Gazeti la Raia Mwema lafungiwa kwa siku 90. Wadaiwa kumlisha Rais Magufuli maneno

Magufuli chapa kazi tuko pamoja wakizingua na wewe wazingue....waache kuokoteza maneno ya mitaani!
 
Hiyo ya pili ndo nimeisikia leo mi ya "wako wapi watu wako, wapumbavu wote" hii waniite na ushahidi.
 
Ila kwa nini nao hao watunge hizo nukuu?

Huo ni uzushi na si vizuri hata kidogo.

Wahariri wa hilo gazeti hawana miiko kabisa.

Huwezi kumzushia mtu namna hiyo.
Tuambie nukuu gani iliyotungwa hapo ......
 
Nchi ya watu zaidi ya milioni 40 yenye kila aina ya shida zijulikanazo na Binadamu Dunia hii mnapoteza muda kujadili maneno ya Raisi wa nchi? Wewe ukifungua tu mlango wa nyumba yako unakumbana na kila aina ya matatizo yanayomkabili Mtanzania, unakuja kupoteza muda hapa kujadili maneno aliyotamka Raisi jukwaani?
Wewe unafanya nini hapa
 
Raia mwema,mwanzoni walivyokua wanaipamba siri kali ya awamu ya tano walihisi watakua salama.

Chahali aliwahi kulalamikia uongozi wa raia mwema kutomshirikisha jinsi walivyokua wakisumbuliwa na siri kali juu ya makala za chahali,lakini hawakua wakimwambia chahali.

Waandishi kumbukeni kua dikteta yoyote hua anataka kusifiwa wakati wote bila kujali nini kitachotokea.
 
Boss.. hapo ndio shida ilipo. Kuna kauli ambazo unaweza kuzipata na kuzithibithsa kuwa ni za Magufuli. Lakini ni sawa na yale ambayo Mugabe anadaiwa kusema. Kudai tu haitoshi, ni muhimu kuonesha kauli hiyo imetolewa wapi na lini na ikiwezekana kuweka clip. Kuna kauli ambazo alizitoa ambazo hakuna mtu anabisha kwani zinaweza kupatikana mahali popote (youtube kwa mfano).
Alitoa zote
 
Niseme mimi binafsi siwezi kumsikiliza Magufuli akiongea...
Hivyo sijawahi kumsikiliza akihutubia mwanzo mwisho
Lakini mara nyingi kwa nafasi yake ya Urais chochote anacho ongea
huwa kinasambaa sana hivyo ukifika mitaani unasikia Magufuli kasema hivi
au vile........

Sasa leo baada ya gazeti la Raiamwema kufungiwa kwa kusema Magufuli
kasema 'watakaofika mwezi wa saba ni wanaume kwelikweli;

na 'Suruali za zamani msizitupe mtazihitaji'

maneno ambayo hata mimi nilisikia na kuamini yalitamkwa na Magufuli

nimeshangaa...sana.....na sasa najiuliza zile kauli zingine nilizosikia katamka
ni kweli alisema au nazo 'anasingiziwa?

1. 'Sikuahidi tetemeko'

2. 'bora unipe mimi kuliko kumpa mwanafunzi mimba'

3. wastaafu wengine wanawashwawashwa

4. huwezi kusaliti na uka survive tu

Na kauli zingine nyingi tu za kushangaza.....hizi sio za Magufuli?

kuna mwenye clip zake atuwekee humu?

Hasa hizo mbili za kubaki mjini hadi mwezi wa saba na suruali za zamani....
sio wa Ku mchukulia serious mana magufuli anaongea tu bila kufikiria kuwa maneno yake yana impact gan kama kiongozi
 
Kauli za Magufuli kwake ni sawa lakini kauli hizohizo zikisemwa na mtu mwingine tofauti na yeye mtu huyo anaitwa mchochezi.
 
Licha ya kuijipendekeza na kukwepa mno kumuudhi Mtukufu..still wamefungiwa..
ha ha haaaa......
Aisee,hasa yule dilunga alie kua akiupigia chapuo udikteta kua ndo unaleta maendeleo.

Cc zama mpyaaa.mzeee slaa kimyaaa,huezi kumsikia akitoa maoni kwenye mambo kama haya.
 
Unatunga nukuu ya uongo, tena kwa mkuu wa nchi, then utegemee kubaki salama tu! kama huu ndo uhuru wa kutoa maoni bora ufutwe.
 
Back
Top Bottom