Gazeti la Mtanzania kigeugeu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gazeti la Mtanzania kigeugeu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Inkoskaz, Feb 27, 2011.

 1. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Wadau nimesoma gazeti la mtanzania toleo la leo jumapili tarehe 27 february 2011 kuna makala isemayo siku za CCM zinahesabika,pia main headline inazungumzia anguko la pato la taifa kutokana umeme...je ni kuwa limejirudi kutoa habari zenye maslahi ya umma au ni janja ya nyani kutafutwa kuungwa mkono ili Dowans ipate mkataba mpya?
   
 2. m

  mshaurimkuu Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka; hawa jamaa (mafisadi) na mawakala wao wanatumia kila mbinu ku-capture minds za watu ili kupata support. Haikupata kuandikwa mahali fulani kwamba wakati mwingine hata shetani huja kwa mfano wa malaika wa nuru? Mwenye ufahamu na afahamu.
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Hata mimi kiukweli siwaamini naona wamekuja kimtego mtego tu
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa hulka yao mafisadi hawana rafiki wa kudumu, rafiki ni yule anayeweza kukidhi mahitaji yao katika wakati uliopo.(They dont have permanent friend but permanent interest); hivyo hawachelewi kumtosa rafiki wa zamani kama hana manufaa nao tena.
   
 5. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Gazeti lilikosa soko, mauzo yalipungua kwa kasi sasa wanataka kulirudisha sokoni kwa staili yake! Mi naona wamechelewa, Bashe kama ni Mkurugenzi wa Habari Corp. amechelewa sana. Wajanja hatulinunui ng'o!
   
 6. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Wamechelewa mno na walijichafua sana,hata kama watakuwa wanaandka ukweli imani kwa wananchi haipo tena
   
 7. T

  Teh Teh Teh Member

  #7
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtanzania belongs to Rostam Aziz. One of the leading Fisadi in Tanzania. He is not loyal to Tanzania, but royal to CCM. He knows that his interest can be defended by CCM only as rulling party.

  Dont be amazed.... ITS JUST A STRATEGIC ANGLE.

  JUST WAIT AND YOU WILL SEE.................
   
 8. s

  salisalum JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Hatuwezi kukubali kununua au kutumia tena mitambo ya dowans. Walie tu!
   
 9. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni propaganda ya kutaka mitambo ya Duwanizi inunuliwe.
   
 10. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  In reality katika kipindi cha miezi miwili Gazeti la Mtanzania limebadilika sana especialy baada ya kupata CEO Mpya Bashe na ni gazeti pekee la daily ambalo limekuwa likiripoti habari kwa usahii na wanafanya utafiti wa kutosha the case in point include Tukio la Gongo la mboto,Tatizo la umeme, mfumuko wa bei ,sometimes nafikiri ni vizuri tuwe tuna apreciate kazi zinazofanywa na wahariri wa Mtanzania, Tatizo mimi ninaloliona ni kwamba tunalihukumu gazeti hili kwa sababu linamilikiwa na Rostan badala ya kuangalia content wameandika nini ,That is unbiased ,Rostan kama Mtanzania ana haki ya kufanya Biashara kama Raia Wengine and so far Rostan ni owner na hausiki na masuala ya Editorial,Tusiwe ni watu wenye mawazo asi tu,tunatakiwa tubadilike penye pema tukubali ,Bashe na Team yako tunawatakia kila la kheri na nawaidi kuanzia sasa nitalinunua gazeti la Mtanzania,
   
 11. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Editor lipaishe ila limeisha. Mtanzani ni sawa na Uhuru
   
 12. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapana..usipoteze watu..kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya yafuatayo..1. Mmiliki wa chombo cha habari (media owner/proprietor). 2. nguvu na mielekeo ya kisiasa (political pressures) 3. Masuala ya kitasinia-Professional culture-ethics, codes 4. Teknolojia-technological possibilities and constaints 5. masuala ya kiutawala/uongozi ndani ya chumba cha habari eg vyanzo vya habari n.k-sources tactics and strategies, news management. Haya masuala matano hubeba sura fulani inayotambulisha chombo cha habari..haiwezi tokea tu usiku mmoja (overnight) eti mwelekeo na itikadi ya chombo fulani inabadilika ghafla..popote duniani katika ulimwengu wa habari haitokei..so ogopa 'kuingizwa chaka na usanii unaofanyika hapo Habari corporation kwa sasa!...ni mtazamo tu
   
