Gazeti la rai laondolewa sokoni leo

Habari zenu senior members!! This is my first post but I'm fascinated. Ni kweli kabisa wakuu kwamba jana raiamwema yalikuwa machache but these sabotages have been going on and on for sometym even RaiaMwema wenyewe walishapublish kuhusu hao saboteurs!!! mi mwenyewe jana nilipata MwanaHalisi peke yake na kwenye website ya RaiaMwema lilikuwa toleo lililopita. Anyway, leo nimelisoma kupitia kwenye wavuti yao and some of the hotNews are hereUnder

VITA YA UMEYA: Siri yafichuka

Paul Sarwatt, Arusha
Disemba 22, 2010

Ni kulinda fursa za miradi nyeti ya ulaji
Ni vita kali Arusha, Mbeya, Mwanza
NGUVU za ziada zinazotumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wakuu wa serikali kwa lengo la kung'ang'ania uongozi wa halmashauri za Mwanza, Arusha na Mbeya katika nafasi ya umeya, zinalenga kuficha ufisadi unaoweza kufichuka iwapo watachaguliwa mameya wapya wasioyumbishwa, Raia Mwema limeelezwa.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), halmashauri nyingi nchini zimekuwa na rekodi chafu za ubadhirifu katika kipindi cha kwanza cha utawala wa Rais Jakaya Kikwete, na hali hii inatajwa kuzua hofu kwa wahusika.
Kutokana na mazingira hayo inadaiwa kuwa katika baadhi ya halmashauri hizo, wakurugenzi wamelazimika kuingilia kati, baadhi yao wakitajwa kuwahi kushiriki kufanikisha miradi ya ufisadi ambayo sasa ipo hatarini kufichuliwa.
Kutokana na mazingira hayo, juhudi na mbinu mbalimbali zimekuwa zikifanywa hata zilizo kinyume cha taratibu, kuzuia uwezekano wa kuchaguliwa kwa mameya wapya wenye misimamo dhidi ya ufisadi.
Hata hivyo, gazeti hili limeelezwa kuwa katika baadhi ya maeneo wakurugenzi wamekuwa wakitishwa kwa kuambiwa kwamba wasipounga mkono mbinu za madiwani wa chama fulani, usalama wao kikazi utakuwa hatarini.
Imedhihirika kwamba katika maeneo hayo, baadhi ya viongozi wa CCM, na hasa madiwani wake wamekuwa wakipigana ' kufa na kupona' kubakisha meya ‘wao' huku lawama zikitanda kuwa wanabomoa hadhi ya chama hicho mbele ya jamii kwa kuthibitisha uroho wa kung'ang'ania madaraka.
Wakati lawama hizo zikitanda miongoni mwa wana-CCM kwenye halmashauri husika, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, ameliambia gazeti hili wiki hii kuwa makao makuu ya chama chake hayajatoa maelekezo yoyote kuhusu mbinu za kufikia uamuzi wa kumchagua meya.
"Sisi kazi yetu ilikuwa kuteua majina na kuyawasilisha TAMISEMI na tumefanya hivyo. Suala la uchaguzi umeharibika au umekwenda vizuri ni la mkurugenzi wa halmashauri, siyo la kwetu," alisema Makamba.
Kutoka jijini Mwanza, gazeti hili limethibitishiwa kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ndiye anayepaswa kuamua kama Jiji hilo lichague meya au yeye ateue tume ya kuliongoza kama ilivyopata kutokea jijini Dar es Salaam.
Habari zilizothibitishwa zinaeleza kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya madiwani wa halmashauri ya jiji hilo kushindwa kuchagua meya na naibu wake kutokana na kutokubaliana kulikojitokeza kuhusu taratibu za upigaji kura.
Wakati madiwani wa CHADEMA ambao ni wengi wakitaka kupiga kura wakiwa wameketi kama inavyotokea bungeni, madiwani wa CCM walitaka kupiga kura kwa foleni kuelekea kwenye sanduku au eneo la upigaji.
Kutokana na mvutano huo, kikao hicho cha uchaguzi kilivunjika, huku Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Wilson Kabwe, akiwa amekubaliana na utaratibu wa CCM. Madiwani wa CCM walikuwa wakiongozwa na aliyepata kuwa naibu meya na diwani wa muda mrefu wa kata ya Igogo, John Minja, kutetea msimamo wao, ambao ulipingwa na madiwani wa CHADEMA, wakiongozwa na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje.
