Gazeti la Tanzania Daima hatarini kufungiwa...!

Gazeti la Tanzania Daima hatarini kufungiwa...!

Haliwezi kufungiwa kwa sababu kesho yake lilisahihisha habari hiyo kwa kuwaomba radhi, yapo makosa ambayo ni ya kawaida isipokuwa kwa kuwa linamilikiwa na CDM sababu ya kutishiwa kufungiwa ni hiyo. Tumeshuhudia sana magazeti yakiandika fulani amefariki dunia kumbe mzima kabisa. Nadhani tuangalie pia magazeti yale ambayo huwa kwa makusudi yanaacha kuchapa habari za msingi maana ni kutunyima haki ya kupata habari sisi wananchi.
 
Hii sasa naona ni kupoteza mwelekeo....... mbona toleo lililofuata liliowaomba radhi kwa mapungufu hayo? Mbona hata habari yenyewe haina athari zozote za uvunjifu wa amani ama uchonganishi? Ama ni utumwa na unafiki wa vyombo vyetu kutaka kuwafurahisha wakubwa? kuna mangapi hawafuatilii?
hivi wanajua leo hii ukipeleka kesi yako polisi iwe ya madai ama jinai unatafuta kufilisika? ukishapewa mpelelezi wa jalada lako ndo utagundua makachero wetu ni wababaishaji. Binafsi niliwahi kumshitaki mtu nikabakia kuombwa pesa kila siku na hakuna lililofanyika zaidi ya kuambiwa mlalamikaji mume wake ni profesa, mtu wa serikali na mtu wa usalama wa Taifa hatanimeamua kuachana nalo kwa mkondo wa kisheria ila lazima nitafanya kile ambacho nisingepnda kukifanya hata ikipita miaka 10. Polisi wanafedhehesha na kuudhi sana. Waache unafiki!
 
Kwani serikali inaogopa nini kinachotakiwa kufichwa?Hawajui hizi ni zama za ukweli na uwazi?Ukilifungia leo Tanzania Daima litaibuka Tanzania Daima mara mbili.Wawe tu wavumilivu.Wangeanza na Ustaadhi Ilunga kwanza ningewaona wa maana.
 
Bora leo umebalansi!

Au wewe leo umebalance? Siku zote Mkjj hana team anayoshabikia bali husimamia ukweli, na kwa hili hata mie nilishangaa sana Tanzania daima kuandika kitu ambacho hawakuwa na uhakika nao..aibu kwao na wanastahili kinachowapata
 
Lilian Mbowe anasakwa!! kwamba nyumbani kwa Freeman Mbowe hawapajui hawa nyoko? hiki chote ni kiwewe cha serikali kukabwa vilivyo na Chadema.

Tanzania ya leo hata ufungie magazeti mangapi bado huwezi kuzima nguvu ya mabadiliko, mimi nawashauri Polisi waelekeze nguvu zao kuwakamata magaidi wote wanaochoma makanisa na kuuwa watumishi wa Mungu na siyo hili ambalo wenyewe Tanzania Daima walishaomba radhi kupitia gazeti lao.
Mzee Mwanakijiji naomba unielimishe kidogo hapa kwenye hili Mkurugenzi Lilian Mbowe anahusika vipi? au naye ni Mhariri mtendaji? nadhani hawa hawajui kwamba Lilian Mbowe ni PHD holder.
 
Last edited by a moderator:
Sasa Tanzania Daima ina maana hawakuwa na mtu ambaye angeweza kuwaambia kilichotokea? Kweli wanaweza kuandika habari nzito kama hii bila uwepo wa ushahidi wa video?
Mzee Mwanakijiji,kwangu mie kiongozi aliyefunga safari toka Dar mpaka Geita na aliloenda kulizungumzia halikufanikiwa kwa vile aliozungumza nao hawakukubaliana na aliloongea zaidi ya miguno na mapingamizi hapa na pale ni sawa na kuwa alitimuliwa tuu.
Tatizo ni kuwa hatutaki kuelewa kuwa wale watu wa Geita kile walichofanya ni maana halisi ya kumtimua Waziri na IGP. Hiyo inaonekana kama lugha kali lakini ndio ukweli. Hata hivyo Tanzania Daima si WALIFUTA KAULI? Shida iko wapi hapo?
 
