Gavana wa Benki Kuu Uganda amshambulia Museveni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gavana wa Benki Kuu Uganda amshambulia Museveni

Discussion in 'International Forum' started by sulphadoxine, Jun 17, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  KAMPALA, Uganda
  GAVANA wa Benki Kuu ya Uganda, Emmanuel Tumusiime-Mutebile amesema sera zisizotabirika za Rais Yoweri Museveni na nidhamu mbaya ya matumizi ya fedha serikalini imesababisha mfumuko mkubwa wa bei na kupunguza akiba ya fedha za kigeni.
  Tumusiime-Mutebile anaripotiwa kuliambia jarida la Financial Times (FT) la Uingereza kwamba hakukubaliana na uamuzi wa Museveni wa kutumia dola milioni 740 kununulia ndege za kivita.
  Alisema uamuzi huo ulisababisha kupungua kwa kiasi kikubwa cha akiba ya kigeni.
  “Alinipa ahadi kadhaa ambazo hakuzitimiza– kama vile njia ya kurekebisha tatizo la akiba hiyo. Na bado ninavutana naye,” Mutebile aliliambia
  FT.
  Wizara ya Ulinzi chini ya amri ya Rais Museveni ilichota dola milioni 400 kutoka Benki Kuu kununulia ndege za kijeshi bila idhini ya bunge.
  Machi 24 mwaka huu, Rais Museveni alikutana na wabunge kutoka chama tawala cha National Resistance Movement (NRM) na kuwataka kuidhinisha ununuzi huo chini ya kura maalumu.
  Rais aliwaambia wabunge hao kwamba ndege hizo ni za lazima kwa usalama wa Uganda kwa sababu sasa nchi imethibitishwa kuwa na akiba ya mafuta.
  Awali Kamati ya Bunge ya Mahesabu ya Umma ya Bunge la nane ilimwandikia gavana wa Benki Kuu kumtaka atoe maelezo kuhusu kuchotwa kwa fedha hizo bila idhini ya bunge.
  Lakini haijajulikana iwapo hilo lilitolewa maelezo lakini sasa inaonekana zilichotwa kutoka mfuko wa fedha za kigeni.
  Mutebile hutoa taarifa hadharani kwa nadra na kauli zake zinaonesha jinsi asivyoridhishwa na mwenendo wa serikali kuhusu uchumi

   
 2. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mutebile risks of being sacked by Museveni because what he spoke to the press is "termed" as insurbodination by Mu7
   
 3. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2016
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  INSURBODINATION OF THE GOVERNER
   
Loading...