Gazeti la Tanzania Daima hatarini kufungiwa...!

Gazeti la Tanzania Daima hatarini kufungiwa...!

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
SAKATA la kuhojiwa kwa Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima Jumamosi, Charles Misango, pamoja na mwandishi, Josephat Isango, kwa madai ya kuandika habari ya uchochezi limechukua sura mpya, baada ya Jeshi la Polisi nchini kudai kuwa linamtafuta Mkurugenzi wa Kampuni ya Free Media Limited, Dk. Lilian Mbowe, kwa ajili ya mahojiano.

Mbali na Dk. Mbowe, polisi imetangaza kumsaka Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Ansbert Ngurumo, pamoja na uongozi wa Kampuni ya uchapaji ya Printech, iliyochapa gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi Februari 16.

Misango na Isango walikamatwa juzi asubuhi na kuhojiwa hadi saa moja jioni kabla ya kuachiwa kwa dhamana kutokana na habari iliyoandikwa na gazeti hili na kupewa kichwa cha habari; ‘IGP na Wassira watimuliwa Geita'.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi pamoja na Ikulu walikanusha tuhuma hizo siku hiyo hiyo, ambapo kufuatia uchunguzi mpya wa habari hiyo, Mhariri Misango aliwasiliana kwa njia ya simu na msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso, kumjulisha juu ya upungufu huo na siku iliyofuata, Jumapili Februari 17, gazeti hili lilisahihisha na kuwaomba radhi Waziri Stephen Wassira na IGP Said Mwema, baada ya kuridhika kuwa habari hiyo haikuwa sahihi na ilikuwa na makosa ya kitaaluma.

Kabla ya kuanza kuhojiwa, mwandishi Isango alikwenda kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake, ambapo maofisa wa polisi kutoka kitengo cha uchunguzi makao makuu kwa kushirikiana na wale wa kikosi maalumu (Task Force) wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, walichukua vitu mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia katika uchunguzi wao.

Hatua hiyo ya polisi imekuja huku kukiwa na taarifa kwamba kunafanyika juhudi kubwa za kutaka kulifungia gazeti hili, kwa madai ya kuandika habari zinazoichonganisha serikali na wananchi.

Mmoja wa maofisa wa Ikulu (jina linahifadhiwa) alisikika akimwambia mmoja wa maofisa wa Kampuni ya Free Media Ltd kwamba serikali haifurahishwi na uandishi wa habari wa gazeti hili, na akaapa kuwa lazima Rais Jakaya Kikwete alifungie kabla ya mwaka 2015, na ikiwa atashindwa basi yule ajaye atafanya hivyo.

Aidha, kuna habari kwamba Idara ya Habari (MAELEZO), nayo imeanza kuhoji mambo kadhaa yanayomhusu Dk. Mbowe, ikiwa ni pamoja na kutumia elimu yake ya udaktari wa binadamu kumiliki chombo cha habari.

Taarifa ya kusakwa kwa Dk. Mbowe ilitolewa jana wakati Misango na Isango wakiongozwa na mwandishi wa habari hizi walipofika jana makao makuu ya Jeshi la Polisi kama walivyotakiwa na ofisa wa juu ya jeshi hilo, Mbuta, aliyewataka kusaidia kufanikisha kupatikana kwa mkurugenzi wao kabla ya Ijumaa wiki hii.

"Nasikia mkurugenzi wenu ni Dk. Lilian Mbowe, naye tunamhitaji hapa kwa ajili ya mahojiano, hivyo tunaomba msaidie apatikane maana tunataka kupata taarifa zake kisha kupeleka kwa wakubwa kwa ajili ya hatua zaidi," alisema Mbuta.

Msemji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, alipoulizwa sababu za kumtafuta Dk. Mbowe, alisema hana taarifa, kwa kuwa tangu asubuhi ya jana alikuwa kwenye kikao, kisha katika msafara, na kuahidi kufuatilia baada ya kumalizika kwa shughuli hizo.

Matukio hayo yamezidi kuleta ‘sintofahamu' ya kile kilicholengwa na serikali dhidi ya gazeti hili, ambalo kwa sasa limetajwa kuwa kero kwa baadhi ya watendaji wa serikali. Kadhalika, gazeti hili limekuwa likichukuliwa kuwa mali ya chama kikuu cha upinzani, CHADEMA, ambacho kimegeuka kuwa mwiba dhidi ya serikali na CCM

Source: Tanzania Daima
 
Kama gazeti limeshaomba msamaha kwa kutoa habari isiyokuwa ya ukweli, kuna haja gani ya kutaka kutumia nguvu kubwa hivyo? Serikali na vyombo vyenu vya dola, mbona kuna mengi ya kufanya/kuchunguza zaidi ya Tanzania Daima.....!
 
Sina hakika double standards hizi zitaisha lini. Mara mbili au tatu hivi nimekutana na habari nzito za kichonganishi ndani ya gazeti la Uhuru.. Hili linafahamika wazi kuwa ni gazeti la Chama Cha Mapinduzi. Wao bila aibu wala hofu ya kufungiwa, wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kuwagombanisha wananchi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo wakikituhumu kwa matendo ya uvunjifu wa amani, udini, ukabila, ukanda, matumizi ya nguvu na mengine huku wakijua wazi kuwa huu ni uzushi mtupu. Lakini sijasikia pahala popote, kwa njia yoyote, kutoka kwa mtu yeyote japo hata wakipewa karipio. Jamani, tunapotaka uhuru wa habari, tukubali kwanza kuwa wawazi na wakweli. Vyombo vya habari vyote, bila kujali vinasimamiwa na nani visimamiwe vema ili kuleta usawa na ufanisi kwenye tasnia ya habari.
 