Kwa hali hii ya polisiccm kujishughulisha na magazeti makini na kuacha vyombo vya kigaidi kama radio imaan na magazeti ya Al nuur pamoja waraka unaosambazwa na UAMSHO tusitegemee kama hii nchi itakuwa salama ila siku mtakapo anza kupima huo u.s.e.n.g.e wa polisi kwa kuchinjwa ndio mtakapojua kumbe polisi mnapaswa kufanya kazi gani hapa tanzania mbwa wakubwa nyie
 
Angalien na muache kuleta UCHDM na userikal ndugu zangu ushabiki huu utatufikisha pabaya kama imefikia hatua tunatetea ujinga eti sababu umefanywa na CHDM....walichofanya ni mwendelezo wa propaganda chafu dhid ya serikal na wanapaswa kuchukuliwa hatua kwan walishapewa onyo kama wenzao HALISI tusitetea maovu please

Acha umbulula wewe yanayoandikwa na gazeti la Uhuru unayasomaga,hapa kuna tatizo ukiandika habari ya kuikosoa maslahi ya wakubwa wa nchi kazima rungu likushukie,yaana waandishi wanalazimishwa kuipamba serikali tu na si kuikosoa.Tatizo hili kwa serikali.
 
Kama Gazeti hili litafungiwa basi nitaamini kuwa huo ni mkakati mwingine wa kuua uhuru wa vyombo vya habari baada ya kufanikiwa kulifungiwa MWANAHALISI. Ikumbukwe kuwa katika siku za hivi karibuni JK alipokuwa Ethiopia alichanganya Gazeti hili na Gazeti la Mwanahalisi.
 
niliwahi kusema siku moja humu kuwa gazeti la tanzania daima ni gazeti la uchochezi na kuleta chuki kati ya serikali na wananchi... hakuna mazuri yanayofanywa na serikali ambayo yanaipendeza gazeti la tanzania daima... habari nyingi ni za kutunga na zakufitinisha tu. na nimewahii uliza humu je gazeti la tz daima ni la chama (chadema ) au la mwananchama( mbowe).... ukweli kwa sasa gazeti hili limezidi na kupitiliza mipaka ya uhuru wa vyombo vya habari.... kama unafuatilia kila siku na kusoma tz daima vichwa vingi vya habari na taarifa zake zinamaudhui ya uchochezi tu..wito kwa serikali hili gazeti litazwe upya tena kwa haraka na pia vyombo vingine vya habari ....
 
Afisa gani wa jeshi la polisi anaongea upuuzi kama huu??!!

“Nasikia mkurugenzi wenu ni Dk. Lilian Mbowe, naye tunamhitaji hapa kwa ajili ya mahojiano, hivyo tunaomba msaidie apatikane maana tunataka kupata taarifa zake kisha kupeleka kwa wakubwa kwa ajili ya hatua zaidi,” alisema Mbuta.
 
huko ni kuishiwa ccm, mtahangaika sana na mtafunga kila chombo kitakacho kuwa kinawaeleza ukweli wananchi. ila hakuna shida kwasababu watu wameshawajua, ujiandae vema 2015
 
Ungeuliza pia je kila kinachofanywa na CHADEMA ni kizuri,hawana makosa? Hawaandiki mabaya ya chama chao cdm hata.
 
Heri lifungiwe tanzania daima gazeti la udaku, nalo mnalitetea wakati siku ile tulisema kwamba ni majungu ya gazeti la chadema mkatoa macho kwa kuchangia kwamba wassira na mwema wamefukuzwa geita, kumbe ni uongo wenu mliouzoea naomba lifungiwe ili liwe fundisho kwa vigazeti kama mwanahalisi na vingine vinavyo andika majungu tanzania.
nafsi yako yenyewe inakusuta. ukweli kuuita majungu.
 
Heri lifungiwe tanzania daima gazeti la udaku, nalo mnalitetea wakati siku ile tulisema kwamba ni majungu ya gazeti la chadema mkatoa macho kwa kuchangia kwamba wassira na mwema wamefukuzwa geita, kumbe ni uongo wenu mliouzoea naomba lifungiwe ili liwe fundisho kwa vigazeti kama mwanahalisi na vingine vinavyo andika majungu tanzania.
inaonekana hata kwenye familia na ukoo wenu sio wema ninyi.
 
Sasa Tanzania Daima ina maana hawakuwa na mtu ambaye angeweza kuwaambia kilichotokea? Kweli wanaweza kuandika habari nzito kama hii bila uwepo wa ushahidi wa video?

Ukiomba radhi katika front page maana yake umekiri na ndio utaratibu wa vyombo vya utangazaji. yawezekana hawakuwa na ushahidi wa kilichotokea but habari ilikuwa sahihi!!
 
Back
Top Bottom