Gazeti la Jamhuri lalipoteza gazeti la Kubenea la Mwanahalisi

Kiukweli jamaa kama kunywa rangi ya kijani,imekulewesha haswaa! Hivi kuna gazeti lililo fichua ufisadi Nchi hii zaidi ya mwanahalisi.Kufungiwa kulitokea baada ya kuona hili gazeti linazidi kuwafumbua watanzania macho.Kwenye ukweli sema kweli na siyo kuleta mihemko ya chama.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Hapo zama za kale kulikuwa na kijigazeti kimoja ambacho kilijiita Mwanahalisi. Kigazeti hicho kilibobea kwa udaku huku kikijificha kwenye chaka la kufanya uchunguzi. Kwa vile baadhi ya watu walikuwa wanashabikia sana udaku, kigazeti hicho kikajipatia umaarufu. Umaarufu huo ukawalewesha wamiliki wa kigazeti hicho.

Baada ya miaka kadhaa kupita, Bonge la Gazeti likaanzishwa kwenye kaya. Gazeti hilo ambalo lilipewa jina la Jamhuri likaanza kuwafumbua macho wana kaya na kuwabainisha zipi habari za uchunguzi na upi udaku. Kilichowafumbua macho wanakaya ni jinsi gazeti hilo la Jamhuri lilivyofichua njama zinazotumika bandarini kuiba mafuta huku wakitumia mchoro unaoelezea kila pahala ambapo mafuta yanachepushwa.

Kuona hivyo ndivyo wana kaya wakany'amua. Wakabaini zipi habari za uchunguzi na upi ni udaku. Kuanzia wakati huo, Mwanahalisi limepotezwa kabisa na Jamhuri linaendelea kupaa. Mwanahalisi limepotezwa na mmiliki wake Saed Kubenea hana ujanja tena. Amebaki anatweta twe twe twe tweeeee!
kuna gazeti linaitwa jamhuri? la hapa hapa Tanzania?
 
Umekopy Na kupest....yawezekana hata hilo gazeti la mwanahali huwa hulisomi....Acha mbwembwe kijana
 
Siri za JK, Singasinga zafichuka

Chanzo:Mwanahalisi

Na Ansbert Ngurumo - Imechapwa 28 March 2016

SIRI kati ya Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete na Harbinder Singh Sethi (Singasinga), aliyekwapua mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Tegeta Escrow, zimeanza kuvuja.

Mabilioni ya shilingi yaliyochotwa katika akaunti ya Escrow, ndani ya Benki Kuu (BoT), yalitoroshewa nchini Austria, kupitia Afrika Kusini na Dubai, MwanaHALISI linaweza kuripoti.

Mkakati wa kukwapua na kutorosha mabilioni hayo, ulisukwa kwa ustadi mkubwa na Singasinga kwa kushirikisha vigogo waandamizi serikalini na Ikulu.

Vyanzo vya taarifa kutoka serikalini na Ikulu vinasema, Sethi "alitoa rushwa kila mahali, ikiwamo Ikulu," ili kufanikisha mpango wake huo.

"Alihonga kila mtu. Alitoa rushwa kwa kila aliyeona faili la Escrow. Hadi maofisa wa Ikulu na viongozi waandamizi serikalini walihongwa," ameeleza mmoja wa viongozi waandamizi kutoka wizara ya fedha.

Amesema, "…hadi ndani ya jumba jeupe (Ikulu kwenyewe), Singasinga alitembeza mlungula. Ni BoT pekee, ambako hakuhonga au kuombwa rushwa."

Kampuni ya IPTL – Independent Power Tanzania Limited – ilijifunga katika mkataba na serikali wa miaka 20, wa kuzalisha megawati 100 za umeme wa dharura na kisha kuuza umeme huo kwa shirika la umeme la taifa (TANESCO).

Akaunti ya Tegeta Escrow ilifunguliwa mwaka 2004 baada ya serikali kubaini udanganyifu katika gharama za ununuzi wa umeme na mtaji wa IPTL.

