Gazeti la "The Citizen" ni tatizo

Hasira Zote Za Kulifungia Lile Gazeti Dada Lao La The East African Sasa Wamehamishia Ktk Gazeti La The Citizen.

Ni Gazeti Zuri Mno ILA Naona Kama Vile Kwa Sasa Lina UANDISHI WA KUKENGEUKA Hivi Wakati Najua WAANDISHI Wote Wazuri, Makini Na Ninaowaheshimu Wapo Huko.

Kwa Habari Ya KIZUSHI Kama Hii Inapoteza Kabisa CREDIBILITY Yao Na Wanahitaji Kubadilika Na Kuwa Makini Hasa Wakizingatia Kuwa Aliyepo Madarakani Sasa HANA MASIHARA Wala MCHEZO Bali HAPA KAZI TU.
 
Last edited by a moderator:
Hasira Zote Za Kulifungia Lile Gazeti Dada Lao La The East African Sasa Wamehamishia Ktk Gazeti La The Citizen. Ni Gazeti Zuri Mno ILA Naona Kama Vile Kwa Sasa Lina UANDISHI WA KUKENGEUKA Hivi Wakati Najua WAANDISHI Wote Wazuri, Makini Na Ninaowaheshimu Wapo Huko. Kwa Habari Ya KIZUSHI Kama Hii Inapoteza Kabisa CREDIBILITY Yao Na Wanahitaji Kubadilika Na Kuwa Makini Hasa Wakizingatia Kuwa Aliyepo Madarakani Sasa HANA MASIHARA Wala MCHEZO Bali HAPA KAZI TU.
what do you know about credibility? mtu unayetukana na kutoa fix sana hapa jf
 
what do you know about credibility? mtu unayetukana na kutoa fix sana hapa jf

Thibitisha Kwanza Tena Kimaandishi Hayo Matusi Yangu Na Hizo Fix Zangu Kisha Ndipo Nikujibu Maana Ya Hilo Neno Uliloniuliza. Nasubiri!
 
Hili nalo linatakiwa lifungiwe kwani halina maana yoyote. Sisi tunalo gazeti la Mwananchi. Hilo The Citizen libaki Kenya huko huko
 
Hili nalo linatakiwa lifungiwe kwani halina maana yoyote. Sisi tunalo gazeti la Mwananchi. Hilo The Citizen libaki Kenya huko huko

Mwananchi na The Citizen yanamilikiwa na kampuni ya Nation Media Group ya Kenya. Kampuni hiyo kwa kiasi kikubwa inamilikiwa na Agha Khan
 
Hivi karibuni hili gazeti limekuwa na Tabia ya kutunga habari sijui kwa maslahi ya nani.

mtakumbuka wiki iliyopita iliandika habari na ikidai kumnukuu waziri wa nishati na madini mh.Sospeter Muhongo kuwa serikali ina mpango wa kuuza hisa zake kwa 49%, Mara serikali ikakanusha habari hizo tena ikaenda mbali zaidi kwa kukana hata waziri kuzungumza na mwandishi yeyote wa gazeti hilo.

Kama hiyo haitoshi juzi tena wamekuja na habari ya serikali eti imesitisha ujenzi wa bandari mpya ya bagamoyo lakini muda si mrefu nimemuona waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano mh.Makame Mbarawa kwenye taarifa ya habari ya TBC1 akikanusha habari hiyo ya gazeti la citizen.

na kueleza kuwa mchakato unaendelea kama kawaida ikiwa ni pamoja na ulipaji fidia kwa watakaopisha mradi huo pia wataalam wetu na wa nchi tunazoshirikiana nazo katika mradi huo kutoka nchi za China na Oman wanaendelea na kazi ili kufanikisha ujenzi huo,sasa sijui hili gazeti lina mkakati gani juu ya nchi yetu.

Natoa wito kwa serikali kulifuatilia ikiwezekana walifutilie mbali maana naona wana lao jambo.


MWANANCHI na THE CITIZEN ni magazeti ya Kenya. Na ufahamu kuwa yapo hapa kwa maslahi, ni magazeti yanayomilikiwa na AGA KHAN na ni magazeti dada ya DAILY NATION la KENYA. Magazeti haya yatafanya juu chini kuiangamiza TANZANIA kwa kisingizio cha demokrasia. Hata registration ya MWANANCHI na the CITIZEN ina matatizo makubwa. Wakati yanaanzishwa wakenya wengi walikuja na kupora ajira wakafukuzwa viongozi waandamizi. Ulikuwa mwanzoni mwa uongozi wa JK. Magazeti haya ni jipu na ambalo kutumbuliwa kwake kutaleta mtikisiko. Mtakumbuka the EAST AFRICAN lilifungiwa hapa kwa kuandika uzushi na nadhani lipo kwenye mtandao tu. Ni kweli MWANANCHI na the CITIZEN yameajiri watanzania wengi lakini sera yake kwa kisingizio cha uhuru wa vyombo vya habari ndiyo tatizo.
 
Mnataka lifungiwe kwa kuandika ukweli??
Mmesahau kuwa ndio gazeti lililo ibua madudu ya ESCROW??.. Acheni kutumika nyie vijana wa Lumumba.
 
Mnataka lifungiwe kwa kuandika ukweli??
Mmesahau kuwa ndio gazeti lililo ibua madudu ya ESCROW??.. Acheni kutumika nyie vijana wa Lumumba.

ESCROW haikuibuliwa na gazeti lolote hapa nchini. Na for your information hakuna kashfa yoyote hapa nchini iwe ni EPA, Twin towers za BOT, na kadhalika iliyowahi kuibuliwa na gazeti. Tanzania hakuna waandishi wa habari makini wanaoweza kufanya investigative stories. Wanachofanya ni kuandika kile ambaqcho kimezungumzwa iwe ni bungeni, mahakamani au kiongozi mmoja kwa taasisi kutoa leak kwa sababu zake. Waandishi wa habari wengi hapa nchini wamenunuliwa na wako kwenye payroll ya wafanyabiashara na viongozi wa kisiasa.
 
Editor aitwe apewe onyo kali kwanza, kama Serikali haitaridhika na mienendo ya magazeti haya kutokana na kuendeleza agenda zao za siri kuhusu Taifa letu, basi wahamuriwe kufungasha virago vyao warudi makwao hatuitaji watu wafitini na wenye hila za kijinga.

Jana nilisema siajabu Wakenya hawa wametunga/ongeza chumvi kwenye habari yenyewe 4 some reasons - sio siri mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bwagamoyo unawatia wasiwasi/kiwewe washindani wetu hawa - watasema chochote under the sun kujaribu kutukatisha tamaa au ikiwezekana wawekezaji wasitishe mrandi mzima, hicho ndicho wanachotaka/omba kitokee!!!
 
Naomba iwe kweli The Citizen wamesema uongo manake ikiwa mtu ubongo wako hutaki kuwa influenced na hisia binafsi hakika huwezi kupinga mradi wa Bagamoyo!
 
Naomba iwe kweli The Citizen wamesema uongo manake ikiwa mtu ubongo wako hutaki kuwa influenced na hisia binafsi hakika huwezi kupinga mradi wa Bagamoyo!
 
Nitapiga marufuku kuletwa hapa ofisini ...limegeuka gazeti la udaku sasa ...
 
Back
Top Bottom