mumak
JF-Expert Member
- Oct 24, 2013
- 1,069
- 661
Mkuu wazo lako ni zuri sana, lakini naona pale jangwani ni kama mapumulio ya maji ya nayotoka huku salenda yakiwa mengi sasa wakiubana yanaweza leta madhara mengine,ila hilo ni wazo langu tu najua hakuna linaloshindikana penye nia.Hivi inamaana huko manispaa ya Ilala hakuna mtu aliyewahi kuwaza hili hata siku moja?, magari ya taka husafiri takriban kilomita 70 toka katikati ya jiji hadi dampo la pugu, sasa ni kwanini hayo magari yasiombwe kuliinua lile bonde la jangwani kuja level ya juu ambayo haitafikiwa na maji huku wakiacha njia katikati (njia ya mto) kwa ajili ya kupitisha maji kwenda baharini. Kisha wapime viwanja vinavyopatikana kwa ajili ya matumizi ya Open space, City garden, City park, Car parking, small scale market place, sports center na mengine mengi. Sidhani kama watendaji wa manispaa wana elimu ya kutosha, seriously..