Kampuni hiyo binafsi ilidai kuwa gharama za umeme zilikuwa asilimia 22.3; na gharama za mtaji asilimia 30 zilikuwa dola za Marekani 38.16 milioni. Hata hivyo, Mahakama ilithibitisha kuwa gharama halisi za mtaji wa IPTL, zilikuwa chini ya dola za Marekani 1,000.

Hadi Novemba 2014, akaunti hiyo ilikuwa imehifadhi zaidi ya dola 120 milioni. Mamilioni hayo ya dola yaligawanywa mithili ya "shamba la bibi" kwa aliyejiita mwekezaji mpya wa IPTL, kampuni ya Pan African Power (PAP).

Mabilioni ya shilingi yalilimbikizwa na Tanesco, katika akaunti hiyo, baada ya kuibuka mgogoro juu ya malipo ya gharama ya uwekazaji wa mitambo na gharama za kuweka mitambo (Capacity Charge), kati ya IPTL na Tanesco.

Lakini fedha hizo zilichotwa kabla mgogoro huo haujapatiwa ufumbuzi na katika mazingira ya udanganyifu; na kwa kutumia baadhi ya nyaraka ambazo zilikuja kugundulika kuwa ni za kugushi.

Sethi aliwasilisha serikalini nyaraka zinazomuonesha kuwa ndiye mmiliki mpya wa IPTL. Alidai kuwa amenunua kampuni hiyo kupitia kampuni yake ya Pan African Power (PAP).

Hata hivyo, Sethi alishindwa kuweka uthibitisho wowote kuwa kampuni hiyo inamiliki hisa za kampuni ya Mechmar Limited ya Malaysia ndani ya IPTL.

Kampuni ya Mechmar inamiliki asilimia 70 ya hisa katika IPTL. Mmiliki mwingine, ni VIP Engineering ya jijini Dar es Salaam, iliyokuwa ikimiliki asilimia 30 ya hisa.

Jitihada za kupata viongozi serikalini wakiwemo wa Wizara ya Fedha, zimeshindikana. Na simu ya Katibu Mkuu wa Hazina, Dk. Servacius Likwelile iliita kwa muda mrefu mara kadhaa bila kupokewa.

Taarifa zinasema, Gavana Ndullu alichukua tahadhari zote juu ya fedha hizo, ikiwamo kumjulisha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi, Dk. William Mgimwa (sasa marehemu), umuhimu wa kumjulisha Rais Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusu malipo hayo.

Anasema mtoa taarifa, "Kwa kuwa BoT ilipewa jukumu hili kwa makubaliano, uwajibikaji wake na mipaka ya uwajibikaji huo unabaki kuwa ni uleule ulioelezwa katika makubaliano hayo."

Lakini gavana anaripotiwa kwenda mbali zaidi, akitaka kupata hakikisho kwamba utekelezaji wa uamuzi wa mahakama, pamoja na makubaliano ya kukabidhi fedha, unapata baraka za wakuu wa nchi kama vile Rais na Waziri Mkuu.

"Pia BoT ilihakikisha kwamba mahitaji yote ya msingi kama vile, makubaliano ya kuhamisha fedha, kinga dhidi ya madai au mashitaka baada ya malipo, na suala la kodi ya ongezeko la thamani (VAT), vinapata ufafanuzi, baraka na mwongozo unaostahili," ameeleza mtoa taarifa.

Anasema BoT iliamua kuchukua hatua hizo, ili kujinasua na madai mapya ambayo yangeweza kuibuka baada ya fedha kuhamishwa kutoka benki.

"Gavana alimkatalia Dk. Mgimwa kuchukua fedha mpaka kwanza amjulishe rais. Alikataa hata maelekezo ya mwanasheria mkuu wa serikali, Jaji Fredrick Werema, aliyetaka fedha hizo zilipwe, hata bila benki kujihakikishia usalama wake," ameeleza ofisa wa serikali.

Kwa mujibu wa nyaraka, BoT ilihamishia mabilioni hayo ya shilingi kwa PAP kupitia akaunti yake iliyoko benki ya Stanbic baada ya Sethi, anayedai kuwa mmiliki wa IPTL, kumuelekeza gavana.

