Kubenea na Mwanahalisi yake

muda wa ukombozi

Senior Member
Jun 28, 2013
119
225
KUBENEA NA MWANAHALISI YAKE

Wakati serikali bado wanahangaika na harakati za kumtafuta Faru john kwa njia mbalimbali ikiwemo utaalamu wa kupima vinasaba vya pembe walizokabidhiwa ikidaiwa ni za Faru john kuna madai ya kichokozi yakaibuka watu wakasema zile pembe ni za Faru Khadija kabla hata uchunguzi wa vinasaba haujatolewa.

Wakati familia ya Ben saanane wapo kwenye sintofahamu hawajui kijana wao yupo wapi, yupo kwenye hali gani, yupo mazingira gani, sasa yapata mwezi wa pili hawajamtia machoni kijana wao huyo, waziri wa mambo ya ndani ametangaza serikali inamtafuta rafiki yake huyo sasa cha kushangaza mwandishi nguli wa habari za kichunguzi anaeaminika na watanzania wengi ameibuka kupitia gazeti lake la mwanahalisi na kudai taarifa alizokuwa nazo zinasema Saanane ambaye haonekani nyumbani wala kazini anaonekana kwa marafiki zake mitaani.

Nimetafakari sana hii habari iliyochapishwa na moja ya gazeti ambalo naliheshimu sana watu wenye uwerevu wengi utakutana nao wameshika mkononi gazeti hili ni gazeti ambalo limepata umaarufu mkubwa kwa habari za kichunguzi tena uchunguzi haswa lakini kwa habari hii ya Ben kuonekana kwa marafiki zake huko mitaani mtu ambaye watanzania wanaamini hajulikani halipo inashangaza sana.

Kwa chanzo cha habari ambacho hakina mashiko, hakuna atayeweza kuelezea taarifa hiyo, hajulikani aliyeanzisha taarifa hiyo, taarifa hiyo haijawahi kuelezea Saanane anaonekana mitaa gani, taarifa hiyo haijawahi kueleza Saanane anaonekana kwa marafiki zake wakina nani? Naendelea kutafakari hata baada ya kupata taarifa hiyo kama ambapo mwandishi anadai andishi la mkono lililoachwa kwenye lango la gazeti hilo Mtaa wa Kasaba, kinondoni Dar es salaam ambalo linasema “Ninyi jisumbueni tu. Huyu mtoto yupo na akitokea mtashangaa”

“hamumfahamu Saanane sisi tunajua alipo wala hatuoni anaetishia maisha yake kuna wanaodai kauawa ni waongo anapumua kaa chonjo” hivi taarifa hii ilikuwa ina ulazima wa kuandikwa kwenye gazeti kama mwanahalisi, hivi taarifa kama hii ambayo inaweza kutungwa na yoyote inaweza ikawa ni chanzo chako cha kuaminika kama taarifa bila kufanya utafiti mwingine wa ziada, sijui nisemaje ila kwa taarifa hii ambayo imeandikwa na gazeti linalomilikiwa na mbunge wa chadema ambapo Saanane ni mwanachama na Mfanyakazi wa chama hicho kwa cheo cha msaidizi wa mwenyekiti wa chama kulikuwa hakuna haja ya kukurupuka na kuandika habari kama hii bila kufanya utafiti kidogo.

Taarifa hii inaweza kupoteza mvuto kwa chama na kwa gazeti pia itaonekana kumbe chadema ili kutafuta “kick”unajipoteza kwanza falsafa za kizamani alizotumia “mfalme makavelli” au ndani ya chama chenyewe wanachaama wanachuki na uroho wa madaraka wapo tayari kupotezana kwasababu ya vyeo na madaraka leo hii vijana wanamshambulia kwa nguvu zote kubenea wakidai alikuwa na mahusiano ambayo sio mazuri na Saanane ndio maana amekurupuka kuandika habari hiyo kwa mihemuko ili hata siku akija kupatikana au kuonekana asije kupata “kick ya kisiasa” kupata faida ya kuonekana ni shujaa kutokana na siasa zake ambazo hazina uwoga hata kidogo.

Sasa kama wanachama wako hivi na harakati za chama siku moja kushika dola, kuwa na wanachama wa aina hii ambao wenyewe tu hawana nia moja, kuna mwanachama mzalendo kweli au wote wanachama maslahi?

Mi nilidhani wakati huu ndio ulikuwa wakati ambapo vijana wote wa bavicha, wanachama wote wa chadema na ukawa kwa pamoja kupaza sauti kwa serikali atafutwe Bena Saanane na sio kejeli kuonesha kwamba kajipoteza ili atafute “kick za kisiasa” na kejeli hizo eti kawasababu hamuelewani, hamuna mahusiano mazuri ikumbukwe unaweza ukawa haupatani na Ben Saanane ila kumbuka huyu mtu ana wazazi wake, baba na mama yake, ana mke wake, ana wadogo zake, ana ndugu zake, ana marafiki zake hawa wote hauwezi kujua maandishi ya kejeli yanayochapishwa wanayachukuliaje, mi naomba tumtangulize Mwenyezi Mungu mbele, tuombe Ben apatikane, ila tusitafute pesa kwa kuuza gazeti kwa taarifa ambazo hazina tafiti, wachina wanamsemo wao wanasema kama haujafanya tafiti, hauna haki ya kuongea.

Muda wa ukombozi
 
miezi inaendelea kupita hakuna dalili yoyote inayoonesha kana kwamba ndugu yetu, kijana mwenzetu, mmoja ya vijana wasomi wa nchi hii, kwamba anaweza kupatikana, bado tunasubiri vyombo vyetu sikivu vya usalama na uweledi waliokuwa nayo jinsi gani vitakuja kutupa taarifa.
vilevile tunasubiri harakati za lema, lissu pamoja na zito kabwe zitafikia wapi kuwezesha taarifa ya kijana mwenzetu.
MUNGU ibariki Tanzania.
 
moudgulf

JF-Expert Member
Jan 23, 2017
87,390
2,000
Kuna gazeti na mmiliki. kama mmiliki ndiye mwandishi wa hiyo taarifa au yeye ndiye mhariri yafaa wahojiwe na vyombo vinavyochunguza kupotea kwake. maana huenda siri ya kupotea kwa Saanane wanaijua. binafsi siamini kama taarifa hiyo ni ya kutunga vinginevyo gazeti hilo lijitokeze kuomba msamaha
 
muda wa ukombozi

Senior Member
Jun 28, 2013
119
225
Bila shaka wakati tunaendelea na harakati za kujua hali ya Ben saanane ingekuwa busara serikali ingewahoji walioandika taarifa kwny gazeti hilo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom