Gari ya Automatic

stephot

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2012
Posts
18,114
Reaction score
28,015
Nimekuwa nikiendesha magari ya automatic (sijui kwa manual gear) kwa muda mrefu,nimepata tatizo na hii ni mara ya pili kunitokea kwa gari tofauti,mafuta(Petrol) inapokuishia gari likiwa kwenye mwendo brake zinakataa kabisa kushika,bahati yangu ni kuwa huwa inanikuta mahali pasipo na mteremko mkali na mbele yangu hakuna gari hivyo inakwenda na kusimama yenyewe ndipo ninaiweka gear kwenye P na kufunga handbrake.Sasa kwa wenye ufahamu naombe tupeane maujuzi nini kifanyike unapokutwa na tukio kama hilo!
 
Nachojua katika hali hiyo brake zinatakiwa zishike. Ingawa si effective sana kama engine ikiwa ina run. The same huwa kwa stearing. Wanaojua zaidi watafafanua.
 

hata ukiwa kwenye mteremko kama iko kwenye D itasimama tu baada ya umbali mfupi,si imezima,ikiwa kwenye N HAPO NDIO HATARI.....solution jitahidi usiishiwe mafuta kwasababu hata usipopata ajali unaua FUEL PUMP,mafuta yakiisha au yakiwa chini sana fuel pump itavuta uchafu na itaanza malfunction na hatimae kufa kabisa,kwahio ndugu jitahidi 20,000/- isije kukugharimu 200,000/- or more.......
 
Asante kwa ushauri ndugu,si unajua mafoleni ya huu mji wa dar,unakaa kwenye foleni mpaka halftank yako inakatika hujafika destination.
 
Njia pekee ya kuepukana na hilo ni kuhakikisha hauishiwi na mafuta kwa gari yako
 

Mbona ni kitu kidogo sana tu,gari inatumia umeme kwenye function nyi gi sana(kwa case yako hydrolics),sasa mafuta yakiisha gari inajizima inabaki switch on(acc), kwa hiyo automatical vitu kama brake zinakua ngumu sana kuminyika..,(booster haifanyi kazi)

Masikitiko: Gari kukuishia mafuta mara kwa mara pamoja na kwamba kuna gauge meter ama indicator,madhara ya mafuta ya 1000 kama pik pik ya boxer ni makubwa zaidi,pump kufa,kuchelewa,uchafu kuingia kwenye sample,mara miss zinaanza unatafuta mchawi....

Goodmorning
 
Na vp baiskel kufel break?inasababishwa na nn?maana hapa kwetu KAHAMA hili limekua tatizo wakati wa mvua,yani unakuta umebeba gunia lako la mtama kwenda kuuza mnadani mara break zinafel na kengere pia inabuma lolz!
 
Na vp baiskel kufel break?inasababishwa na nn?maana hapa kwetu KAHAMA hili limekua tatizo wakati wa mvua,yani unakuta umebeba gunia lako la mtama kwenda kuuza mnadani mara break zinafel na kengere pia inabuma lolz!

Haiyumkini na mwenda kwa miguu ataleta hapa tatizo la breki zake!
 
Mkuu kama wadau wengine walivyochangia
Hapo lazima ujue tumadhara yatafuata baadaye maana Pump inanyonya hewa huaribika,na gari inapokuwa kwenye D

Upande mfano wa gari ya Manual husimama kwakuwa inakuwa na gear na mafuta yamekwisha. Na hiyo AT pia ilitakiwa isimame hapo bila kujari kama ni Mlima ama mteremko.
 

Nna mashaka na hilo mkuu! Kitu hakisimami kama kiko kwenye D, mpaka kifike sehem yenye kigongo ndy acceleration ikome! Hapo mi nadhani ukishaona kiwese kime tupia N kisha unaapply brake taratiibu to a standstill, other wise ukiiacha kwenye D kama ni kwenye mteremko jiandae na kuingia mtaroni,....even worse!
 
Nawashukuru wadau mawazo yenu ni mazuri sana ntayafanyia kazi,nawakaribisha wengine wenye ziada ili nipate maujuzi zaidi kwani natumaini somo hili litawasaidia wengi wanaopata matatizo kama yangu,karibuni!
 
Na vp baiskel kufel break?inasababishwa na nn?maana hapa kwetu KAHAMA hili limekua tatizo wakati wa mvua,yani unakuta umebeba gunia lako la mtama kwenda kuuza mnadani mara break zinafel na kengere pia inabuma lolz!

tatizo ni kununua baiskeli kwenye mnada, izo si nzuri...nunua swala mpya then ondoa au kata mud guard ya nyuma kwa upande wa mbele...apo tairi la nyuma litakuwa linaonekana....apo itakubidi uende kule Kaliua ununue makubazi...zamani tuliziita Arusha-to-Monduli shoe...zinavaliwa sana na wamasai ,then ukipanda swala au feniksi kwenye mteremko unaweka mguu wenye shoe kwenye tairi...utasikia wiiiiiiiiiiiiii,mpaka unasimama.
ONYO: 1.usifanye mchezo huu kwa kuvaa kandambili, itatoboka katikati karibu na kisigino.
2. Don't try this at home nor in town....
 

mkuu mimi si mtalaam sana kwenye maswala ya mzunguko wa umeme ila nijuavyo gari ikikata umeme lazima vitu vyote vinavotumia umume vitafeli, sio kuishiwa mafuta tu hata gari ikikata moto wakati iko spidi lazima breki itakuwa ngumu, sio kuwa itafeli kabisa ila utatumia nguvu ya ziada ili isimame, na hapo kuna hatari kama kuna gari au kisiki mbele ndo itakuwa breki yako ya nje....
Kama wadau walivoshauri inafaa usikubali gari iishiwe mafuta, fanya estimates ndo utakuwa umesevu kila kitu pamoja na pump. Tusisingizie foleni, foleni hautumii mafuta kiasi kuwa kutoka tazara mpaka mwenge uwe umemaliza lita 10,hapana. Kwa vi gari vya kawaida kama vyetu, gx 100, pajero, vitz,etc huwa unaweza kutumia si zaidi ya lita 3 ukikaa foleni kama lisaa na nusu bila ya kutembea ila usiwashe kiyoyozi(nb Kwa mtu wenye kipato kidogo,kiyoyozi ni anasa, ila usafiri ni non-luxury need). Je gari yako inatembea bila lita4?unalipenda kweli? na ikiwa kuna folen, ni bora ukaweka park gear au ukazima kabisa kama kwako wese ni test1. Ila kama gari iko kwenye D,then unakanyaga breki kwa muda wa lisaa uko palepale,sio siri utamaliza wese....
Mimi ni maskini ila kiukweli gari haijawahi kunikatia mafuta barabarani, huwa nacheza na gauge ya mafuta muda wote, ikienda down nafanya vinginevo....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…