Heri lifungiwe tanzania daima gazeti la udaku, nalo mnalitetea wakati siku ile tulisema kwamba ni majungu ya gazeti la chadema mkatoa macho kwa kuchangia kwamba wassira na mwema wamefukuzwa geita, kumbe ni uongo wenu mliouzoea naomba lifungiwe ili liwe fundisho kwa vigazeti kama mwanahalisi na vingine vinavyo andika majungu tanzania.
 
Makosa katika uandishi wa habari ni jambo lisiloepukika. Hii ni kutokana na ukweli kuwa, kunapozuka burning issue, waandishi hupenda kupata taarifa kutoka kwenye chanzo. Inapotokea vyanzo hivi vinakuwa biased, uwezekano wa kuwepo asymmetric kwenye taarifa ni mdogo. Labda hili ndilo lililoanzsha utaratibu mzuri kuwa, mwandishi anapotoa taarifa isiyo sahihi, aikanushe kupitia chombo hichohicho haraka iwezekanavyo. TanzaniaDaima wamelifanya hilo., na wao si wa kwanza kufanya hilo.,nakumbuka vizuri limewahi kujitokeza kwenye The Guardian around last year.. Serikali ijifunze kuwa na uvumilivu hasa kwa wale wanaoikosoa kwa nia njema.., TanzaniaDaima inclusively..
 
Mkurugenzi wa Radio Imaan na ustadhi Hassan Ilunga watakamatwa lini?

Wanashindwa kutumia nguvu kubwa namna hii kumtafuta mtu anayehusika na mauaji ya Padri wao wamekomaa na gazeti la Tanzania Daima...

Hapa kuna harufu ya udini wa JK, huenda wanamtafuta Dk Lilian Mbowe kwa vile ni cheap target ya JK kuwadhalilisha watu wa dini nyingine. Kwanza polisi hawa ni vilaza hawaelewi kabisa kuwa Business is a separate entity from the owner
 
Heri lifungiwe tanzania daima gazeti la udaku, nalo mnalitetea wakati siku ile tulisema kwamba ni majungu ya gazeti la chadema mkatoa macho kwa kuchangia kwamba wassira na mwema wamefukuzwa geita, kumbe ni uongo wenu mliouzoea naomba lifungiwe ili liwe fundisho kwa vigazeti kama mwanahalisi na vingine vinavyo andika majungu tanzania.

Sikumbuki kama imewahi kutangazwa popote kuwa TanzaniaDaima ni mali ya CHADEMA, sikumbuki. Kulihusisha TanzaniaDaima na CHADEMA kunakuja kutokana na ukweli kuwa, chombo hiki kinaipinga serikali waziwazi, waandishi wake wengi wana itikadi za kipinzani (mf. Isango, Edson n.k), viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakipata nafasi ya kuandika makala (mf. Mnyija, Kabwe, Mkumbo n.k), pamoja na umiliki wake unaohusishwa moja kwa moja na Mwenyekiti wa CHADEMA.. HATA HIVYO, uzito na ukweli wa mambo yanayoandikwa na Tanzania Daima umewaonesha watanzania wengi njia.. Serikali ya CCM haijawahi kupinga popote jambo lolote lililochapishwa na TanzaniaDaima kabla ya hili la geita. Umiliki wa chombo si tatizo, kinachopaswa kupewa kipaumbele ni uzito na uhalisi wa yanayoandikwa.
 
Hawawezo kitu, Mwanahalisi yenyewe kwa sasa kuna Mbinyo wakutaka Lifunguliwe,
 
Sasa Tanzania Daima ina maana hawakuwa na mtu ambaye angeweza kuwaambia kilichotokea? Kweli wanaweza kuandika habari nzito kama hii bila uwepo wa ushahidi wa video?

Namfahamu vizuri Isango, sio mtu wa kukurupuka kiasi hicho. Naamini kilikwepo chanzo cha habari hii, labda kilikuwa si cha kuaminika kwa 100%.,lakini tayari gazeti limeomba radhi, na ndio utaratibu tulionao..
 
La kuomba radhi, tayari limefanyika, sasa ili sakata naona wanalikuza tu bila sababu

Namfahamu vizuri Isango, sio mtu wa kukurupuka kiasi hicho. Naamini kilikwepo chanzo cha habari hii, labda kilikuwa si cha kuaminika kwa 100%.,lakini tayari gazeti limeomba radhi, na ndio utaratibu tulionao..
 
Angalien na muache kuleta UCHDM na userikal ndugu zangu ushabiki huu utatufikisha pabaya kama imefikia hatua tunatetea ujinga eti sababu umefanywa na CHDM....walichofanya ni mwendelezo wa propaganda chafu dhid ya serikal na wanapaswa kuchukuliwa hatua kwan walishapewa onyo kama wenzao HALISI tusitetea maovu please
 
sielewi hawa wanafiki wa magharibi wanasubiri nini kuiweka tanzania kwenye list ya nchi zinazokandamiza demokrasia?au sababu wamepewa migodi?
 
Angalien na muache kuleta UCHDM na userikal ndugu zangu ushabiki huu utatufikisha pabaya kama imefikia hatua tunatetea ujinga eti sababu umefanywa na CHDM....walichofanya ni mwendelezo wa propaganda chafu dhid ya serikal na wanapaswa kuchukuliwa hatua kwan walishapewa onyo kama wenzao HALISI tusitetea maovu please

toa vituko vyako
 
Hatimaye tulokuwa tunayasema yametimia, TANZANIA DAIMA haliko makini na kwa kukiri wamejipambanua.leo humu inaonekana ni kawaida ila jambo hili lingefanywa na gazeti lingine mashabiki humu wangetoa kila aina ya matusi ila kwakuwa gazeti lenu basi mnapaka rangi uwongo uonekane kawaida.shame on them
 
Back
Top Bottom