CHADEMA walikuwa wakisisitiza kuwa hata bungeni wakati wa kuchagua spika na naibu wake na hata wakati wa kuthibitisha jina la Waziri Mkuu, wabunge walipiga kura wakiwa wamekaa na bado zikahesabiwa kuwa ni kura za siri na kwa hiyo, si lazima kufuata utaratibu wa CCM ndipo usiri wa kura uthibitishwe.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa malumbano juu ya utaratibu upi utumike katika kupiga kura yalitokana na kuwapo kwa hofu ya kuhujumiana, ikiaminika kuwa upande wa CHADEMA ulihofia kuwa iwapo zingepigwa kura za siri kwa utaratibu uliotangazwa na Mkurugenzi, CCM wangeweza kushinda ingawa wao, CHADEMA, ndio wengi.
Kwa upande mwingine, CCM nao walihofia zingepigwa kura kwa utaratibu uliotakiwa na CHADEMA basi ilikuwa ni dhahiri kuwa wangepoteza nafasi zote za meya na naibu wake kwani CHADEMA wangedhibitiana ili kuhakikisha kuwa kila diwani wao anapiga kura kwa mgombea wao.
CHADEMA ina jumla ya madiwani 15 pamoja na wabunge wawili hivyo kufanya idadi ya kura zao kuwa 17 wakati CCM ina madiwani 12 na mbunge mmoja wa Viti Maalum, Maria Hewa, hivyo kufanya kura zao kuwa 13.
CUF kina diwani mmoja na mbunge mmoja wa viti maalumu ambao walikubaliana kuungana na CCM dhidi ya CHADEMA, ili diwani wa CCM kata ya Mkolani, Stanslaus Mabula achaguliwe meya na diwani wa CUF kata ya Pamba, Bhiku Kotecha, awe naibu meya.
Hata hivyo, mkurugenzi wa jiji anatajwa kwamba ndiye aliyechangia kutofanyika kwa uchaguzi huo kutokana na kukosa msimamo. Inaelezwa kwamba mara ya kwanza alisisitiza utaratibu wa kwenda kupiga kura kwa diwani mmoja mmoja kwenye kisanduku lakini baada ya kubanwa na madiwani wa CHADEMA, akakubaliana kuwa wapige kura wakiwa wamekaa pale walipokuwa wamaketi. Lakini wakati kura zikikaribia kupigwa madiwani wa CCM walikuja juu kupinga utaratibu huo kwa madai kuwa sio wa siri, na kwa mara nyingine tena Kabwe akakubaliana nao .
Hata hivyo, haikujulikana ni kwa nini Kabwe hakutoa fursa kwa madiwani hao kuamua utaratibu wa kutumia hata angalau kwa ya kunyoosha mikono, lakini badala yake akahitimisha kuwa madiwani walikuwa wameshindwa kutimiza wajibu wao, na akaripoti hivyo kwa Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Akizungumza na Raia Mwema wiki hii Kabwe alisema kuwa tayari amepeleka barua kwa waziri mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na anatarajia kuwa baada ya madiwani kushindwa kuchagua meya na naibu wake pamoja na wenyeviti na wajumbe wa kamati za kudumu za halmashauri waziri ataunda tume kuongoza jiji la Mwanza.
Kutoka Arusha, inaripotiwa kwamba hali ni tete zaidi. Kilichotokea Ivory Coast kwa nafasi ya Rais, ndicho kilichotokea Arusha kati ya CHADEMA na CCM. Diwani wa CCM, Gaudance Lyimo alichaguliwa meya na diwani wa TLP, Michael Kivuyo, alichaguliwa naibu meya, lakini CHADEMA ikamtangaza diwani wake, Estomih Mallah, kuwa ndiye meya.
Hata hivyo, "uchaguzi" huo wa CCM na wa CHADEMA haujakidhi matakwa ya kikanuni, kwa maana ya ula kuwa ya upigaji kura unaowahusisha angalau theluthi mbili ya madiwani wote.
Kutoka Mbeya, inaripotiwa kwamba hali ni tete pia, ingawa huko meya na naibu wake wamekwisha kupatikana. Athanas Kapunga wa CCM ndiye aliyechaguliwa meya na Frank Mayemba, pia wa CCM, naibu meya.
Katika uchaguzi huo mbinu zinazodaiwa kukandamiza demokrasia zilitumika ili kuhakikisha CCM kinashinda, hasa baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa kuna madiwani 10 wa chama hicho walikuwa tayari kuungana kumchagua meya kutoka kambi ya CHADEMA.

