Gazeti la "The Citizen" ni tatizo

Gazeti la "The Citizen" ni tatizo

Katika Hilo Neno " Pumba " Mimi Naongeza Neno " Vu " Je Ukiyaunganisha Yote Linakuwa Neno Gani? Ukipata Jibu Lake Basi Ndiyo Ulivyo Wewe.
Ndiyo hulka yako kuandika ujinga huu sasa ulichokuwa unabisha nini? tayari umejirudi kwenye hali yako ya kawaida. Alafu wewe ndiwe unaona Credibility za watu wengine.
 
Duh, aise, wewe una msimamo mkali.Yaani serikali imekanusha lakini wewe unaendelea kukomaa!!??
serikali hii ongo ongo?! muhongo na kikwete walisema pale nyakato mwanza kipindi wanazindua mitambo ya umeme kwamba 'mgao wa umeme mwanza sasa ni historia' hapohapo umeme ukakata na hadi sasa miaka mitatu mgao bado upo
 
Ndiyo hulka yako kuandika ujinga huu sasa ulichokuwa unabisha nini? tayari umejirudi kwenye hali yako ya kawaida. Alafu wewe ndiwe unaona Credibility za watu wengine.

Nilikuambia Uyaunganishe Hayo Maneno Na Unipe Jibu Je Assignment Yako Umeshaimaliza? Haya Jibu Lake Ni Nini? Nataka Jawabu Tu Na Siyo Maneno Mengi.
 
Hili nalo linatakiwa lifungiwe kwani halina maana yoyote. Sisi tunalo gazeti la Mwananchi. Hilo The Citizen libaki Kenya huko huko
Mwananchi na The Citizen ni identical twins. Ukimfukuza The Citizen, Mwananchi atakuwa anafanya tale pacha wake angelifanya. Solution ni wote kuwaweka under watching brief na yule atakaye tenda sivyo achukuliwe hatua za kisheria na mwingine atalielewa somo kutoka kwa pacha wake. Both papers are anti establishment
 
Mtu

mtu kutukana na kutoa fix katika hoja nyingine hakubadilishi ukweli wa hoja yake au uzito wa hiyo kama hiyo hoja yake mpya kama ni ya ukweli na ina mantiki.
MIMI NAMAANISHA MTU ANAYEJALI KUHUSU CREDIBILITY HAWEZI KUA ANADANGANYA NA KUTUKANA, MAANA ZINASHUSHA CREDIBILITY..GOT IT?
 
MIMI NAMAANISHA MTU ANAYEJALI KUHUSU CREDIBILITY HAWEZI KUA ANADANGANYA NA KUTUKANA, MAANA ZINASHUSHA CREDIBILITY..GOT IT?
Binadamu simwamba kusema hausogei au haubadiliki na kukua, inawezekana kukua kumeanza, hata hivyo huwezi kudharau hoja yake inayozungumzia credibility kwa vile tu yeye hana credibility, katika dunia ya nonsense arguement hiyo inaitwa irrelevance appeal katika kundi la argumentum ad hominem, jaman arguement nayo pia ni art, tujiongeze
 
Mhh nina doubt kidogo

Hao mawaziri wawili wametajwa katika gazeti. Hakuna aliyelifikisha gazeti hilo popote pale
Walichofanya ni kukanusha

Katika mazingira ya kawaida, mawaziri ambao ni viongozi wa serikali walitakiwa wachukue hatua kali endapo wamesingiziwa, hawakufanya hivyo. Hii maana yake ni nini?
 
Investigative Journalists hawapo Tanzania? Nani kasema? Kubenea yupo....Mbwambo yupo...
 
..serikali imejaribu kukanusha na kujitetea, lakini muda ukifika, mbivu na mbichi zitajulikana (..time will tell).
 
Hivi karibuni hili gazeti limekuwa na Tabia ya kutunga habari sijui kwa maslahi ya nani.

mtakumbuka wiki iliyopita iliandika habari na ikidai kumnukuu waziri wa nishati na madini mh.Sospeter Muhongo kuwa serikali ina mpango wa kuuza hisa zake kwa 49%, Mara serikali ikakanusha habari hizo tena ikaenda mbali zaidi kwa kukana hata waziri kuzungumza na mwandishi yeyote wa gazeti hilo.

Kama hiyo haitoshi juzi tena wamekuja na habari ya serikali eti imesitisha ujenzi wa bandari mpya ya bagamoyo lakini muda si mrefu nimemuona waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano mh.Makame Mbarawa kwenye taarifa ya habari ya TBC1 akikanusha habari hiyo ya gazeti la citizen.

na kueleza kuwa mchakato unaendelea kama kawaida ikiwa ni pamoja na ulipaji fidia kwa watakaopisha mradi huo pia wataalam wetu na wa nchi tunazoshirikiana nazo katika mradi huo kutoka nchi za China na Oman wanaendelea na kazi ili kufanikisha ujenzi huo,sasa sijui hili gazeti lina mkakati gani juu ya nchi yetu.

Natoa wito kwa serikali kulifuatilia ikiwezekana walifutilie mbali maana naona wana lao jambo.