 13. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
 14. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kuna mawili.
  1. Mkumbukeni Jenerali Twaha Ulimwengu aliwahi kuandika kwenye moja ya makala zake wakati wa kampeni kwamba....... 'Wakati wa kampeni, baadhi ya wanahabari huweka akili zao pembeni na kuanza kufanya mambo kama wanyama, uchaguzi ukiisha, hurejea kujivika akili zao za kawaida na kurudi kuwa binadamu"..... Nimesema hiyo kuwakumbusha kuwa sasa huenda wamerejesha akili zao za kawaida baada ya kuziweka pembeni kwa muda mreeefu sana, tatizo ni kurejesha imani ya watu tena sio kazi rahisi. nakumbuka moja ya makala za Deo Balile mwezi Novemba au desemba mwaka jana baada ya uchaguzi alimchambua JK na familia yake bila woga hadi nikajiuliza ni yule yule Balile Kibaraka wa CCM anayeitukana kila siku chadema au mwingine???? Hapo akili yake kidogooo ilikuwa inaanza kurejea kwenye uhalisia. Sina hakika kama anaendelea hivyo au la kwa sasa.
  2. Mtanzania Jumapili ni gazeti ambalo Mhariri wake walau ana akili, anaitwa KUrwa Nyerere Karedia. Mwanzoni alikuwa Tanzania Daima. Nimjuavyo huyu mtu ana akili ikilinganishwa na wahariri wengine wa gazeti hilo kwahiyo usishangae ukaona Mtanzania Jumapili limekwenda shule, lakini ikifika Jumatatu unakutana na mauzauza hadi ijumaa.
  Bashe anayo kazi kubwa kuamua, afanye biashara kwa kufuata maadili ya uandishi au amtumikie Kafiri na kulamba miguu ya RA na CCM
   
 15. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Hivi wewe unaongea nini? Kama Rostam hahusiki na editorial kwa nini kule nyuma gazeti lilisheheni upumbavu mwingi? Mbona gazeti la RAI ambalo mmiliki ni huyo huyo Rostam na CEO wake ni huyo huyo Bashe linaendelea kuandika upuuzi ambao hata mtoto aliye labour kule Muhimbili anajua kwamba ni upuuzi amabo ama umeandikwa naye Rostam au kwa amelekezo yake. Hicho mnachokisifia humu ni janja yao na ni baada ya kuona kwamba hasira na chuki za watanzania kwao ziko dhahiri kiasi cha kwamba hata hilo gazeti wamelipuuza na kuliona ni uchafu mtupu. Hiyo imewapa hofu kwamba rundo la magazeti yasiyoaminiwa likiongezeka basi ajenda yao ya uchaguzi 2015 watakosa kwa kuiuza maana watu wataona kwamba huo ni udaku tu. RAI ambalo huko nyuma lilikuwa linaoongoza kwa mauzo sasa hivi linachapa nakala 2500 tu wakati Mwanahalisi linapiga nakala 75,000 kwa wiki.

  Hawa jamaa ndiyo ambao juzi tu walikuwa wanapiga debe kwenye gazeti lao kwamba Dowans walipwe ili kuepuka fedheha kwa wawekezaji huko nje wakati wote tuanjua kwamba mmiliki wa hilo gazeti ndiye mwizi anayesubiri kujazwa mapesa yetu kwenye kaunta ya benki. Kama gazeti hili ni objective mbona bado linaendelea kuwatukana wale wote wanaowafikiria kwamba wanakwenda kinyume na matakwa na maslahi ya bosi wao kama vile Mwakyembe, Sitta, Membe na wengineo?

  Ndugu yangu, tumeshatangaza kwamba Rostam ni janga la Taifa na atabaki hivyo hata ukimpamba na kumtetea vipi? Nchi hii haikuwa na tatizo na Rostam kama mwekezaji na ndiyo maana kabla ya Kagoda, Richmond na sasa Dowans hakuna aliyemgusa yeye au kuzungumzia uwekezaji wake. Sasa kama wewe unadhani kwamba watanzania kupaza sauti dhidi ya maovu yake ni kumuonea basi mchukue ukanywe naye chai lakini sisi HATUMTAKI!
   
 16. T

  Tata JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Usishangae ndugu yangu hizo ndiyo habari zinazouza magazeti kwa sasa hivi. Upepo ukibadilika nao watabadilika ili waendelee kuuza magazeti yao.
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,138
  Trophy Points: 280
  kuna gazeti linaloandika upupu zaidi ya Tanzania Daima?
   
 18. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #18
  Feb 28, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145  Nashukuru umekiri kwamba mtanzania limebadilika ,kwa Rai sina coment, second issue hauwezi ukalinganisha (compare) Mwanahalisi na Mtanzania ,Mtanzania ni gazeti la daily (Kila siku) wakati Mwanahalisi ni gazeti la wiki(Weekly Newspaper),Msimamo wangu bado upo pale pale kwamba Mtanzania limedilika , kama kuna ajend behind haya maboresho I am not sure na hainihusu,kinachonihusu mimi kama consumer wa product ni ubora wa bidhaa, mision na vision havinihusu,Hata tukiangalia Heading ya ya leo ''Chadema washika kasi' ni kielelezo tosha kwamba Mtanzania wamebadilika
  Bashe usivunjike moyo endelea kuboresha gazeti sisi wasomaji tunakuhunga mkono na tupo pamoja ,kama siku zote tulivyounga mkono magazeti mengine serious like Mwanahalisi, Tanzania Daima, Mwananchi
   
 19. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  suala la Dowans litatupa jibu kama wamejirudi amani wapiga debe
   
 20. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  elezea huo upupu nje ya hapo utakuwa umekurupukia hoja.:a s 13:
   
Loading...