you can read the details in attachments
 
Attachments

  • Utata wa UMeya.doc
    94 KB · Views: 165
Sina mchango apa maana aya majarida mawili sijawahi kuyasoma na sina mpango wa kuyasoma maishani! Hata kama Yesu Mwokozi atarudi kupitia vijarida ivi viwili basi mi ataniacha maana sitamjua kwani sisomi vijarida vya mafisadi.

Naona hueleweki!! Magazeti ya mafisadi unaliweka Raia Mwema?
 
Habari zenu senior members!! This is my first post but I'm fascinated. Ni kweli kabisa wakuu kwamba jana raiamwema yalikuwa machache but these sabotages have been going on and on for sometym even RaiaMwema wenyewe walishapublish kuhusu hao saboteurs!!! mi mwenyewe jana nilipata MwanaHalisi peke yake na kwenye website ya RaiaMwema lilikuwa toleo lililopita. Anyway, leo nimelisoma kupitia kwenye wavuti yao and some of the hotNews are hereUnder

VITA YA UMEYA: Siri yafichuka

Paul Sarwatt, Arusha
Disemba 22, 2010

Ni kulinda fursa za miradi nyeti ya ulaji
Ni vita kali Arusha, Mbeya, Mwanza
NGUVU za ziada zinazotumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wakuu wa serikali kwa lengo la kung’ang’ania uongozi wa halmashauri za Mwanza, Arusha na Mbeya katika nafasi ya umeya, zinalenga kuficha ufisadi unaoweza kufichuka iwapo watachaguliwa mameya wapya wasioyumbishwa, Raia Mwema limeelezwa.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), halmashauri nyingi nchini zimekuwa na rekodi chafu za ubadhirifu katika kipindi cha kwanza cha utawala wa Rais Jakaya Kikwete, na hali hii inatajwa kuzua hofu kwa wahusika.
Kutokana na mazingira hayo inadaiwa kuwa katika baadhi ya halmashauri hizo, wakurugenzi wamelazimika kuingilia kati, baadhi yao wakitajwa kuwahi kushiriki kufanikisha miradi ya ufisadi ambayo sasa ipo hatarini kufichuliwa.
Kutokana na mazingira hayo, juhudi na mbinu mbalimbali zimekuwa zikifanywa hata zilizo kinyume cha taratibu, kuzuia uwezekano wa kuchaguliwa kwa mameya wapya wenye misimamo dhidi ya ufisadi.
Hata hivyo, gazeti hili limeelezwa kuwa katika baadhi ya maeneo wakurugenzi wamekuwa wakitishwa kwa kuambiwa kwamba wasipounga mkono mbinu za madiwani wa chama fulani, usalama wao kikazi utakuwa hatarini.
Imedhihirika kwamba katika maeneo hayo, baadhi ya viongozi wa CCM, na hasa madiwani wake wamekuwa wakipigana ‘ kufa na kupona’ kubakisha meya ‘wao’ huku lawama zikitanda kuwa wanabomoa hadhi ya chama hicho mbele ya jamii kwa kuthibitisha uroho wa kung’ang’ania madaraka.
Wakati lawama hizo zikitanda miongoni mwa wana-CCM kwenye halmashauri husika, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, ameliambia gazeti hili wiki hii kuwa makao makuu ya chama chake hayajatoa maelekezo yoyote kuhusu mbinu za kufikia uamuzi wa kumchagua meya.
“Sisi kazi yetu ilikuwa kuteua majina na kuyawasilisha TAMISEMI na tumefanya hivyo. Suala la uchaguzi umeharibika au umekwenda vizuri ni la mkurugenzi wa halmashauri, siyo la kwetu,” alisema Makamba.
Kutoka jijini Mwanza, gazeti hili limethibitishiwa kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ndiye anayepaswa kuamua kama Jiji hilo lichague meya au yeye ateue tume ya kuliongoza kama ilivyopata kutokea jijini Dar es Salaam.
Habari zilizothibitishwa zinaeleza kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya madiwani wa halmashauri ya jiji hilo kushindwa kuchagua meya na naibu wake kutokana na kutokubaliana kulikojitokeza kuhusu taratibu za upigaji kura.
Wakati madiwani wa CHADEMA ambao ni wengi wakitaka kupiga kura wakiwa wameketi kama inavyotokea bungeni, madiwani wa CCM walitaka kupiga kura kwa foleni kuelekea kwenye sanduku au eneo la upigaji.
