzingatia Sana shuleni mambo ya accountant na finance au pengine nimesahau maana kiukweli sijui GDP Inatafutwaje ila swali langu la msingi kabisa Ni nataka kujua Kama GDP ndio jumla ya fedha ambayo Kama taifa tunayo yaani mikoa yote ukijumlisha pesa ambayo iko bank,hazina na kwa wananchi wote.Na je ile fedha ambayo husomwa Kama BAJETI ya serikali kwa mwaka husika ni Kama ASILIMIA ngapi ya fedha yote nchini.yaani nataka kujua wanaposema kwa mwaka BAJETI itakuwa trillion 36 je hio ndio fedha ambayo Ni jumla kuu ya hela zote zilizo mifukoni kwetu na zilizo kwenye mifumo yao??na swali langu la mwisho Ni je wanawezaje kujua net amount ya fedha tulizonazo wakati kuna hela zinapotelea let's say kuungua moto hazitakuja kuwepo Tena kwenye mzunguko japo wao watajua Bado zipo mifukoni mwetu.