Msigwa yeye ni mchungaji
na anajua tuhuma zipo za CHADEMA kuwa chama cha wakristo
hata kama hizo tuhuma si za kweli na za kutunga
hakupaswa kuwa reckless na kuanza kuita CHADEMA kanisa
Mifano ipo mingi ya kufikisha ujumbe
Kutumia mifano ya aina hiyo ni ama uzembe au kiburi na kutokujali kina nani hawatapendezwa
Gazeti limeripoti kama alivyosema Mchungaji wa Chadema Msigwa.
Kasema kweli Chadema ni kama Kanisa.
Sasa hapo unalishambulia gazeti kwa kosa gani, wewe umejuaje kama Mchungaji Msigwa alikuwa hana maana hiyo.
bill of right is part of our constitution na ina guarantee freedom of expression na speech. acheni kuturudisha kwenye ukoloni wa waarabu na wazungu, no way!!Hakuna kitu kilokuwa low, and nothing has been blown out of proportion, it was bad judgement on his part kutumia maneno hayo, kama previous contributors walivosema, there were a lot of examples angeweza kutumia, without resorting to religion. Wakati huu is no time to add fuel to the fire.
Wemwenyewe mamlaka bado ujiamini??nenda peleka malalamiko police ukiwa na vithibitisho na pia ujiandae kulipa garama zakesi kama utashindwaNimefadhaishwa sana na gazeti la Al-Huda litokalo kila wiki toleo na.523 SHAWWAL1436 la tar23-29, Julai 2015 Uk wa mbele limepambwa na maneno.
Msigwa: CHADEMA kama kanisa
*Asema wanahubiri habari ya wokovu
*Wanachama waislamu sasa mashakani
Kimsingi kauli hizo ni za kichochezi dhidi ya waislam na wakristo! Ifahamike kuwa Mchungaji Msigwa(Mbunge wa Iringa) alitoa kauli hiyo kifalsafa kumkaribisha Lowassa ndani ya Chadema! Msigwa alisema "...CHADEMA ni kama kanisa, hakataliwi mtu, tunahubiri habari njema ya wokovu, unatubu unafanya kazi!"
Mimi siyo msemaji wa Msigwa, lakini nimekerwa na gazeti hilo kwa sababu kauli ya Msigwa haikulenga kutugawa Wanachama wa CHADEMA kwa misingi ya kidini! Ni kama kauli ya Tundu Lissu alipotamka kuwa "...John Pombe Magufuli na kabila lake la MaCCM..." hakulenga kuwa kuna kabila la MaCCM!
Kwahiyo siyo kweli kuwa Msigwa alimaanisha CHADEMA ina wafuasi wa Kikristo pekee!
Naomba mamlaka husika iingilie kati! Mungu Ibariki Tanzania!
Mkuu wanakera sana! Wanatufanya tuchelewe kujadili mustakabali wa taifa letu wanatutumbukizia mambo ya kipuuzi, wanataka kutuchelewesha tujadili upuuzi wao huu wa udini!