Kutokana na mvutano huo, kikao hicho cha uchaguzi kilivunjika, huku Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Wilson Kabwe, akiwa amekubaliana na utaratibu wa CCM. Madiwani wa CCM walikuwa wakiongozwa na aliyepata kuwa naibu meya na diwani wa muda mrefu wa kata ya Igogo, John Minja, kutetea msimamo wao, ambao ulipingwa na madiwani wa CHADEMA, wakiongozwa na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje.
CHADEMA walikuwa wakisisitiza kuwa hata bungeni wakati wa kuchagua spika na naibu wake na hata wakati wa kuthibitisha jina la Waziri Mkuu, wabunge walipiga kura wakiwa wamekaa na bado zikahesabiwa kuwa ni kura za siri na kwa hiyo, si lazima kufuata utaratibu wa CCM ndipo usiri wa kura uthibitishwe.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa malumbano juu ya utaratibu upi utumike katika kupiga kura yalitokana na kuwapo kwa hofu ya kuhujumiana, ikiaminika kuwa upande wa CHADEMA ulihofia kuwa iwapo zingepigwa kura za siri kwa utaratibu uliotangazwa na Mkurugenzi, CCM wangeweza kushinda ingawa wao, CHADEMA, ndio wengi.
Kwa upande mwingine, CCM nao walihofia zingepigwa kura kwa utaratibu uliotakiwa na CHADEMA basi ilikuwa ni dhahiri kuwa wangepoteza nafasi zote za meya na naibu wake kwani CHADEMA wangedhibitiana ili kuhakikisha kuwa kila diwani wao anapiga kura kwa mgombea wao.
CHADEMA ina jumla ya madiwani 15 pamoja na wabunge wawili hivyo kufanya idadi ya kura zao kuwa 17 wakati CCM ina madiwani 12 na mbunge mmoja wa Viti Maalum, Maria Hewa, hivyo kufanya kura zao kuwa 13.
CUF kina diwani mmoja na mbunge mmoja wa viti maalumu ambao walikubaliana kuungana na CCM dhidi ya CHADEMA, ili diwani wa CCM kata ya Mkolani, Stanslaus Mabula achaguliwe meya na diwani wa CUF kata ya Pamba, Bhiku Kotecha, awe naibu meya.
Hata hivyo, mkurugenzi wa jiji anatajwa kwamba ndiye aliyechangia kutofanyika kwa uchaguzi huo kutokana na kukosa msimamo. Inaelezwa kwamba mara ya kwanza alisisitiza utaratibu wa kwenda kupiga kura kwa diwani mmoja mmoja kwenye kisanduku lakini baada ya kubanwa na madiwani wa CHADEMA, akakubaliana kuwa wapige kura wakiwa wamekaa pale walipokuwa wamaketi. Lakini wakati kura zikikaribia kupigwa madiwani wa CCM walikuja juu kupinga utaratibu huo kwa madai kuwa sio wa siri, na kwa mara nyingine tena Kabwe akakubaliana nao .
Hata hivyo, haikujulikana ni kwa nini Kabwe hakutoa fursa kwa madiwani hao kuamua utaratibu wa kutumia hata angalau kwa ya kunyoosha mikono, lakini badala yake akahitimisha kuwa madiwani walikuwa wameshindwa kutimiza wajibu wao, na akaripoti hivyo kwa Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Akizungumza na Raia Mwema wiki hii Kabwe alisema kuwa tayari amepeleka barua kwa waziri mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na anatarajia kuwa baada ya madiwani kushindwa kuchagua meya na naibu wake pamoja na wenyeviti na wajumbe wa kamati za kudumu za halmashauri waziri ataunda tume kuongoza jiji la Mwanza.
Kutoka Arusha, inaripotiwa kwamba hali ni tete zaidi. Kilichotokea Ivory Coast kwa nafasi ya Rais, ndicho kilichotokea Arusha kati ya CHADEMA na CCM. Diwani wa CCM, Gaudance Lyimo alichaguliwa meya na diwani wa TLP, Michael Kivuyo, alichaguliwa naibu meya, lakini CHADEMA ikamtangaza diwani wake, Estomih Mallah, kuwa ndiye meya.
Hata hivyo, “uchaguzi” huo wa CCM na wa CHADEMA haujakidhi matakwa ya kikanuni, kwa maana ya ula kuwa ya upigaji kura unaowahusisha angalau theluthi mbili ya madiwani wote.
Kutoka Mbeya, inaripotiwa kwamba hali ni tete pia, ingawa huko meya na naibu wake wamekwisha kupatikana. Athanas Kapunga wa CCM ndiye aliyechaguliwa meya na Frank Mayemba, pia wa CCM, naibu meya.
Katika uchaguzi huo mbinu zinazodaiwa kukandamiza demokrasia zilitumika ili kuhakikisha CCM kinashinda, hasa baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa kuna madiwani 10 wa chama hicho walikuwa tayari kuungana kumchagua meya kutoka kambi ya CHADEMA.

