Gazeti la Mwananchi kupanda bei

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Wadau wa JF.
Nimesoma gazeti la Mwananchi la leo Januari 31, wanawataarifu kuwa kuanzia Februari mosi bei itakuwa Sh800 kutoka Sh500.
 
Aaaaangrrr umenistua kweli??
Nimesoma fasta fasta nikajua ni jf.
Hata liuzwe 10000 gazeti letu teule,tukufu jf lipo na lidum milele
 
Nyokoo

Gazeti lenu na nani mkenya mkubwa we


Uchochezi tu.......[/COLOR][/COLOR]
 
wata linunua wao wenyewe!!hawaoni serkali imegoma kupandisha maslahi yetu madaktari!
 
Hata mimi nimeshangaa sana kwani mapato ya magazeti, duniani kote, sio bei ya gazeti bali matangazo ya biashara ndani ya magazeti, na Mwananchi kwa hili wapo juu sana compared na magazeti mengine. Vinginevyo, unaweza hata kulitoa gazeti bure, ili mradi uwe na circulation nzuri tu itakayokupa good ratings.
 
Kutoka shilingi 5oo mpaka 8oo du ni kali sijui tunaenda wapi ?

Hilo ni ongezeko la asilimia sitini (60%).

Sababu za ongezeko hili bila shaka zitakuwa ni hizi (wenyewe watathibitisha ama kukanusha):
1. Kupanda kwa posho na mishahara ya waandishi wao, wanaofanya kazi kubwa ya kwenda huku na kule kutafuta na kuripoti habari!
2. Kupanda kwa gharama za uendeshaji kufuatia ongezeko la bei ya umeme.
 
Tutakuwa tunasoma kwenye website sio lazima kubebana na makaratasi
 
Hata mimi nimeshangaa sana kwani mapato ya magazeti, duniani kote, sio bei ya gazeti bali matangazo ya biashara ndani ya magazeti, na Mwananchi kwa hili wapo juu sana compared na magazeti mengine. Vinginevyo, unaweza hata kulitoa gazeti bure, ili mradi uwe na circulation nzuri tu itakayokupa good ratings.

Mkuu wafanyabiashara wanafanya kila mbinu ku capitalize ktk huu ulegelege wa serikali ku maximise profit.

Kitu ambacho bado najiuliza, haya magazeti pamoja na majarida wao wanajipangia bei kadri wanavyotaka wao? hakuna chombo cha kiserikali cha kuwadhibiti? maana naona hii nchi bila kuweka regulatory authorities ktk kila bidhaa na huduma inakuwa ni vurugu badala ya biashara ama huduma.
 
Nacut down ununuzi wa gazeti hili toka mara 7 kwa wiki hadi tatu tu kwa wiki, j3, j5 na ijumaa baaasi
 
Karne gani hii mkuu?

Kiongozi nafahamu hii ni karne ya tekelinalokujia lakini usisahau kwamba mwananchi wanafanya biashara.

Sasa kama tukiamua kusoma kwenye mtandao na wao wakaona circulation imepungua, unadhani watafanyeje ili muendelee kusoma gazeti lao? si wanaweza kuamua kusitisha kutoa online edition, au wanaitoa ikiwa delayed!!
 
sukari ilipanda,mafuta, pantoni,umeme,sasa magazeti,subirini nauli za daladala sasa maana hao sumatra siku hizi wanamaarifa zaidi.mwananchi nao mafisadi na wanamatangazo mengi.wameona watu wanasoma sana.hakuna mwenye huruma kwenye hii nchi.
 
wamenipunguzia lundo la makaratasi nyumbani mwangu: kama nikitaka habari nitazifuata kwenye mtandao. hata hivyo ni mara chache sana kukuta habari mpya tofauti na zile zinazoongelewa mitaani.
 
Back
Top Bottom