Gazeti la Jamhuri: Nyani walewale msitu tofauti

Ni gazeti zuri sana na wamelipa rangi safi sana kwa mbele. Nimeliona leo na watu wanaligombea sana kwa kweli. Kichwa cha habari kinasema ''LOWASSA AONGOZA KURA ZA MAONI''
 
kwa kweli tunakazi this regime tutashuhudia mengi, ombi langu kwa Mungu wetu ni kwamba kuliokoa taifa hili ccm ife kabisa kwa manufaa ya walalahoi wa nchi hii, naamini kabla mvi haziota kichwani mwangu Mungu wetu atakuwa ameshatujibu maombi haya.
 
Habari nilizozipata usiku huu ni kwamba gazeti mnalolisubiri kwa shauku kubwa liitwalo JAMHURI linalomilikiwa na EL nitaingia mtaani Jumanne hii. Anzeni kupata toleo la kwanza hadi mfikie hatua ya ku-judge kama linampigia debe kweli EL kwa 2015, linampigia debe kwa 2012 CCM chaimanship au kuna jingine nyuma ya pazia. Tahadhari: USINIULIZE SOURCE PLZ
Nani kakwambia tunalisubiri kwa shauku kubwa,wewe kama unatangaza ,tangaza tu hayo mambo ya kulazimishana huko huko
 
Ni gazeti zuri sana na wamelipa rangi safi sana kwa mbele. Nimeliona leo na watu wanaligombea sana kwa kweli. Kichwa cha habari kinasema ''LOWASSA AONGOZA KURA ZA MAONI''
Heh heh hizo kura za maoni zimefanyika wapi ,lini na chombo kipi cha utafiti.Kura za maoni ya kuwa raisi au kuwa fisadi hebu tuhabarilsheni huku Likurufusi bado halijafika hilo gazeti huenda tutapata baada ya wiki ,ngoja nibofye kwenye kasimu kangu sijui kama lipo online.Hizi mbio za Magogoni balaa ni kwa udi na uvumba,kuna dili gani huko
 
Kujiuliza kama litampigia debe au la ni kuuliza the obvious. Mmiliki ni yeye, wahariri au waandishi ni Manyerere jackton na Deodatus Ballile. Unategemea nini hapo?
Huyu Jacton mbona anauharibu na kuutia aibu ukoo wa Nyerere yaani kufundishwa kote na Nyerere leo anakuwa kama mpiga filimbi wa Hamelin
 
Ni gazeti zuri sana na wamelipa rangi safi sana kwa mbele. Nimeliona leo na watu wanaligombea sana kwa kweli. Kichwa cha habari kinasema ''LOWASSA AONGOZA KURA ZA MAONI''

Sasa kitendawili cha dhamira halisi ya gazeti hili kimeteguliwa. All the best katika njia ya kuelekea kule yaliko Mtanzania na Rai.
 
Akiandika kama mwanahalisi na mengine yafananayo tutalisoma,otherwise linapigwa na jua kwenye vituo mpaka litapauka
 
Gazeti bomba hili, nimeshapata nakala yake we ponda tuu wenzako tunasoma wewe endelea na magazeti yako ya TAZAMA na UHURU magazeti ya kufungia vitumbua uswahiliini
 
Habari nilizozipata usiku huu ni kwamba gazeti mnalolisubiri kwa shauku kubwa liitwalo JAMHURI linalomilikiwa na EL nitaingia mtaani Jumanne hii. Anzeni kupata toleo la kwanza hadi mfikie hatua ya ku-judge kama linampigia debe kweli EL kwa 2015, linampigia debe kwa 2012 CCM chaimanship au kuna jingine nyuma ya pazia. Tahadhari: USINIULIZE SOURCE PLZ

JUMANNE INAKARIBIA KWISHA SASA HIZO NAKALA ZA JAMHURI ZIKO WAPI??AU JK KAZINUNUA ZOTE NA KUZICHOMA??

nani ameona hili gazeti au ndio uzushi wa wazushi
 
Ni gazeti zuri sana na wamelipa rangi safi sana kwa mbele. Nimeliona leo na watu wanaligombea sana kwa kweli. Kichwa cha habari kinasema ''LOWASSA AONGOZA KURA ZA MAONI''

Acha uzushi Mwita...!Title ya gazeti la Jamhuri la leo j4 ni "MTEGO WAINASA CCM".Hilo la kwako sijui la lini!
 