1. Nadhani ungewasaidia wachangiaji kama ungeonyesha a) jinsi gazeti lilivyotunga hiyo habari na b) habari yenyewe sahihi ilikuwaje.
2. Habari ikitoka kwenye gazeti na kukanushwa siyo ushahidi kuwa siyo sahihi. Kwani ni mara ngapi habari au taarifa zinakanushwa wakati ni za kweli? Kama kukanushwa kwa habari ndiyo ungekuwa ushahidi kuwa habari hiyo siyo sahihi basi kesi zote mahakamani zingefungwa baada ya mtuhumiwa kukana kuhusika na kesi.
3. Kama The Citizen wangeandika habari ambayo si sahihi, wangekanusha kesho yake (front page) na kuwaomba radhi wasomaji.
4. Kuhusu habari ya bandari, The Citizen iliandika: 'The govt halts Bagamoyo port' na ndani ya habari wakaendelea kusema project yenyewe is "halted not shelved". Sijui kama habari hii ilpokanushwa ilikanushwa kwa lipi: a) kwamba it's not halted, but it's shelved? b) au kwamba it's neither shelved nor halted, but construction is in progress even now/yesterday/today?
5. Natoa wito kwa wanaoleta mada kujaribu kuwa fair na si kukimbilia kutoa "blanket/wholesale judgement" hata kwa kitu ambacho hakijaelezwa kilihusu nini.
 
MWANANCHI na THE CITIZEN ni magazeti ya Kenya. Na ufahamu kuwa yapo hapa kwa maslahi, ni magazeti yanayomilikiwa na AGA KHAN na ni magazeti dada ya DAILY NATION la KENYA. Magazeti haya yatafanya juu chini kuiangamiza TANZANIA kwa kisingizio cha demokrasia. Hata registration ya MWANANCHI na the CITIZEN ina matatizo makubwa. Wakati yanaanzishwa wakenya wengi walikuja na kupora ajira wakafukuzwa viongozi waandamizi. Ulikuwa mwanzoni mwa uongozi wa JK. Magazeti haya ni jipu na ambalo kutumbuliwa kwake kutaleta mtikisiko. Mtakumbuka the EAST AFRICAN lilifungiwa hapa kwa kuandika uzushi na nadhani lipo kwenye mtandao tu. Ni kweli MWANANCHI na the CITIZEN yameajiri watanzania wengi lakini sera yake kwa kisingizio cha uhuru wa vyombo vya habari ndiyo tatizo.

Kwani hoja hapa ni nini ni magazeti ya Kenya au kuandika habari ambazo si za kweli ingawa hata mleta mada hajatuonyesha hizo za kweli zilikuwa zinasomekaje? Kwa nini unakimbilia kusema ni magazeti ya Kenya? Kwani hayo ambayo ni ya Tanzania huwa hayawezi kuandika kitu serikali ikakanusha? NI aina gani ya reasoning hii jamani? Inabidi tuanzishe tena vipindi vya debate shuleni na kwenye mitandao!
 
Haya kachukue tiketi yako kwa safari ya mapumziko mombasa
Siyo kusema hivi. Lengo ni kueleweshana ili wote kwa pamoja tujue ukweli ni upi. Lakini ukijibu hivyo ina maana hatuwezi kujua ukweli wa jambo.
 
Siyo kusema hivi. Lengo ni kueleweshana ili wote kwa pamoja tujue ukweli ni upi. Lakini ukijibu hivyo ina maana hatuwezi kujua ukweli wa jambo.

Majibu yake yanadhiirisha jinsi ustaarabu wake ulivyo mkuu.wala hata usibishane naye.
 
Kwani ujenzi was bandari ya bagamoyo unafaida gani kwa taifa? Wakati bandari ya mtwara IPO tu inaoza oza
 
Mhh nina doubt kidogo

Hao mawaziri wawili wametajwa katika gazeti. Hakuna aliyelifikisha gazeti hilo popote pale
Walichofanya ni kukanusha

Katika mazingira ya kawaida, mawaziri ambao ni viongozi wa serikali walitakiwa wachukue hatua kali endapo wamesingiziwa, hawakufanya hivyo. Hii maana yake ni nini?
Hizo habari hazikuandikwa na The Citizen directly Ila zimekuwa quoted from The East African. Hata Bloomberg waliquote hiyo habari ya Tanesco kufloat shares zao.
Magazeti sometimes hutumia habari kutoka chombo kingine, wakenya wanachezaga sana tricks hizi kwa ku quote magazeti yaliyofungiwa au off shoot journals kuepuka litigation na kusambaza propaganda. Haya magazeti yapo connected na vyombo vya usalama vya Kenya.
They are very lucky and hence effective kwa sababu watanzania tu wavivu wa kusoma na Hata tukiwa na moyo wa kusoma huwa hatujui kusoma.
Hint: The most important part ukisoma gazeti ni mleta habari na quotations....
 
Kuna habari leo twitter walimwandika Maalim seif ni rais wa zanzibar, watu walipopiga kelele wakaifuta na kujifanya wanaomba radhi. Kuna tatizo na hili gazeti.
 
Hizo habari hazikuandikwa na The Citizen directly Ila zimekuwa quoted from The East African. Hata Bloomberg waliquote hiyo habari ya Tanesco kufloat shares zao.
Magazeti sometimes hutumia habari kutoka chombo kingine, wakenya wanachezaga sana tricks hizi kwa ku quote magazeti yaliyofungiwa au off shoot journals kuepuka litigation na kusambaza propaganda. Haya magazeti yapo connected na vyombo vya usalama vya Kenya.
They are very lucky and hence effective kwa sababu watanzania tu wavivu wa kusoma na Hata tukiwa na moyo wa kusoma huwa hatujui kusoma.
Hint: The most important part ukisoma gazeti ni mleta habari na quotations....
Ni kweli maana walikuwa wanatumia gazeti la 'the economist' kuchafua Tanzania. Lakini pia lazima tuwe na mkakati maana ipo siku watachomeka habari itakayotuletea matatizo kwa faida yao
 
Back
Top Bottom