Wanafunzi wengi waliomaliza vyuo vikuu hawana reasoning and cognitive skills

Ultimate

JF-Expert Member
Nov 29, 2016
713
1,738
Aise hali sio poa kabisa.

Sijui sasa hivi huko vyuoni wanawafundisha nini hawa watoto.

Ipo hivi juzi juzi hapo kulikua kunaitajika new staff. Pendekezo lilikuza hawa staff wapya wawe graduate wapya (Walio maliza mwaka huu) au mwaka jana lengo lilikua kuwapata fresh from school ile wawe trained hapa hapa wasije kuharibu kazi.

Tukapeleka pendekezo chuo kimoja kikubwa tu hapa mjini. Tunaomba Top Performer kenye course moja inayohusiana na Mambo ya Economics, Econometrics na Actuary Analysis.

Tukapewa list na namba zao za simu. Baada ya Hapo Vijana wakatafutwa wakapewa maelezo, Ofisi zilipo na siku yakuja kwa maelezo zaidi. moja ya japo waliopewa ni kwamba saa nne kamili wawe tayari wameshafika tayari.

Siku ya tukio sasa (Tulipata vijana sita). Hapa ndio vituko vilianza (Sijui walijua wanakuja kufanya interview) tukawachukua wakapelekwa meeting room, tukawapa magazeti haya haya ya Kiswahili sijui Nipashe, Uhuru Mwananchi, Raia Mwena, MwanaSpoti etc. wakaambiwa kwenye hayo magazeti wachambue habari zinazohusu economy (Mfano labda kwenye gazeti wameandika Serikali imezindua daraja la Wami. Watuambie hii kiuchumi ni nini na ina implication gani kwenye Macreconomic).

Pia condition ilikua moja wapo ikiwa habari au concept itajirudia kwa watu watatu hiyo concept au habari inakua deducted kwa watu wote (Haihesabiki). Tukawapa na mtu wa kuwasimamia pia na wifi (Free wifi speed ilipunguzwa, network iwe nzito <ili tuangalie watapoteza muda kwenye network au wata concentrate kwenye task)

Muda Ukaenda ukaisha. Kila mtu aka submit copy ya alichopata. Wakaja kwenye panel ku-present findings zao. Aise Hali ni mbaya mtu masaa karibia 6 magezeti karibu 8 amepata habari 2 za kiuchumi, mwingine 4, mmoja alijitutumia akapata 7.

Mtu unamuuliza sasa wewe imekuje umepata habari mbili tu anaanza mara hoo, mageti langu lilikua na habari za siasa nyingi yaani bla bla tu hamna kitu. Mtu unamuuliza hii habari yaserikali imetoa fedha za kujanga madarasa kwa kutumia force account hii si monetary policy hihii? au sio habari za ki uchumi anaanza kumumunya maneno.

Kitu kilicho nishagaza ni mtu unamwambia tupe twakimu za watoto chini ya miaka 5 kwa sasa hapa nchi. Mtua anaingia google jibu la kwanza au lapili litakalo tokea ndio analitaja.

Nikawa nawaza sasa kama hawa ndio top performer sijui best students hao wengine itakuaje. Imebidi tuchukue tu baadhi sasa tutafanyaje.

Lkn kiujumla baadhi ya wasomi wengi hama kitu.

Kuna kijana alikuja saa nne Karibia na robo nikesema hapa kazi ipo.
 
Wanakaririshwa na kiukweli siku hzi vyuoni hakuna usomaji narudia tena hakuna usomaji na tena hakuna usomaji visichana na vivulana haviko serious na shule viko kazi kupiga picha na kupost wanasubiri kugraduate, nilikua siku moja naongea na mdogo wangu kamaliza chuo akawa ananiambia yaani vyuoni hawasomi maana wengine Wana uhakika wa ajira wakimaliza hata akiwa na 'c'cheti kizima haijalishi, wengine wenzangu na Mimi wao wanakula Bata balaa hawajali na zile marks za kunnua Wachache sana wanajitambua very few of them kti ya 200 ni mmoja tu.

Yaani vitoto hivi wao na social media tu mda wote ila ukimuuliza hata waziri wake mwenye dhamana hamjui...
Sijaongelea kingereza hapo, huko ni majanga matupu.
 
Tuseme uko chuo kwenye hizo course za uchumi walisomea kuchambua habari au makala za kiuchumi kwenye magazeti ?

Waajiri wa hii nchi wamejaa ujinga ujinga mwingi Sana na ukweli ulio wazi ni kwamba wengi Elimu zao niza kuunga unga hivyo kuona kwamba vijana wapya kuwa tishio la nafasi zao
Kama magazeti yamewashinda kuchambua, data ndo wataweza?

Wewe nae huna reasoning and cognitive skills
 
Tusilaumu systems za chuo, sometimes wanafunzi wenyewe nd changamoto! Chuo kitasimam kwenye upande wake wa provision ya 25% of the contents na the rest itabaki kwa mwanafunzi mwenyewe.

Hapo ndo kwenye kazi sasa màana wanafunzi wanaaminishana chuo bata! Baada ya kujifunza na kutafuta knowledge! Wanajifunza ulevi, umalaya pamoja na kukimbizana na fashions!!
 
Wanakaririshwa na kiukweli siku hzi vyuoni hakuna usomaji narudia tena hakuna usomaji na tena hakuna usomaji visichana na vivulana haviko...
Acha kupotosha mkuu hiyo tafiti ya 200 anaye jitambua ni 1 umeitoa wapi?

Alafu tambua kwamba mitandao ya kijamii imekuwa sehemu ya Maisha ya watu hivyo hakuna kosa lolote kisheria mtu kutumia mitandao ya kijamii.

Unadai hawa somi Sasa wanafaulu vipi mitihani ? Unadai wanakula bata Sasa unataka waishe maisha Kama ya karne ya Nyungu ya mawe empire ?
 
Sijui sasa ivi huko vyuoni wanawafunisha nini hawa watoto
Mkuu, labda nikukumbushe jambo moja tu ya kwamba, hakuna interview ya siku moja inayoweza kukupa mfanyakazi bora, na hata CIA wanalijua hilo ndio maana wanafanya screening ya muda mrefu.

Kazi is not all about giving correct answers to few randomly chosen academic questions. Kazini kuna suala zima la kuishi na wafanyakazi wenzio, punctuality, interactions na mambo lukuki.

All in all, wakati ninasoma IAA watu wa computer science walilazimishwa kusomea accountancy semister ya kwanza, what for?

Mifumo yetu ya elimu bado ni hovyo sana.
 
Tuseme uko chuo kwenye hizo course za uchumi walisomea kuchambua habari au makala za kiuchumi kwenye magazeti ?

Waajiri wa hii nchi wamejaa ujinga ujinga mwingi Sana na ukweli ulio wazi ni kwamba wengi Elimu zao niza kuunga unga hivyo kuona kwamba vijana wapya kuwa tishio la nafasi zao
Sasa waajiri huwezi kuwapangia unachotaka mkuu! Wao ndio wenye dhamana na wanajua ni interview ipi inafaa kwa ajili ya kazi yao.
Sasa wewe unawapangia interview tena!
 
Back
Top Bottom