Liache lije. Wasomaji tutaamua kama linafaa au la. Si unaona RAI limeanza kubadilika, siku hizi linaandika yale ambayo miezi michache iliyopita lisingeandika. Uchaguzi wa 2015 unaanza kuandaliwa, Si unajua tena wakati huo magazeti huota kama uyoga na hupotea mara baada ya matokeo kutangazwa.
 
Nilikuwa nalipitia Gazeti jipya la kila wiki la JAMHURI ambalo nakala yake ya kwanza imetoka leo. Gazeti hili linalodaiwa kumilikiwa na waandishi nguli Deodatus Balile na Manyerere Jackton limekuwa likipigiwa upatu kwa muda mrefu kwamba litakuwa bora na hata kauli mbiu yao ni kwamba "Tunaanzia wanapoishia wengine" inaashiria hilo.

Kilichojitokeza katika pitia yangu ni kwamba gazeti hili halijaja na kitu kipya au chochote kinachoakisi weledi wa uandishi na ubobevu wa wamiliki wake. Habari zimeendelea kuwa ni nyepesi, na character assassination ya wale wanaochukuliwa kwamba ni maadui wa wenye magamba imeendelezwa. Kwa ujumla "layout" ya gazeti hili na hata maudhui yake yanafanana sana na gazeti la Mtanzania na pengine ni sahihi kwamba wao wameanzia pale yanapoishia magazeti dada ya gazeti hili, nikimaanisha Mtanzania na Rai.

Kwa haya niliyoyaona humu, ni dhahiri kwamba kumbe misitu tu ndiyo imebadilika lakini nyani ni wale wale.
 
hebu acheni ku-promote magazeti ya kuwashia majiko ya kuni

why you people like these kind of bad publicity na vitu vilivyotengenezwa kwa faida ya wachache??
 
Kwanza niliposikia mapacha hawa wanaanzisha gazeti mimi nikajua ni kupanua wigo wa magazeti mamluki baada ya kuona kwamba Habari Corporation imeshashtukiwa na haina tena mvuto wala ushawishi kwenye jamii. Hata mimi nimelipitia na tayari kwenye toleo la kwanza Sitta ameanza kuwambwa msalabani. Sishangai hata hivyo kwa sababu mfadhili mkuu wa gazeti hili ni Fred Lowassa.
 
hebu acheni ku-promote magazeti ya kuwashia majiko ya kuni

why you people like these kind of bad publicity na vitu vilivyotengenezwa kwa faida ya wachache??

Hivi umeeleweka mkuu? Issue hapa ni kwamba gazeti limeboa. Wewe una maoni gani?
 
Nilikuwa nalipitia Gazeti jipya la kila wiki la JAMHURI ambalo nakala yake ya kwanza imetoka leo. Gazeti hili linalodaiwa kumilikiwa na waandishi nguli Deodatus Balile na Manyerere Jackton limekuwa likipigiwa upatu kwa muda mrefu kwamba litakuwa bora na hata kauli mbiu yao ni kwamba "Tunaanzia wanapoishia wengine" inaashiria hilo.

Kilichojitokeza katika pitia yangu ni kwamba gazeti hili halijaja na kitu kipya au chochote kinachoakisi weledi wa uandishi na ubobevu wa wamiliki wake. Habari zimeendelea kuwa ni nyepesi, na character assassination ya wale wanaochukuliwa kwamba ni maadui wa wenye magamba imeendelezwa. Kwa ujumla "layout" ya gazeti hili na hata maudhui yake yanafanana sana na gazeti la Mtanzania na pengine ni sahihi kwamba wao wameanzia pale yanapoishia magazeti dada ya gazeti hili, nikimaanisha Mtanzania na Rai.

Kwa haya niliyoyaona humu, ni dhahiri kwamba kumbe misitu tu ndiyo imebadilika lakini nyani ni wale wale.
Hapo kwenye red huo si ndo mpambe no.Wa RA?
 
Back
Top Bottom