Waraka wa Sethi kwenda kwa gavana Ndulu ulielekeza fedha hizo kulipwa kwa akaunti Na. 9120000125324, iliyopo benki ya Stanbic, tawi la Tanzania.

Sethi alimwandikia gavana tarehe 28 Novemba 2013, zikiwa siku 37 (21 Oktoba hadi 28 Novemba 2013) tangu mkataba kati ya serikali na PAP kufungwa.

Mkataba wa upelekaji fedha katika akaunti ya Escrow ulifungwa tarehe 21 Oktoba 2013.

Malipo hayo kwa PAP yalifanyika bila Waziri wa Nishati, Prof. Sospeter Muhongo, wala BoT kuhakiki uhamishaji wa hisa kutoka Mechmar kwenda PAP; bila PAP kusajili hisa zake nchini; bila PAP kuthibitisha kujisajili Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC); na bila kuwa na hati ya mlipa kodi (TIN).

Mkataba kati ya serikali na IPTL ulielekeza fedha zilizohifadhiwa katika akaunti ya Escrow, zilipwe kwa kampuni ya PAP kupitia tawi la Tanzania la United Bank Limited (UBL) – yenye matawi zaidi ya 1,300 katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Qatar, Yemen, Marekani, Pakistani, Uingereza, Uswisi, Oman, China na Tanzania.

Mkataba huo uliagiza fedha hizo zilipwe kupitia akaunti mbili za PAP; ambazo ziko katika benki ya UBL; hizo ni zile zenye Na. 010-0016-0 – ambayo ni ya fedha za Tanzania na 060-0016-7 ya dola za Marekani.

Hata hivyo, gazeti hili limeelezwa kuwa kilichofanya fedha hizo kutolipwa katika akaunti ya UBL, ni kukosekana kwa fedha katika Akaunti ya Escrow.

"Serikali ililazimika kukopa "kwa siri" kiasi hicho cha fedha kutoka Stanbic kwa kuweka dhamana ya hati fungani, ili kufanikisha upatikanaji wa fedha za kumlipa Singasinga wa IPTL," ameeleza mmoja wa maofisa wa Stanbic ambaye ametoka katika benki hiyo hivi karibuni.

Anasema, "…fedha zote zilizopaswa kuwepo, kiasi cha dola 122 milioni, zilikuwa zimewekezwa na BoT na kiasi kingine cha dola128 milioni, zilikuwa hazijawasilishwa na Tanesco kwa muda mrefu."

Taarifa zinasema, BoT iliwekeza dola za Marekani milioni 22 nchini Ufaransa na Sh. 148,071,613,572.93 iliwekeza katika Hati Fungani (Treasury Bills) za siku 182 .

Kigogo huyo anasema, "kwa vile wakubwa walishapanga kumlipa Sethi, kabla ya kumalizika Desemba 2013, ikabidi wakope benki kwa kuweka dhamana hati fungani zilizoshushwa bei (discounted treasury bills)."

Anasema, katika muhamala huo, Benki ya Stanbic, tawi la Tanzania, ilitengeneza faida ya kitita cha dola za Marekani 18 milioni (Sh. 39 bilioni).

"Ile haikuwa biashara ndogo kwa benki. Yaani siku moja, unapata biashara inayokupa faida ya dola 18 milioni. Hizi ni fedha nyingi sana; na ambazo hakuna benki ambayo inaweza kuziachia," anaeleza.

Anasema, "kile ambacho kinaniumiza moyoni, ni kuona taifa linakopa ili kumlipa mtu ambaye mpaka leo kuna utata juu yaumiliki wake katika IPTL."

Taarifa zinasema, katika kiasi hicho cha dola 180 milioni, dola takribani 100 milioni, kilitoreshewa nje katika nchi za Falme za Kiarabu, huko Dubai na Afrika Kusini, kabla ya kuhamishiwa tena nchini Austria.

