Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Makampuni ya mafuta nchini yamewaandikia EWURA kulalamika dhidi kile kinachoonekana ni uchakachuaji wa mafuta ya diesel na petrol unaofanywa na kampuni inayoagiza mafuta nchini, Augusta Energy. Uchakachuaji huo, ambao pia unaathiri magari, ni ule wa kuchanganya diesel au petroli na ethanol kwa kiwango cha juu bila hata idhini ya serikali. Mafuta yaliyochanganywa na ethanol kwa kawaida yana bei ndogo zaidi, hivyo kampuni ikiagiza mafuta yaliychanganywa na ethanol na kuyauza kama yasiyo changanywa inapata faida kubwa sana.
Kuchanganya diesel au petrol na ethanol ni kitu cha kawaida bila gari kuathirika kwa kiwango cha 90:10, 10% ikiwa ethanol. Ukichanganya zaidi ya hapo lazima ubadilishe mfumo wa mafuta wa gari.
Rwanda, ambayo inapitisha mafuta yake Tanzania, tayari imeshakataa kupokea consignments za mafuta toka Tanzania kutokana na tatizo hili la uchakachuaji na ethanol. Rwanda huko nyuma ilifanya hivi pia kwa uchakachuaji wa kutumia mafuta ya taa, na hata kuwaweka ndani madereva wa Kitanzania waliobeba mafuta yaliyochakachuliwa.
Kisichoeleweka ni jinsi gani TBS wamekuwa wakiruhusu shehena ya mafuta yaliyochanganywa na ethanol iingie nchini wakati Tanzania haina utaratibu wa kutumia "blended fuel". Zaidi ya hapo, swali la kujiuliza ni kwa nini TBS waliruhusu kuingia nchini mafuta yaliyochanganywa na ethanol kwa kiasi cha juu sana cha kuharibu magari ya watu.
Original source: IPP media