you can read the details in attachments
 
Gazeti la kifisadi nalo linafanyiwa hujuma!!

Sio hujuma ni kwamba story zilizotoka na makala wenye gazeti hawajazipenda na wanaoziondoa sokoni ni wao si HUJUMA, naona waandishi wao wameamua kupiga kazi na kwenda kinyume na wakubwa zao, na wameshasema liwalo na liwe. Tusubiri tuone, maana isije ikawa hao wenyewe wanafanya danganya toto ili wakianza kumshughulikia JK waseme wameamua kuacha waandishi wafanye kazi
 
Rai lipo nimeliona kituo cha mabasi Mwenge,sababu silisomi toke RA alinunue sikuweza kufahamu kuwa lina jambo lolote la maana la kunifanya nilinunue
 
Ukweli ni kwamba gazeti la Rai kweli limekusanywa japo wamecheleweshwa sana baadhi ya maeneo limeshasambazwa.

Utata ni kwamba hata Raia Mwema jana lilikua chache sana kiasi likaisha sokoni, hata sasa baadhi ya maeneo halipo.

Wanangu UMEME inaweza ikawa tatizo maana siku hizi umeme ni wa kudunduiza!
 
Gazeti la Rai limekusanywa leo na halipatikani kabisa. Taarifa tulizonazo zinaeleza kuwa lilikuwa na habari inayoonyesha kuwa Beno Malissa na Ridhwan Kikwete wanaandaa mapinduzi ya kumng'oa Katibu wa UVCCM Martine Shigella. Taarifa za ndani kutoka Habari Cooperation zinaeleza kuwa habari hiyo iliwanukuu wenyeviti 17 wa UVCCM mikoa ambao walikuwa wakipingana na harakati hizo. Tena inaelezwa kuwa Usalama wa Taifa wamepewa jukumu la kuhakikisha gazeti hilo haliingii mtaani. Wenye taarifa zaidi mnaweza kuendelea ikiwemo kutupa habari iliyosababisha gazeti kukusanywa.

Library ya UDSM lazima watakuwa nalo maana wako ki-CCM zaidi.

ukifika hapo lazima kukutana na Mtanzania, Uhuru na RAI.

hadi mkandala analo
 
Back
Top Bottom