Gazeti gani hulipendi?

thuma

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
369
496
Magazeti yapo mengi lkn kila gazeti lina heshima yake kutoka na habari zinazochapishwa.

Hata ukienda kwa mawakala wa magezeti watakwambia kuna gazeti wanauza idadi kubwa lkn kuna mengine wanazalisha kopi chache na bado haziishi yaani hayana wateja kabsa.

Mm binafsi nalichukia sana gazeti la Uhuru, hili gazeti usitegemee kupata habari ya kweli, ni gazeti linaloandika lisiyo yataka maana Wahariri hawana Uhuru ...

Je wewe gazeti gani hulipendi toa na sababu.
 
Kuna Gazeti moja ambalo hata wamiliki wake hawalisomi "UHURU".

Na sijui kama UHURU Publications bado wanafanya biashara au wanachapisha tu kwa ajili ya kulinda jina? Sijawahi kwa muda mrefu kuona mtu anasoma gazeti la Mzalendo, Uhuru! Au ndiyo sheria kuwa yanaenda kwenye ofisi za serikali na Chama
 
Mwaka Jana nilikuwa wilaya moja mkoa Wa RUKWA akapita muuza magazeti. Japo kule Gazeti zinachelewa nikaona nichukue moja. Nikanunua Mwananchi lakini nikaona Gazeti la Uhuru, nikamuuliza hili Gazeti linanunuliwa? Akasema huwa analetewa nakala 10 tu lakini akibahatika anauza moja. Cha ajabu alichonieleza, Hata Mkuu Wa wilaya ambaye ni kada ananunua Gazeti zaidi ya 3 lakini Uhuru si mojawapo.

ACHA nikae KIMYA...!
 
Wanajua hakuna cha maana watakachopata humo
 
Na sijui kama UHURU Publications bado wanafanya biashara au wanachapisha tu kwa ajili ya kulinda jina? Sijawahi kwa muda mrefu kuona mtu anasoma gazeti la Mzalendo, Uhuru! Au ndiyo sheria kuwa yanaenda kwenye ofisi za serikali na Chama
Wapo kwaajili ya kulinda ajira zao tu.
 
Back
Top Bottom