Nchini Austria, taarifa zinasema, ndiko ambako mtoto wa mmoja wa waliokuwa viongozi wajuu serikalini, amefungua akanuti.

Anasema, "Austria ndiyo imechukua nafasi ya Uswisi…nchi hiyo haina mkataba wa aina yoyote wa kuibana kufichua taarifa za kibenki za wateja wake na ndiyo maana fedha zilipelekwa huko."

Anasema, taarifa za kukopa fedha ili kumlipa Sethi na PAP zilifanywa kuwa siri kwa hofu kwa vile taratibu nyingi zilikiukwa, hali ambayo ingeweza kuibua tena mjadala mwingine juu ya sakata la Escrow.

Anasema, "mnachokiona kwenye maandishi ni nyaraka tu toka BoT kwenda kwa Sethi; fedha zilitoka Stanbic kwa makubaliano maalumu ya kuuziana hati funganizi lizoshushwa thamani."

MwanaHALISI limeelezwa kuwa katika mradi huo, Benki ya Stanbic, ili kufanikisha ukwapuaji wa dola milioni 250 (Sh.550 bilioni), ililazimika kupata baraka kutoka makao makuu nchini Afrika Kusini.

Kibali kutoka nchini Afrika Kusini, kimesainiwa na Bw. S. J Kok ambaye ni mkuu wa hazina wa kanda ya Afrika Mashariki na Malcom Low.

Fedha ambazo zilichotwa kwa njia ya uuzaji wa hati fungati, zingetosha kununua madawati milioni tatu na nusu (yanayohitajika nchi nzima); na kiasi kingine kujenga barabara ya urefu wa kilomita 50, kingebakia mikononi mwa serikali.

Taarifa hizi zinakuja kukiwa na kigugumizi kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kufikisha mahakamani watuhumiwa wote wakuu wa wizi katika akaunti ya Escrow, licha ya uchunguzi kukamilika miaka miwili iliyopita.

Mara baada ya mabilioni hayo kuingizwa katika akaunti, kiasi cha dola 70 milioni, Sethi alikilipa kwa Rugemalira.

Kiasi kingine cha fedha kilichosalia, wanufaikaji walikibeba kwa magunia na mifuko ya plastiki.

Baada ya Rugemalira kupewa kiasi alichohitaji, Sethi alibakiza kiasi cha dola 180 milioni, pamoja na mtambo wa kuzalisha umeme wa IPTL aliopewa kama sadaka.

Mbali na fedha hizo, Sethi na PAP wameendelea kulipwa kiasi cha Sh. 6 bilioni kila mwezi na Tanesco.

Sethi ameanza kulipwa mabilioni hayo ya shilingi, tokea Januari 2014, licha ya Bunge kuamuru malipo hayo kusitishwa.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, mkataba wa kugawana fedha kati ya serikali na IPTL, ulisainiwa na Eliakim Maswi. Alikuwa katibu mkuu wizara ya nishati na madini.

Wengine waliosaini mkataba wa uhamishaji fedha, ni Singasinga Sethi na Joseph Makandege, ambaye ni mwanasheria na katibu wa kampuni ya PAP.

Hadi sasa, wote wanne, hawajafikishwa mahakamani kujibu tuhuma za wizi wa fedha za umma.

Bunge ambalo lilijadili ripoti ya uchunguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), lilimtaja Sethi kuwa mhalifu aliyekubuhu; anayepaswa kukamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Vyombo vya habari, ikiwamo mitandao ya kijamii, vimeripoti kuwa Singasinga "alitokea ikulu" kabla ya kukwapua mabilioni ya shilingi kutoka akaunti ya Escrow katika Benki Kuu.

Bunge limeagiza kufanyika taratibu za kisheria, kuitangaza benki ya Stanbic kuwa ya utakatishaji fedha haramu.

Mkataba wa malipo kati ya IPTL na serikali, umeambatana na muhtasari wa kikao cha pamoja cha uhakiki wa malipo ya tozo kati ya kampuni hiyo ya kigeni na Tanesco.
 
Hicho ni udaku au uchunguzi?
 
Back
Top Bottom